Search This Blog

Thursday, March 22, 2012

GOGORO KUHUSU LIGI YA TAIFA MKOA WA TANGA LAENDELEA KUFUKUTA MOTO.

Ndugu yangu shaffih pole kwa kazi ya kutupasha habari za michezo kutoka sehemu mbalimbali daniani mungu akubariki maisha marefu.
 Nataka kuzungumza ukweli kuhusu sakata la ligi ya taifa ngazi ya mkoa wa Tanga mana ripoti yako uliyotumiwa na kuisoma siku ya jana ya tarehe 19/03/2012 ilikuwa haina ukweli wowote kuhusiana na suala zima la mgogoro uliojitokeza hapa Tanga.
 Kwanza bila kificho chochote timu ya Small Prison  waliamuwa kuutia aibu mchezo wa soka hapa mkoani kwa kitendo chao cha kuwanunua na kuwahimiza timu ya Segera Fc kususia mchezo dhidi  ya African  Sports  ili wao Small Prison waweze kuingia hatua ya nusu fainal kwa idadi ya magoli.
 Kuthibitisha hayo wachezaji wa timu ya Segera walikuwa wakitamka wazi bila kificho kuwa wakifungwa magoli matatu basi wao wataitoa timu uwanjani, na viongozi wa timu ya Small Prison walikuwa nyuma ya benchi la ufundi la timu ya Segera na kuwahimiza kufanya hivyo.
 Sasa watu wanaosema African Sports wamepanga matokeo wana maanisha nini hivi timu ipange matokeo na timu nyengine wanaweza kweli kiususia mchezo?
 Ushahidi wa pili siku ya mchezo asubuhi yake viongozi wa timu ya Small Prison walipeleka malalamiko yao chama cha soka mkoa wa Tanga kuwa matokeo ya mchezo wa jioni hiyo kati ya African Sports na Segera Fc yalikuwa yamepangwa ili kuipa nafasi klabu hiyo kongwe hapa nchini, hii inaonyesha wazi hawa Small Prison walikuwa wanatumia defenceve mechanism ili kuficha mabaya yao waliyokwisha kuyafanya.
 Lakini kitu cha kushangaza hata jana kwenye waraka wako huyo, anayejiita kiongozi wa timu ya Raidon anataka kujifanya yeye kuwa ni pweza wa kihispania  kwa kuweka wazi kuwa matokeo yatakayotoka  baada ya rufaa iliyokwata yataipa nafasi timu ya African Sports.
 Kitu cha msingi  ni kuwa lazima watu wawe wakweli katika waraka zao wanazozituma kwenu tuache masuala ya chuki na maslahi binafsi, na nyie kama clouds kituo kilicho bora zaidi nchini Tanzania na ukanda huu wa Africa mashariki inabidi mfanye utafiti kabla ya kuweka hewani taarifa kama hizi ambazo zinawachafua viongozi na baadhi ya wadau wa mchezo huu hapa nchini pamoja na timu husika.
 Tukumbuke kuwa kwa mwaka huu tunakwenda katika chaguzi mbali mbali za vyama vya soka hapa nchini na baadhi ya watu wanatumia nafasi hizi za vyombo vya habari kuwachafua wenzao, kwa kusema yasiokuwa ya kweli.

HITIMISHO
Kwa ushahidi wa kimazingira  uliopo na kila mtu anajua hapa mkoani Tanga ni wazi timu ya Small Prison walipanga matokeo kwa kununua michezo yote miwili ule wao dhidi ya Segera Fc na pia waliucheza mchezo wa Segera Fc na African Sports mambo ambayo yalikuwa yakifanyika miaka ya 47 ya mababu na mabibi zetu.

Bila ubishi viongozi wa Small Prison na wale wa Segera wanatakiwa kufungiwa kwa kitendo chao hicho , pia huyo anayejiita kiongozi wa timu ya Raidon anatakiwa kumuomba radhi katibu wa chama cha soka mkoa wa Tanga kwa kumbagua kijinsia kwa kweli chama cha soka mkoa wa Tanga wanafanya kazi kubwa sana kwani wilaya zote nane zimeshiriki ligi hiyo, wameweza kuipandisha timu ya Coastal Unioni, na pia kwa miaka miwili timu ya mkoa wa Tanga imekuwa na matokea mazuri kwenye mashindano ya Taifa cup.
MWISHO-Tuache majungu

1 comment:

  1. Usiwahakumu wenzio inawzekana wewe ndiyo unapotosha,mbona hujaongolea wale wachezaji mamuruki kutoka Zanzibar?

    ReplyDelete