Kwa mara nyingine Wekundu wa Msimbazi wameendeleza rekodi yao nzuri kwenye mechi za kimataifa kwenye uwanja wa nyumbani.
Kabla ya mchezo watu wengi walidhani mchezo ungekuwa mgumu hasa kutokana na aina ya timu waliyokuwa wanakutana nayo.
Rekodi za ES Setif zinaonyesha kuwa ni timu kubwa na yenye uwezo ambao kwa hali halisi ya tofauti iliyopo kwenye soka la Algeria wanakotoka Setif na Tanzania wanakotoka Simba unaona kabisa kuwa wenyeji wa Mchezo wa jumapili walikuwa na mlima mrefu wa kupanda kupata matokeo mazuri.
Hata hivyo ukiangalia zaidi takwimu za Setif utagundua kuwa ni timu ambayo haina rekodi ya kufanya vizuri ugenini na Simba walidhihirisha ukweli unaozungumzwa na takwimu hizi.
Setif waliingia mchezoni wakiwa na wazo la kuepuka kufungwa, labda kupata sare ili wajiweke kwenye mazingira mazuri ya kumaliza kazi kwenye mchezo wa nyumbani kama ambavyo wamekuwa wakifanya.
Walicheza sana kwenye eneo lao huku wakipanda kufanya mashambulizi ya kushtukiza pale ambapo Simba walikuwa wame-commit wachezaji zaidi mbele. Hata hivyo mfumo ambao mwalimu wa Siba Milovan Curkovic aliutumia siku hiyo uliwafanya Simba kucheza kwa ku-balance uwanja mzima kwa maana ya nafasi moja hadi nyingine. Simba walicheza wakitumia mfumo wa 4-2-3-1 ambapo mabeki waliokuwa wakimlinda Kipa Juma Kaseja walikuwa Shomari Kapombe , Amir Maftah ,Juma Nyoso na Kevin Yondani, kwenye kiungo walicheza Mwinyi Kazimoto na Patrick Mafisango . Mbele ya viungo hawa walikuwepo maforward ambao kazi yao kubwa ilikuwa kusaidia mashambulizi , Emannuel Okwi na Salum Machaku wakicheza pembeni na Haruna Moshi Boban akicheza katikati yao na mbele alikuwepo Felix Sunzu.
Aina ya mfumo huu ilikuwa sahihi kwa mchezo ambao Setif walicheza kwa sababu kulikuwa na ulinzi w kutosha kwa mabeki toka kwa viungo wawili waliocheza kati yao ambapo akati timu ikiwa inashambuliwa jambo ambalo lilitokea kwa nadra sana mmojawapo kati ya Mwinyi na Mafisango angeshuka kusaidia au wakati mwingine hata wote wawili na kujenga ukuta wa wachezaji sita nyuma ya mpira.
Wakati Simba wakishambulia wachezaji hawa wawili pia walikuwa wakiongezeka na kufanya maforward kuwa watano jambo ambalo liliwafanya Simba kuonekana wako wengi huku waki-flow bila ya upande wowote kuelemewa. Hili lilitokea kwa urahisi kwa sababu karibu muda wote Setif walikuwa nyuma wakijaribu kutuliza presha, wakimiliki mpira walikuwa wanapiga pasi fupi huku wakiwa na tempo ya chini sana pengine wakiepuka kuchoka na mara nyingi Mwinyi Kazimoto au Mafisango walikuwa wakinyang'anya mipira katikati ya uwanja na kuanzisha upya mashambulizi.
Simba walitengeneza nafasi karibu nne za wazi kwenye kipindi cha kwanza ambazo labda kwa bahati mbaya, ukosefu wa umakini au kukamia kupita kiasi hawakuzitumia kutengeneza magoli na ndio maana kipindi cha kwanza kiliisha kwa matokeo ya bila kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa aina ya mchezo ule ule kama wa kipindi cha kwanza tofauti pekee ikiwa kwa simba kuongeza kasi na wingi wa mashambulizi, labda kwa sababu ya ile "urgency" ya kutaka kupata matokeo kwenye mchezo wa nyumbani.
Haruna Moshi Boban alikuwa aki-link vizuri na Emanuel Okwi pamoja na Salum Machaku huku Machaku na Okwi wakibadilishana wingi mara kwa mara kujaribu kuwachanganya mabeki wa Seif . Beki wa Kati wa Setif alikuwa akimkamia sana mshambuliaji wa Simba Felix Sunzu. Kwa vyovyote lazima Setif walikuwa wamefanya "homework" ya kuifanyia ushushu Simba na kugundua kuwa Sunzu ni mtu muhimu kwenye ufungaji na ndio maana walimbana kama walivyombana.
Presha ilizidi kuongezeka kwa Setif na Simba waliweza kufunga mabao mawili katika kipindi kisichopungua dakika 10. Bao la kwanza lilianzia upande wa kushoto ambako Emmanuel Okwi alikokota mpira na kucheza pasi za kugongeana na Boban na alipofika hatua chache nje ya eneo la hatari alipiga shuti hafifu ambalo kwa mazingira ya kawaida lingeweza kuokolewa lakini golikipa hakuliona vizuri kwani msitu wa mabeki wake walimzinga na hivyo mpira ukatinga wavuni.
Bao la pili lilitokana na Free kick ya Salum Machaku ambayo ilipanguliwa na kipa wa Setif na Haruna Moshi Boban alimalizia rebound na kuipa Simba bao la pili. Baada ya hapo Setif walilazimika kutoka kwenye nusu yao ya uwanja kwenda kushambulia na kutafuta bao muhimu la ugenini lakini defence ya Simba ilisimama imara na kuhakikisha kuwa hakuna hatari yoyote inayofika kwenye lango lao.
No comments:
Post a Comment