Baada ya kufunga magoli mawili wikendi iliyopita, Cristiano Ronaldo sasa anashika namba 10 katika listi ya wafungaji bora wa muda wa Real Madrid.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United mpaka sasa ameshacheza mechi 131 akiwa na Real Madrid, akifunga magoli 33 msimu wa kwanza, 53 msimu wa pili, 45 akifunga mpaka sasa katika 2011-12. Na bado hajamaliza, bado ana mechi 12 zilizobakia katika la liga huku timu yake ikiwa katika hatua ya robo fainali ya Champions league.
THE TOP 10 GOALSCORERS FOR REAL MADRID |
|
Ikiwa Ronaldo atabakia Madrid msimu ujao, inaaminika Ronaldo atapanda hadi nafasi ya 6 katika listi ya wafungajibora wa muda wote wa klabu hiyo, akiwapita Emilio Butragueno, Paco Gento, Pirri na Amancio.
Wakati huo huo pia Cristiano Ronaldo ataweka rekodi mpya katika ligi hiyo ikiwa atafanikiwa kufunga goli katika mechi ijayo dhidi ya Mollorca, atakuwa ndio mchezaji wa kwanza kuzifunga timu zote za la liga katika msimu mmoja.
No comments:
Post a Comment