Search This Blog

Monday, March 19, 2012

OLYMPIAKOS VS PANAITHINAIKOS: MASHABIKI WAWASHA MOTO UWANJANI UGIRIKI - VURUGU KUBWA ZAIBUKA.


 
 
 
The Athens derby kati ya mahasimu Panathinaikos na Olympiakos ilivunjika jana jumapili baada ya vurugu kubwa kuibuka kati ya mashabiki na polisi.



Police wametangaza kwamba watu 57 wamehojiwa wakati 20 walikamatwa na kutiwa ndani. Pia polisi 9 walijeruhiwa vibaya.
Vurugu kati ya polisi na mashabiki zilianza kabla ya mchezo, wakati mamia ya washabiki vijana wakiwa hawana tiketi walipojaribu kuingia uwanjani. Vurugu ziliendelea muda wote wa mchezo na kusababisha kipindi cha pili cha mchezo kusubiri kwa dakika 35.


Group la mashabiki karibia 200 waliokuwa wamekaa katika VIP, karibia na sehemu ya kuingilia vyumba vya mapumziko wakiwa na silaha tofauti ndio walioanza kuanzisha vurugu uwanjani baada ya kuanza kuwashambulia baadhi ya polisi waliokuwa wakilinda amani uwanjani.


Katika kipindi cha pili mashabiki wa Panathinaikos walianza kuchoma moto siti uwanjani, kabla ya refa Tassos Kakos kutimua uwanajani baada ya mabomu ya moto kuanza kurushwa uwanjani na mashabiki kuelekezwa kwa polisi na wapiga picha.
Hadi wakati huo wageni Olympiakos walikuwa mbele kwa bao 1-0 kupitia goli la Djamel Abdoun.


Katika mechi hiyo hakuna shabiki hata mmoja wa Olympiakos aliyeruhusiwa  kuhudhuria mechi hiyo katika uwanja wa Olympic kutokana na utaratibu na sera za kutoruhusu mashabiki wa timu ngeni kuhudhuria mechi hizo ili kuepeusha vurugu.

No comments:

Post a Comment