Mwanaume ambaye anatajwa kuwa manager ajaye wa timu ya taifa anahitaji kuweka jicho lake kwenye mpira na kuongeza umakini katika kuhakikisha Spurs hawaendelei kufanya vibaya katika mechi zilizobaki ili kuweza kugombania nafasi ya kwenda champions league.
Ikiwa Tottenham wakifeli kumaliza katika top four ya premier league msimu huu, lawama hazitokwenda kwa kitu kinachoitwa 'Bahati mbaya'.
Baada ya miezi mitatu katika top 3, Spurs wameshuka chini mpaka nafasi ya nne Jumatano iliyopita walipotoka suluhu na Stoke, wakiendelea na performance yao kubwa baada ya kupata pointi moja kutoka katika michezo yao minne iliyopita.
Timu ambayo hapo mwanzo ilionekana kuwa itakuwa na uhakika wa kumaliza na kupta nafasi ya kushiriki Champions league kwa sasa wana changamoto moto kubwa ya kupigana na mahasimu wao wawili wa London, Arsenal na Chelsea, ili kuweza kuepuka na aibu mwishoni mwa msimu ambao ulitoa matumaini makubwa kwa wapenzi wao.
Jumamosi hii, Spurs wataendelea na mbio ngumu wakienda pale Stamford Bridge, uwanja ambao hawajawahi kushinda tangu 1990. Ikiwa Chelsea watashinda, pengo la pointi kati yao na The Blues litakuwa pointi 2 na Harry Redknapp ataanza kulisikia joto la benchi la ufundi.
Haihitaji mwanasayansi wa hali juu kuweza kutambua hili, suala la ukocha wa timu ya taifa, nafasi anayohusishwa nayo Harry Redknapp, imeanza kuharibu akili na umakini kocha huyu kupelekea Tottenham kuanza kupata madhara juu ya suala hilo.
Tnagu Fabio Capello alipokiuzulu kama kocha wa England, Spurs wamepata wastani wa pointi 0.8 kwa mchezo. Kabla ya hapo Spurs walikuwa na wastani wa pointi 2.1 kwa mechi moja.
The North Londoners wameshinda mchezo mmoja tu tangu Capello ajiuzulu.
Wiki iliyopita siri ilitoka kutoka katika base ya mazoezi ya Tottenham in Chigwell kwamba Redknapp ameamua kwamba atachukua nafasi ya ukocha wa England kiangazi kijacho, juku Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy akipoteza matumaini ya kumshawishi Harry mwenye miaka 65 kubaki White Hart Lane.
Wakati Spurs wakiwa bado hawajafuatwa rasmi na FA, hali ya kutokueleweka ndani ya klabu inaonekana imewachanganya wachezaji, huku Harry Redknapp mwenyewe akionekana kushindwa kuhumili joto la kuwania nafasi ya ukocha England, hivyo kupoteza umakini.
Redknapp ni chaguo la nchi kuiongoza England kwenye EURO 2012 lakini Harry anahatarisha mafanikio ya kazi nzuri aliyoifanya tangu alipojiunga na Spurs October 2008 wakati klabu hiyo ilipokaa chini kabisa ya msimamo wa ligi.
Iwe kazi ya ukocha wa England au sio, Redknapp lazima akubali lawama nyingi kwa kuchangia kushuka vibaya kwa Tottenham.
Pia kukosekana kwa wachezaji wao muhimu kutokana na majeruhi, akiwemo Aaron Lenon na Emmanuel Adebayor pia kumechangia, lakini amefanya maamuzi ya kushangaza sana wiki kadhaa za hivi karibuni.
Timu imekosa balance, shape na mbinu. Gareth Bale amekuwa akiruhusiwa kuzunguka popote dimbani, Luka Modric amekuwa akipangwa pembeni, na Redknapp akiacha safu ya kiungo nyepesi kwa kuwapanga washambuliaji wawili dhidi ya timu ngumu kama Arsenal, Everton na Manchester United.
Wanashindwa kupasiana vizuri, safu ya ulinzi inaonekana kuparanganyika na hasa wanaposhindwa kuzuia set-pieces, kitu ambacho mazoezini whawajifunzi na hata wachezaji wamekuwa wakilalamika kuhusu hilo kwa pembeni pembeni.
Redkanpp na manager mzuri sana wakati timu ikiwa inacheza vizuri, lakini mara nyingi maswali yamekuwa yakizuka kuhusu namna anavyo-handle mambo wakati timu inapoanza kucheza hovyo. Walishinda mechi zao 2 tu kati ya 12 za mwisho mwishoni mwa msimu uliopita, matokeo ambayo mwisho wa siku yaliwakosesha nafasi ya kushiriki champions league.
Wakati Sir Alex Ferguson akifundisha na kupanga mipango ya kikosi chake cha Manchester United ku-peak katika hatua za mwisho wa ligi, inaonekana ni tofauti sana na kwa Redknapp. Manager wa Spurs anasisitiza kuchezesha kikosi chake cha kwanza kila wiki, kwa maana wachezaji kama Modric na Scott Parker wanakuwa wamechoka ligi ikiwa inaingia katika hatua za mwisho za msimu.
Kukosea kwake katika kufanya rotation(mzunguko) pia unachangia sana kuwafanya wachezaji wake muhimu kuumia ama kuchoka msimu unapokuwa kwenye crucial moments.
Namna gani Redknapp anavyojuta, kwa mfano, maamuzi yake ya kumuachia Steven Pienaar kuondoka kwa mkopo kwenda Everton in Jnauary. Kiungo huyo wa Afrika ya Kusini angeweza kutoa msaada mkubwa na kubalance timu lakini alilazimisha kuondoka katika dirisha dogo kwa sababau alikuwa anaudhiwa na ukosefu wa namba ndani ya kikosi cha Spurs.
Matokeo ya mwisho wameanza kupoteza points muhimu na Redknapp ameibuka na visingizio eti Spurs wamepewa mategemeo makubwa kuliko uwezo wao wakati hivi karibuni alikuwa akizungumzia kuchukua ubingwa.
Ama kwa hakika ana asilimia 70 za kuwa kiongozi wa benchi la ufundi la England in Euro 2012 - lakini kwa sasa Redknapp ana kazi ya kumaliza vizuri muda wake wa kukaa White Hart Lane kwa kuisadia Spurs kupata nafasi ndani ya top four.
No comments:
Post a Comment