Wachezaji wa Chelsea wamehaidiwa na bosi wao Roman Abramovich kupata bonasi ya £10 million ikiwa watafanikiwa kuifunga Barca, kisha kwenda fainali na kuchukua ubingwa wa kwanza wa ligi ya mabingwa wa ulaya katika historia ya timu hiyo.
According to gazeti la The Sun la Uingereza ikiwa Chelsea watafanikiwa kuchukua kombe hilo watapewa kiasi hicho cha fedha huku manager wao wa muda Roberto Di Matteo nae hatoondoka mikono mitupu.
Kila mchezaji wa kikosi cha wachezaji 25 atapokea kiasi cha £350,000 ikiwa watafanikiwa kubeba kombe la ulaya pale Allianz Arena mwezi ujao.
Roberto Di Matteo ambayo bado hajapokea ongezeko la mshahara ukiachana na 1.2millionaliyokuwa akilipwa kwa mwaka kama kocha namba 2 nyuma ya Villas Boas.
Bonasi yake itajadiliwa katika kikao cha baina yake na mmiliki wa The Blues.
Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kiungo huyo wa zamani wa klabu atavuta mkwanja unaofikiwa paundi 500,000 kama shukrani kwa kugeuza msimu wa Chelsea - japokuwa bado hajapewa uhakika wa kupewa kazi ya moja kwa moja kama kocha mkuu.
Di Matteo amefungwa mechi moja tu tangu amrithi Villas Boas huku akiwa aemcheza mechi 14.
No comments:
Post a Comment