Ikitokea klabu ya Simba ikafanikiwa kuwatoa wapinzani wao katika kombe la shirikisho,
ES Setif ya Algeria katika Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, itaingia hatua ya mwisho ya mchujo ambako itamenyana na ama El Ahly Shandy ya Sudan au Ferroviario de Maputo ya Msumbiji, ambayo ina kipa Mtanzania, Muharammi Mohamed ‘Shilton’ aliyewahi kudakia Simba. Kuna uwezekano mkubwa Simba ikacheza na Al Ahly, kwa sababu imeanza kwa ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Ferroviario.
Simba ikifanikiwa kumtoa na mpinzani wake ajaye, moja kwa moja itafuzu kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ikiwa timu ya kwanza ya Tanzania kucheza hatua hiyo.
Tanzania imewahi kufikisha katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa tu, mara mbili mwaka 1998 Yanga na 2003 Simba wenyewe.
Mwaka 2007 Yanga ilikaribia kuingia hatua ya makundi ya Makundi ya Kombe la Shirikisho, lakini ikatolewa na El Merreikh ya Sudan, wakati mwaka jana pia Simba ilikaribia kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo, ikatolewa na Daring Club Motema Pembe ya DRC.
Kama wakifanikiwa kufika hatua ya makundi ya michuano hiyo, Simba watapewa donge nono la dola za Kimarekani 150, 000, zaidi ya Sh. Sh Milioni 250,000 za Tanzania.
No comments:
Post a Comment