Denis Law akifunga bao lake maarufu kwa kisigino dhidi ya Man United na kupelekea timu hiyo kushuka daraja. |
Huku United wakiwa wanaongoza kwa pointi 3 dhidi ya City lakini upungufu wa toafuti ya magoli, unaufanya mchezo huo uwe mkali zaidi kwa timu hizi mbili katika derby ambayo inatajwa itakuwa kubwa kama ile ya ya mwaka 1974.
Hapo zamani, City walisafiri mpaka Old Trafford huku wakijua ushindi kwao watafanya mahasimu wao United kushuka daraja.
Denis Law akipongezwa na mashabiki wa City |
Kama ilivyokuwa inaogopwa ndivyo ilivyokuwa, mchezaji wa zamani na shujaa wa United Denis Law alifunga goli maarufu kwa kisigino lilowapa ushindi City wa 1-0, ingawa matokeo haya yalimaanisha United wangekuwa wameshuka daraja.
Wachezaji wa wawili wa pande mbili wameizungumzia mechi hiyo ambayo imekuwa ikimsumbua sana Denis Law na moyo wake.
DENIS LAW - MFUNGAJI WA GOLI LA CITY
Nilijisikia vibaya sana, na hii ilikuwa tofauti na mimi. Baada ya miaka 19 ya kuhangaika kufunga magoli, hili hapa lilikuwa ni moja ambalo nilikuwa sitamani kufunga - nilitamani linsingeingia kwenye nyavu. Iliniuma sana - sikuwa nataka kufunga lile goli.
Hili ni tukio ambalo kila siku limekuwa likinisumbua - kila siku lipo pale na nakumbukwa sana kwa tukio lile - ni aibu kwangu.
Nilicheza na wachezaji wote wa United, walikuwa marafiki zangu, sikuwa nataka washuke daraja. Kilikuwa ambacho labda ningefanya kama dunia ingekuwa imefika mwisho - kiukweli sikujisikia vizuri
Hawakuwa marafiki zangu uwanjani. Tulikuwa tukichezeana rafu. Lakini pindi ilipopigwa filimbi ya mwisho hapo ndio kila kitu kilipobadilika. Nilihisi uchungu sana kuona watu ambao nilicheza nao kwa kipindi kirefu wakiwa na machungu mazito baada ya mchezo kuisha.
Sitoisahau hiyo siku kiukweli inanisumua mpaka leo.
MARTIN BUCHAN - MLINZI WA UNITED
Sitoisahau sura ya Denis Law ilivyokuwa. Ilikuwepo na itaendelea kuwepo kwenye kumbukumbu zangu milele.
Ulikuwa ni uchinjaji wa kikatili kutoka Denis, United tulikua tunashuka daraja kutokana na goli la mchezaji mwenzetu wa zamani.
Ningeweza kuuita mchezo wa Jumatatu ijayo kama derby kubwa kuliko zote tangu mwaka 1974 - United wamejitahidi na wamecheza vizuri sana msimu ambapo walikuwa wameandamwa sana na majeruhi ya wachezaji muhimu kama Nemanja Vidic.
Ni vizuri kuona timu zote zikiwa juu ya msimamo wa ligi lakini sitojaribu kutabiri chochote juu ya nini kitachotokea. Nilishindwa kufanya hivyo nilipokuwa mchezaji hivyo sitofanya hivyo sasa.
No comments:
Post a Comment