Mimi ni mdau wa soka katika mkoa wa Tanga na Mshabiki wa Vasco, nina masikitiko makubwa na uendeshaji wa ligi ya mkoa wa Tanga mpaka kufikia hatua hii iliyofikia.
Kwa kuanzia katikaki ya ligi hiyo, nisichukue muda mwingi kwa kuelezea jambo hilo kwani tangia mwanzo wa ligi ilijionesha mapema kuwa kuna timu ambayo inatakiwa na sasa tumechoshwa na tumeamua kusema ili kuokoa soka la mkoa huu wa Tanga na Tanzania kwa jumla.
Ni kuhusu ubebwaji wa timu ya African Sports ambayo inacheza ligi ya Taifa ngazi ya Mkoa wa Tanga. Timu hiyo inawachezesha wachezaji ambao wapo ligi daraja la kwanza Zanzibar inayoendelea sasa hivi. Ushahidi wahilo tunao, kwa kumuelezea mchezaji mmoja ambaye anaitwa Saidi Wambuje ambaye alikatiwa Rufaa na timu ya Monga F.C kwa mujibu wa sheria ya ligi hiyo na vielelezo vikapelekwa na ikaonekana ni kweli simchezaji halali kwao, na rufaa hiyo kabla ya kusikilizwa kulikuwa na mechi nyingine dhidi ya Monga F.C na Viva F.C lakini cha ajabu wachezaji wa wa timu zote mbili wakafika uwanjani isipokuwa viongozi wa Timu ya Viva FC hawakufika kiwanjani na kadi za wachezaji wa Viva zikafichwa ili mchezo huo usifanyike kwa lengo kuipa ushindi timu ya Monga F.C ili wapuuzie rufaa yao dhidi ya African Sports maanake kama ingekaliwa rufaa hiyo African sport angetoka kwenye mashindano lakini Monga F.C wakarudishiwa fedha zao (TDFA) wakaacha kuikalia rufaa kisingizio timu mkataji rufaa na mkatiwa wote wamepata nafasi.
Baada ya matokeo hayo Monga FC wakapewa Point 3 na kua na jumla ya 11, nao African Sports ambao walikuwa wacheze na City Center ambayo mechi hiyo ilikuwa ni muhimu sana kwao ili kupata nafasi ya kusonga mbele lakini mchezo huo haukuchezwa kisingizio timu pinzani imechelewa kitu ambacho sio chakweli wakafikisha point 11 nao timu ya Air shooting ikafikisha point 10 na katika kundi zilitakiwa timu 2.
Air shooting wakaandika barua ya malalamiko baada ya kuona kua kunatimu za makundi mengine wamepewa nasafi ya best loser lakini timu ya Air shooting wenye point 10 wakaachwa wakachukuliwa wenye point chache kutoka wilayani kwa sababu ya kutakakura nyingi kutoka kwenye wilaya. Haikuishia hapo ratiba ikapangwa tena kwa zengwe kwa lengo la kuibeba African Sports na timu zote 3 zilikapangwa kundi moja mbali na uchezeshaji mbovu wa marefa, timu ya African sports ndio ilianzakucheza kwenye kundi hilo na ilicheza mechi mbili lakini timu iliyochenza mechi mbili za mwanzo ikiwa ya mwisho kumaliza katika mechi nne (4).
Tukiachana na hilo kutokana timu kutokuwa na uwezo wa wachezaji wake African sports waliamua tena kuwachezesha wachezaji wa ligi ya daraja la kwanza Zanzibar bila ya kuogopa sheria na kanuni za mashindano kuna viongozi ambao wanasema ligi ya Zanizibar ni kama ligi ya Mbuzi kwa hiyo niruhusa kucheza nao wakaamua kumchezesha.
Kwa kuona hilo timu ya Air shooting iliamua kumkatia rufaa mchezaji huyo ambaye anaitwa Pera Ramadhani anayechezea timu ya J.K.U FC ya Zanzibar ambayo ipo ligi daraja la kwanza kwa msimu huu unaoendelea, na mchezaji huyo alicheza mechi tatu katika timu yake hiyo ya JKU tarehe tofauti kama ifuatavyo:-
Tarehe 21/10/2011 JKU V/S Ngome ya Zanzibar
Tarehe 03/12/2011 JKU V/S Bandari ya Zanzibar
Tarehe 28/12/2011 JKU V/S Kijichi ya Zanzibar
Mchezaji huyo katika ligi ya Taifa ngazi ya Wilaya hakuwepo mpaka ligi inaisha, na ligi ya Taifa ngazi ya Mkoa hatua ya makundi pia hakuwepo kwenye timu ya Africa Sports alikuwepo Zanzibar kwenye timu yake na akaomba ruhusa kuja Tanga kwa ajili ya kumuuguza baba yake ndipo African sports wakaamua kumsajili kwa udanganyifu na TDFA kwa vile wameamua kubeba timu kongwe akakubaliwa katika usajili ambao haueleweki katokea timu gani kwani JKU kwa mawasiliano tuliofanya nao wanajua kua mchezaji huyo amepewa ruhusa kuja kumuuguza baba yake wanashaanga kusikia anacheza ligi Tanga na mchezaji wao halali.

No comments:
Post a Comment