Search This Blog

Monday, February 20, 2012

WENGER BADO ANA SAPOTI YA BODI. APEWA PESA KIBAO ZA USAJILI - GEORGE GRAHAM AMWAMBIE AMUIGEE FERGIE

Struggling: But Wenger has the backing of Arsenal's board

Kwa mara nyingine tena pamoja na mambo kuendelea kuwamabaya @Emirates bodi ya wakuregenzi ya klabu ya Arsenal imeonyesha kuwa bado na imani kubwa juu ya kocha Arrsene Wenger ambaye amehakikishiwa kupewa kiasi cha paundi million 55 kwa ajili ya kuimarisha kikosi katika kipindi kijacho cha kiangazi.

Majority shareholder wa klabu ya Arsenal Stan Kroenke yupo nyuma ya Wenger kwa asilimia 100 pamoja na kocha huyo kuwa karibu na kutimiza mwaka wa 7 bila kikombe.

Msimu wa klabu hiyo ya London kaskazini uliendelea kumwa mbaya zaidi baada ya kutolewa katika FA Cup na Sunderland wikiendi iliyopita, baada ya pia kutoka kufungwa kipigo cha aibu cha cha 4-0 dhidi ya AC Milan katika mechi ya kwanza ya mtoano ya Champions league.

Matokeo mabaya ya msimu huu yamekuwa yakizusha maswali wengi wakijiuliza juu ya hatma ya kocha huyo ndani ya klabu hiyo ya London. Ingawa sasa bodi ya Arsenal wameendelea kuwa na imani Wenger wakiweka wazi ndio mtu sahihi wa kurudisha enzi za ushindi ndani ya klabu.

Lakini pamoja na kuendelea kupata sapoti kutoka kwa bodi ya wakurugenzi pamoja kupewa fedha nyingi za usajili, Wenger anajua bado ana upinzani mzito katika kuendelea kukaa kwa amani katika benchi la klabu hiyo.
Hivi karibuni legend wa Gunners George Graham - ambaye alishinda makombe 9 na klabu hiyo kipindi akiwa kama mchezaji na kocha, nae ameanzisha mashambulizi dhidi ya Wenger na Arsenal kwa ujumla.

Alisema: 'Nafikiri Arsenal wapo katika crisi. Nadhani ni kutokana na kuteleza amakuangguka kutoka walipokuwa miaka 8 iliyopita na tatizo lao kubwa wamekuwa hawajazi nafasi za wachezaji wanaondoka kwa wabadala sahihi. Wana fedha ya kununulia wachezaji hivyo sielewi kwanini Wenger hanunui wachezaji wenye ubora wa hali juu wakati wa usajili.
"Siku hizi inabidi uwe unawaingiza vijana wadogo kwenye timu kama afanyavyo Sir Alex Ferguson, lakini at the same time atanunua mchezaji aliye tayari tena mwenye ubora kwa ada ya paundi million 25 ili kukipa ubora zaidi kikosi chake. Nafikiri sera ya Wenger ya wachezaji vijana anaitumia vibaya na wachezaji anaowaingiza kwenye timu ya wakubwa sio wazuri kama ambao wanakuwa wameondoka."

No comments:

Post a Comment