Josep Guardiola aliifikia rekodi hiyo baada ya kuiongoza Barcelona kwenye jumla ya michezo 146 ya ligi,amabyo ni sawa na asilimia76.8% kwa idadi hiyo ya michezo inabaki kuwa historia ya kocha aliyepata mafanikio makubwa kwenye historia ya klabu hiyo,
Asilimia ya michezo ambayo Frank Rijkaard aliiongoza Barcelona kupata ushindi ni 56.9%.
Pep Guardiola ameishuhudia Barcelona ikipata vichapo kwenye michezo kumi tu kati ya michezo 146 ikipata matokeo ya sare kwenye michezo 24 huku timu yake ikifunga jumla ya mabao 392 na kufungwa mabao 103. Kwa kipindi hicho cha misimu minne Barcelona ya Guardiola imekusanya jumla ya pointi 354.
Ni Johan Cruyff pekee aliyeiongoza Barcelona kushinda michezo mingi ktk kipindi chake akiwa kocha, mdachi huyo aliiongoza Barca kushinda jumla ya michezo 183 kwenye michezo 306.
No comments:
Post a Comment