Asalam Aleikum
Nikiwa kama mdau wa soka hususan mpenda maendeleo ya mpira wa miguu,kama kawaida kupitia blog yako maarufu ninayoipenda,ningependa kutoa maoni yangu kuhusiana na mechi inayofuata kati ya simba na El Ahl ya sudan,
lakini awali ya yote nachukua fursa hii kawapongeza Wachezaj,viongozi,wanachama na wapenzi wa klabu ya simba kwa mafanikio waliyoyapata kuingia raundi ya pili,naamini kazi kubwa na nzuri imefanyika hivyo hatuna budi kwa ujumla Watanzania wote tukajivunia..Sasa ningependa kueleza maoni yangu niliyokusudia kuyawakilisha leo.
Nimesoma magazeti ya leo upande wa michezo yakieleza juu azma ya mfadhil wa zamani wa simba ndugu Azim Dewji juu ya mpango wake wa kuileta TP Mazembe ili kuipima nguvu simba kabla ya mechi yake ya kimataifa inayofuata.Siwezi pinga nia na melengo mazuri ya mfadhili huyo lakani nafikiri kwa maoni yangu mechi hii kwa wakati huu si muafaka.
Kwa nin nasema hivyo?
Kwanza kabisa licha ya uzoefu wangu mdogo ktk soka nina imani ya kwamba mechi hii ipo karibu sana na mchezo unaofuata yani wiki moja kabla ya mchezo na wasudani na ukizingatia itakuwa ni mechi ya kirafiki kubwa na yenye ushindani.
Pili,sidhani kama simba watakuwa hawafahamu kuwa wana mechi 3 ngumu ndani ya wiki 3.nikimanisha tar 29 dhid ya Ahli,mei 5 mchezo na mahasimu wo yanga na mei 11 wanarudiana na wasudan.Hivyo iwapo watakubali kucheza na mazembe ina mana watakuwa na mech 4 ngumu za ushindan ndan ya majuma manne mfululizo kitu ambacho kitaalamu si kizuri.
Tatu na mwisho,uongozi wa simba lazima utambue wachezaj wanaweza kupata injury na kuiathiri timu yao katika mchezo huo wa kirafiki,kwani nina hakika watacheza kwa kujituma kwa lengo la kupata soko wakifahamu fika timu hiyo inamilikiwa na bilionea Moise Katumbi na ukizingatia kuna wachezaj wawili wametokea hapo ktk mechi kama hiyo ingawa hii ni ya kirafiki.
Kwa kumalizia kabisa simba wakumbuke walimpoteza Sunzu alipoumia mech ya kirafiki dhid ya Tusker wiki moja kabla ya raundi ya pili kuanza na akakosa mech 3 za mwanzon.
wenzetu waliopiga hatua ktk soka wanapokaribia kucheza mechi ngumu wanajipima na timu dhaifu,hivyo basi ni matumaini yangu watakuwa makini ktk maandaliz ya mchezo huo,nawatakia kila la heri Simba.
Shukran
wako kutoka tanga
Nuru Jumbe
Kwanza kabisa napenda kumpa big up bwana Azim Dewji kwa kuangalia team ambayo itaipa Simba uzoefu mzuri wa kisoka kabla ya mechi zake za shirikisho.
ReplyDeleteBwana Nuru Jumbe ana mawazo ya uoga wa kisoka,kitu ambacho si kizuri.Injury wanaweza kupata hata wakicheza na team mbovu,kiujumla injury wakati wowote na wala huwezi kujua inatokea wakati gani,kama ni mwanasoka utalitambua hili,kama si mwanasoka lazima utaona kuwa Simba wakicheza na Mazembe watapata injury,hayo ni mawazo hasi.
Ulaya tunaona mara nyingi,team inacheza week end mechi ngumu ya league,Jumanne au J'tano inacheza tena Uefa Champions League,sembuse Simba kucheza na Mazembe?
Nawashauri wachezaji wa Simba,komaeni mcheze game na Mazembe lazima mtapata kitu fulani ktkt soka na kitawasaidia ktk game zenu za shirikisho,ukizingatia kwamba league yetu ina team chache,mpaka sasa mechi za league mlizocheza ni chache na mbovu,maana ndiyo league yetu mbovu kiujulma.
Mdau kutoka Dodoma,
Mr.BM Yanga daima.
Mimi binafsi nimebarikiwa sana na taarifa hii ya TP-Mazembe kukipiga na Simba, kiukweli naupongeza sana uongozi wa Simba kwa kuona mbali. Mechi hii itawasaidia sana mabeki wa Simba kurekebisa makosa mengi ambayo huwa wanafanya pasipo kuazibiwa, Pia kwa forward na midfielders kwa jinsi watakavyocheza vizuri na kusababisha magoli, au kutengeneza tuu nafasi, itazidi kuwapa kujiamini kucheza vzuri zaidi kwa mechi ya El Ahl. Na pia naamini ni sehemu ya mipango ya timu ya kuongeza kipato kupitia kiingilio. TP-Mazembe haina cha (washabiki hawa ni wapenda soka na hawa ni wapenda yanga)nauhakika pale patafurika tuu, so big up Dewji.
ReplyDeleteshabiki mkubwa wa Blog hii.
Ernest wa Mlandizi.