Search This Blog

Wednesday, March 28, 2012

MBWANA SAMATA ATEGUKA BEGA - KUKAA NJE KWA TAKRIBANI SIKU 10

Straika wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samata atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku baada ya kuteguka bega la mkono wa kushoto. Samata aliteguka bega hilo wakati timu yake ya TP Mazembe ya DR Congo ilipokuwa ikicheza dhidi ya timu ya Power Dynamos ya Zambia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye uwanja wa Arthur Davies mjini Kitwe, Zambia.

Mshambuliaji huyo kijana ambaye mashabiki wa TP Mazembe wanamuita 'Samagoal' aliumia wakati alipokuwa akitaka kufunga bao, ambapo aliangushwa kwenye eneo la hatari na beki wa Dyanamos, lakini mwamuzi hakutoa penati wala kadi nyekundu.

Kutokana na kuumia huko katika dakika ya 61, Mbwana Samata alilazimika kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Deo Kanda.Hivi sasa Samata yupo katika hospitali ya TP Mazembe akifanyiwa uchunguzi zaidi baada bega hilo kuendelea kumsumbua, ambapo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku 10. 

Katika mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa matokeo ya bao 1-1, bao la TP Mazembe lilifungwa na Mbwana Samata katika dakika ya 16, huku mchezaji huyo akiwa anaifungia bao TP Mazembe katika kila mechi anayocheza na akiwa na uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.


1 comment:

  1. HUYU MCHEZAJI NI ILE EXPENSIVE CATEGORY AMBAYO INATAKIWA KUIPA MUDA KUFANYA MAKUBWA, THE WAY ANAVYO-PERFORM AKIWA NA WACHEZAJI KAMA TRESSOR MPUTU NA KUWEZA KUFUNIKA MPAKA AKAITWA "SAMAGOAL" ITS VERY RARE TO TANZANIA FOOTBALLERS, TUWAPE POSSITIVE SUPPORT WACHEZAJI WETU NAO WATATUWAKILISHA KAMA VILE TUNAVYO-WISH. BRAVO SHAFFII KWA KAZI NZURI.

    ReplyDelete