Huku soka likiingia katika mfumo wa kuongozwa na fedha zaidi, tabia ya kukuza wachezaji wao wenyewe hasa kwa vilabu vikubwa imeanza kupungua sana, kwa kuwa wamekuwa wakitaka mafanikio ya haraka, lakini kuna wachezaji wawili ambao ni mfano bora wa wachezaji waliotoka kutoka ngazi ya chini mpaka kwenye level ya juu ya mafanikio katika klabu zao.
Paolo na Ryan Giggs ndio wanaume wawili ambao majina yao unaweza kuyafikiria wakati atakapotajwa mtu ambaye ni 'one-club man' kwa sababu wachezaji hawa wote wawili wametumia muda wao wote wa kucheza soka katika zao AC Milan na Manchester United.
Usiku wa jumatatu, Giggs alivunja rekodi ya Maldini kwa kucheza mechi nyingi kwa timu barani ulaya, akicheza mechi rasmi 903 na United miaka 21 baada ya kukitumikia kikosi cha kwanza cha Red Devils na haonekani kwamba ataacha kucheza hivi karibuni, akiwa na lengo la kutimiza michezo 1000 na Manchester United.
Huku wachezaji wa kisasa wakiwa wanahama kutoka klabu moja mpaka nyingine, Maldini na Giggs wametengeneza historia ambazo ni vigumu sana kuja kufutika katika mfumo wa soka la kisasa.
Mtandao wako bora wa michezo unakuletea namna gani na ijnsi gani magwiji hawa wanatofuatiana na kufanana vipi kupita takwimu mbalimbali.
| RYAN GIGGS | FACT FILE Appearances: 903 Honours: 33 |
Years active: 1991-present Mwaka alioanza kucheza: 1991-mpaka sasa Magoli aliyoyafunga: 163 Tuzo: PFA Players' Player of the Year 2008-09 BBC Sports Personality of the Year 2009 OBE for services to football - 2007 Ukweli: Anabakia kama mchezaji pekee kucheza na kufunga katika kila msimu wa premier league. Ukweli: Anashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi kwenye Premier League. | GIGGS IN QUOTES "Giggs ni mchezaji daraja la juu duniani." - Zinedine Zidane "Nimelia mara mbili tu kwa sababu kumuangalia mcheza soka, wa kwanza alikuwa RobertoBaggio na wa pili ni Ryan Giggs." - Alessandro Del Piero "Eric Cantona ni mchezaji mkubwa na bora lakini sio kama Giggs." - Johann Cruyff |
Ni klabu chache sana duniani ambazo zimepata mafanikio katika ligi ya nyumbani na ulaya kama ambavyo Manchester United imepata katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Wameshinda EPL mara 20, makombe mawili ya champions league, huku wakichukua makombe ya FA na Carling Cup. Ilimchukua Sir Alex Ferguson miaka kadhaa kuibadili United kuwa washindani wa makombe na Giggs amekuwepo around tangu kipindi Fergie akianza kuleta mapinduzi Old Trafford. Akicheza mechi yake ya kwanza akiwa na miaka 17 on March 1991, na United wakashinda kombe la premier league msimu uliofuatia. Takwimu hii inaonyesha kwa The Welshman ndio mchezaji pekee aliyecheza na kufunga katika kila msimu wa premier league tangu ilipoanza mwaka 1991. Giggs alifunga goli lake la kwanza dhidi ya Manchester City in May 1991, huku goli lake la mwaka 1998-99 kwenye nusu fainali ya FA Cup dhidi ya Arsenal litakumbukwa kama moja ya magoli bora kabisa kuwahi kufungwa kwenye FA Cup, aliwatoka karibia wachezaji wote wa Arsenal kwenda kumfunga David Seaman kisha kuvua shati akionyesha kifua chake kilichaa nywele. Nahodha huyo wa zamani wa Wales alishinda medali yake ya kwanza ya Champions league msimu huo huo akiwa moja ya wachezaji muhimu wa United ambao walishinda makombe matatu, japokuwa aliandamwa na majeruhi pia. Ingawa aliwahi kupata majeruhi alipokuwa mdogo, kuepeuka kwake majeruhi ya muda mrefu kulimfanya aweze kucheza at least mechi 32 kila msimu tangu msimu wa 1991-92, lakini haonekanai sana kama amekuwa affected na uchovu, akiwa ameshacheza mechi 27 msimu huu. Baada ya kuwa sehemu ya matukio ya kihistoria, lakini kubwa kuliko ni kuwa mmoja ya wachezaji mhimu waliowamaliza utawala wa Liverpool kama klabu iliyofanikiwa zaidi nchini England baada ya United kuwafikia na kuwapita Liverpool kwa kuchukua vikombe vingi vya premier league. Wakichukua mara 19.
| PAOLO MALDINI | FACT FILE Appearances: 902 Honours: 26 |
Miaka aliyocheza: 1985-2009 Magoli aliyofunga: 33 Tuzo: Champions League Best Defender 2007 Uefa Team of the Year 2003 & 2005 Ballon d'Or Bronze Award 1994 & 2003 Ukweli: Amecheza mechi nyingi za Champions League - 168. Ukweli: Amecheza mechi 23 za World Cup matches akiwa na Italy, akipoteza mechi tatu tu. | MALDINI IN QUOTES "Zidane alikuwa kiboko bila shaka lakini Paolo Maldini alikuwa ndio kipenzi changu." - Sir Alex Ferguson "Ni moja ya wachezaji bora ambao nimewahi kuwashuhudia" - Marcello Lippi |
Jina la 'Maldini' lilikuwa sio maarufu kihivyo kipindi kijana wa 16-year-old Paolo alipocheza mechi yake ya kwanza kwa Milan mwaka 1985. The youngster alikuwa mtoto wa kiume wa Cesare Maldini, mchezaji wa Milan katika miaka ya 1950s and 60s, kabla haifundisha timu hiyo katika miaka ya 70, hivyo Maldini alikuwa amekulia ndani ya klabu hiyo. Kama ilivyokuwa kwa Giggs, haimkuchukua muda mrefu kabla ya Maldini hajaanza kuthamniwa na kuaminiwa kwa kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza, akicheza mechi 27 za Serie A katika msimu wake wa kwanza na mechi nyinginwe 13 katika mshindano mengine.
Ndani ya kipindi chake cha kucheza soka kwa miaka 25, Maldini alishinda makombe saba ya ligi, huku kombe la kwanza akishinda in 1987-89 season, lakini kombe la msimu wa 1991-92 ndio la kukumbukwa zaidi kwake kwa sababu AC Milan walimaliza msimu bila kupoteza mechi chini ya ukuta wa Maldini, Franco Baresi, Mauro Tassotti and Alessandro Costacurta was becoming more imperious by the year. Makombe 7 ya ligi katika miaka 25 yanaweza kuonekana madogo lakini ni wachache wanaoweza kumfikia legend huyu linakuja suala la ligi ya mabingwa wa ulaya, akiwa ameshinda makombe matano katika miaka ya 1988, 1989, 1994, 2003 na 2007. Mchezaji wa Real Madrid Francisco Gento Alishinda makombe sita ya European titles with the Spanish giants katika miaka ya 50s and 60s, mchezaji pekee aliyemzidi Maldini, huku wote wawili ndio wakiwa wamecheza fainali nane, idadi kubwa kuliko mchezaji yoyote katika historia ya kombe hilo.
****Jiulize ni wachezaji wangapi wataweza kufikia mafanikio ya watu hawa wawili kwa kucheza soka la kiwango katika mechi zaidi ya 900.?******
No comments:
Post a Comment