Search This Blog

Tuesday, March 27, 2012

MUTESA MAFISANGO: NIYONZIMA HAFIKII UWEZO WA HARUNA MOSHI BOBAN.


Midfielder wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango, anayechezea Simba SC, anaamini Haruna Moshi 'Boban' ni bora kuliko Haruna Niyonzima wa Yanga. Akizungumza na tovuti ya Simba, Mafisango alisema yeye amecheza na wachezaji wote hao wawili katika timu moja na pengine ndiye mtu pekee hapa nchini anayewajua wachezaji hao wawili kindakindaki.

“Nimecheza na Haruna katika timu ya taifa ya Rwanda na ninacheza na Boban hapa Simba. Bila ya upendeleo wowote, Boban ni zaidi ya Niyonzima. Hii ni kwa uwezo binafsi (technic) na kiufundi (tactic),” alisema. 

Alisema ukitaka kujua tofauti ya Boban na Niyonzima angalia tofauti iliyopo kwenye nani mwenye pasi nyingi zilizosababisha magoli na yupi mwenye magoli mengi ya kufunga baina ya wachezaji hao wawili.

“Niyonzima anajua mpira. Lakini Boban ana mambo mengi ya ziada. Pasi nyingi za Niyonzima si za hatari lakini za Boban ni za hatari kwa maana zinaweza kusababisha lolote lile. Si lazima iwe pasi ya kuzaa goli lakini pia inaweza kuwa pasi iliyosababisha pasi ya bao,” alisema. 

Alisema jina la Niyonzima limepata umaarufu kwa kuwa pengine ndiye mchezaji wa Yanga mwenye kiwango cha juu zaidi kuliko wengine, lakini la Boban halivumi sana kwa vile kuna mastaa wengi Simba.

Simba kuna Mafisango, Kazimoto, Kaseja, Kapombe, Sunzu na Boban. Wote hawa ni wachezaji wa kiwango cha juu na wanagawana sifa. Lakini inaonekana kwa Yanga nyota ni Niyo pekee na ndiyo maana anatangazwa sana ila mimi nakuambia Boban ni zaidi yake.

Mafisango amefunga jumla ya mabao saba kwenye Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na ndiye mchezaji wa kiungo aliyefunga mabao mengi zaidi msimu huu.

4 comments:

  1. kwli mafisango kachemsha kwa hili mimi ni simba ila yule mtoto niyonzima jaman ni hatar anateleza kama samaki majin anautaka anautupa anaufuata anapiga chenga ana kasi ana uwezo wa kufunga boban ni mzur ila hana kasi anapokuwa uwanjan harudi nyuma kuchukua mipira na pumzi yake ni yakubip. AU MAFISANGO ANABIF NA HUYO NIYONZIMA KISA KAMNYANGANYA NAMBA RWANDA

    ReplyDelete
  2. Mi naungana na mafisango, haruna niyonzima anpiga square pass zaidi ila boban anapiga killer pass, mara nyingi square pass hazina madhara sana kuliko killer pass ambazo ni aidha za goli au moja kabla ya goli, hii inadhihirisha wazi na idadi ya magoli yanga wanayofunga, mara nyingi ni moja wakiwakuta dhaifu ndo wanapiga kadhaa, zamaleki si timu nzuri kwa sasa km niyonzima angekuwa anapiga killer pass au yy mwenyewe kufunga km boban basi siku ile goli zingekuwa nying, huo ni mtazamo wangu.

    ReplyDelete
  3. There is no midfilder like Niyonzima in Tz,Niyo is a complete set in a midfild zone,he offers every service needed in the midfild.Always Niyo shines every game,how about that marijuana taker?.Mafisango wa just enjoying the freedom of speech.In fact Niyo is unique and is not in the same class with Boban.By Gard.

    ReplyDelete
  4. mafisango kazungumza sports tupu ukiangalia uwezo wa boban na niyonzima utaona tofauti kwanza boban ana uwezo wa pasi za mwisho ambazo ht ukimtengea chiz lzm afunge angalia pasi za niyo nying huwa c za hatari kingine niyonzima apendi akabwe kitu ambacho ktk soccer la leo hakipo angalia mechi ya yanga na azam ktk kombe la mapinduz niyonzima alikabwa na humud mpk akakasilika. Niyo anataka acheze peke yake aisibugiziwe tofaut na boban anataka mcheze kwa kushindana waulize wa senegal kule ccm kirumba watakwambia haruna moshi nan... @kwanja from boom fc ilala

    ReplyDelete