Search This Blog

Sunday, March 11, 2012

KITUKO CHA LEO: AFUNGUA MASHTAKA KULIDAI KANISA PAUNDI MILLIONI 10 - KWA KUMZUIA KUICHEZEA MANCHESTER UNITED.

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni.
Mchezaji wa zamani wa ligi daraja la tatu Arquimedes Nganga ameamua kulishtaki kanisa la Baptist akidai fidia ya paundi million 10, kwa madai ya kutumia miaka 19 kama kama mtumishi mwinjilisti wa kanisa hilo hivyo kumpotezea nafasi ya kuweza kuichezea Manchester United.

Bwana Nganga.

“Ningeweza kabisa kucheza kwa muda mrefu kwenye katika premier league,” Nganga mwenye miaka 46 aliliambia gazeti la the Guardian. “Nawaona wachezaji wengi wanaocheza siku hizi ambao naona sio wakali kihivyo na hata wengine nimewazidi sana uwezo. Mimi nilikuwa kiungo mzuri sana – viungo wa siku hizi wengi ni aidha ni waushambuliaji au wakabaji,lakini nilikuwa nipo fiti kotekote kwenye ukabaji na kushambulia pia. Nilikuwa tofauti sana.”

Nganga, ambaye kwa sasa anaishi London,alikuwa akicheza soka katika nchi yake aliyozaliwa lakini aliacha soka alipokuwa na miaka 25, miaka miwilibaada ya kuingia katika dhehebu ya Baptist. Anaamini angeweza kutengeneza paundi 20,000 kwa wiki, japokuwa hakuwahi kutengeneza japo paundi 200 akicheza katika soka la ridhaa.

Na sasa japokuwa hakuwahi hata kuzivutia timu kubwa mpaka anafikisha miaka 25, Nganga ameamua kufungua mashtaka katika mhakama nchini Uingereza akilidai kanisa la Baptist fidia ya paundi million 10.

No comments:

Post a Comment