Search This Blog

Tuesday, April 24, 2012

Chelsea wana nafasi finyu ya kupata ushindi kwenye mchezo wa leo


Siku saba baada ya takwimu za shuti moja bao moja kwa Chelsea na mashuti zaidi ya 24 bila mabao kwa Barcelona kwenye uwanja wa Stamford Bridge,  timu hizi zinarudiana kwenye uwanja wa Nou Camp.
Barcelona wamekuwa kwenye wakati mgumu baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo huku nyota wake Lionel Messi akisindwa kung'aa kwenye kwenye mechi zote mbili.
Chelsea walipoifunga Barca mapema wiki iliyopita wengi waliona kuwa timu hii toka London imepanda baiskeli ya miti na Barcelona ingeshinda kiwepesi mchezo wa marudiano . Hata hivyo kipigo cha kwenye El Classico kimewaweka Barca kwenye hali tofauti ya kisaikolojia ambayo inaweza kuwa sababu ya aidha kushinda au kufungwa kwenye mchezo wa marudiano.
Ukirudi nyuma na kutazama sababu ambazo zinaweza kuwa zimeipelekea Barca kufungwa michezo yote miwili na kuzichanganya kwa pamoja hapa ndio unapoweza kugundua hali ngumu waliyo nayo Barca hii leo.
Kwenye mechi ya jumatano iliyopita mfumo waliotumia Chelsea na bahati kwa pamoja viliwasaidia vijana wa Di Matteo. Mfumo aliotumia siku hiyo ulikuwa rahisi,kuta mbili za wachezaji wanne kila moja nyuma ya mpira na kujaribu kupunguza nafasi ya Barca kufaidi kumiliki mpira kuanzia katikati mwa uwanja kuelekea liliko lango la Chelsea .
 Pamoja na hilo , Di Matteo aliwaelekeza viungo Raul Meireles na John Obi Mikel kuhakikisha wanakufa na Lionel Messi ,Xavi na Andres Iniesta huku Ramires akifanya kazi ya kuua mashambulizi ya upande wa kulia aliko Mbrazil mwenzie Dani Alves . Mbinu hizi zilifaulu kwa kusaidiwa na ari waliyokuwa nayo Chelsea kisaikolojia pamoja na bahati iliyokuwa upande wao kwani ukiachilia mbali jinsi Chelsea walivyoshinda huwezi kusahau mara ambazo Barca waligongesha miamba na mara ambazo Petr Cech alifanya kazi ya ziada kuokoa au mabeki kina Ashley Cole wakiondosha hatari langoni mwao.
Kwenye mchezo dhidi ya Real, Barca waligharimiwa sana na kuwakosa wachezaji mbadala wanaoweza kufanya kazi ya ufungaji zaidi ya Lionel Messi. huwezi kuacha kufikiri kuwa nafasi mbili alizopata Christian Tello na kushindwa kuzitumia zingekuwa zimetumiwa vyema na mtu kama Pedro au David Villa .
Pengo la David Villa limeonekana sana kwenye El Classico na kuna kila uwezekano kuwa endapo Chelsea watafuzu basi pengo hilo litaonekana kwenye mchezo huo pia. Pamoja na hayo Real walikuwa na aina ya uzoefu na uwezi wa kutumia nafasi chache za kufunga walizozipata jambo ambalo si timu nyingi zinazocheza na Barca zinafanya.
Ukiwaangalia Barcelona wenyewe kama Barcelona kuna baadhi ya viashiria mbalimbali ambavyo vilionyesha kuwa hawako mchezoni siku ya jumamosi. Lionel Messi hana kawaida ya kuwa mlalamishi lakini alilalama kwa waamuzi kuliko mchezaji yoyote siku ile na hata Xavi na wengineo walikuwa wanaonekana kupagawa jambo ambalo linakufanya uhisi kuwa ile hali ya woga ambayo timu pinzani inakuwa nazo ikicheza dhidi ya Barca inakuwa nayo imehamia kwa Barcelona wenyewe.
Safu ya ulinzi nayo imekuwa tatizo kubwa. Carles Puyol anastahili kubeba lawama  kwenye mabao yote matatu ambayo Barca imeruhusu kwenye michezo miwili iliyopita na endapo atacheza tena huenda Di Matteo akawaelekeza wachezaji wake kupeleka presha kwenye upande wake .
Hata hivyo Barcelona wanabaki kuwa timu yenye uwezo hata pale ambapo wanapitia kwenye kipindi kigumu kama livyokuwa kwenye msimu huu na quality yao pekee ambayo dhahiri shahiri ni bora kuliko ya Chelsea inaweza kutosha kugeuza matokeo.
Kikubwa kitakachoamua mchezo ni hali ya kisaikolojia ya wahezaji a Barcelona.
Wanapaswa kuacha yaliyotokea kubaki huko nyuma yaliko na ku-deal na mchezo wa leo kama wa leo . Endapo wataruhusu kuingiwa na hali ya woga kwa maana wanaweza kufungika kirahisi. Kwa hali ya kawaida  Barcelona ni washindi na hiki ni kitu ambacho wahezaji wanaingia nacho uwanjani kwa kuwa wana "winning mentality" . Ila hiyo hiyo mentality inaweza kuondoka na swali ambalo kila mmoja anajiuliza ni kama hiyo winning mentality ipo baada ya michezo miwili migumu ambayo Blaugurana wamefungwa?
Chelsea wana nafasi finyu ya kupata ushindi kwenye mchezo wa leo na nafasi pekee kubwa waliyo nayo ya kusonga mbele ni kutafuta bao la ugenini huku wakilinda kwa nidhamu kama waliyolinda nyo kwenye mchezo wa Stamford Bridge .
Tetesi toka kwenye magazeti ya Hispania kwa masaa 24 yaliyopita zimekuwa zikisema kuwa Lionel Messi hayuko kwenye physique nzuri , pengine michezo imekuwa mingi mfululizo pengine kama ilivyo kwa kila binadamu wachezaji wa Barcelona wamechoka baada ya kuwa na msimu ambao mambo yamekuwa magumu kwao ?
Haya ni maswali ambayo majibu yake yatapatikana ndani ya masaa machache yajayo

7 comments:

  1. Napingana sana na uchambuzi wako, kwenye mpira lolote laweza kutokea, wewe kusema kuwa Chelsea wana nafasi finyu hayo ni mapenzi yako binfasi...kuna jamaa mmoja wa BBC huwa nampenda sana anapofanya uchambuzi wake Pat Nevin kila mara yupo fair sana...ni hilo tu, Chelsea anaweza kufungwa na Barcelona pia anaweza kufungwa kwani wao ni kina nani?
    Mdau
    Washington

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli mdau kaka Shafii umeumbuka mpira dakika 90

      Delete
  2. Kaka nilisema asubuhi sikubaliani nawe, okay Chelsea hao kwenye finali....
    mdau
    Washington

    ReplyDelete
  3. Mi nadeclare interest..
    Timu yangu imeingia fainali kwa kuivua ubingwa timu bora kabisa duniani..

    Ila nawashangaa mashabiki wa timu nyingine za EPL(wa hapa TZ) ambao wanashabikia Barca hata inapocheza na Chelsea...

    ReplyDelete
  4. HAHA DAUDA NADHANI UCHAMBUZI WAKO FEKI UMEDHIHIRIKA SASA.SIKU NYINGINE UJIFUNZE KUCHAMBUA NA SIO KUBEZI KUWA FULANI KWA KUWA KUNA FULANI WATASHINDA.
    TRY AGAIN MAY BE NEXT TIME BRO.

    ReplyDelete
  5. watu weng watasema sana kutolewa kwa Barca na Chelsea, kwa upande wangu naamin kwamba Barca bado ni wazuri sana na wanastahili pongezi, wametolewa si sababu soka lao limeisha isipokuwa ni sababu ya uchovu wa mechi nyingi walizocheza msimu uliopita, unapocheza mech nyng uchov unaweza kukufanya ukose ile hali ya ushindi, hicho ndicho kilichowatoa Barca, ni mara chache sana kuona Barca wakikosa magol kias kile, angalia darajan pia na pale kwao jana. all in all me ni REAL MADRID damu,
    nakukumbusha kuwa hili kombe nyumban kwake ni Santiago Bernerbeu pale Madrid, usishangae sana utakapoona Jose analibeba kombe hili.

    ReplyDelete
  6. wamecheza mechi nyingi ki vp?kati ya uingereza na spain ni nchi gani ina vkombe vngi?spain kuna vi wili na uingereza kuna vi tatu.ni kwamba barc kumfunga chelsea huwa ni ngum,coz chelsea ina wachezaji wanao kamia mechi na si mchezaji kama timu nyingine,we angalia wacheza kumi wamewazuia timu kama barc,na walikuwa nyuma kwa mabao mawili,ila wali2lia nakusawazisha yote,

    ReplyDelete