Search This Blog

Wednesday, February 22, 2012

EXCLUSIVE: WAYNE ROONEY NJE DHIDI YA AJAX


Sir Alex Ferguson amethibitisha Wayne Rooney atakosa mchezo wa marudiano ya Europa league dhidi ya Ajax baada ya kupata maambukizi ya koo.

Rooney alifika mazoezini lakini aliambiwa arudi home katika matumaini kwamba atapona na aweze kucheza katika mechi ya Jumapili dhidi ya Norwich.



“Wayne atakuwa nje kesho,” alisema Fergie. “Ana matatizo kwenye koo. Alionekana kuwa na dalili hizo tangu tulivyokuwa Amsterdam na tulimpa dawa lakini ugonjwa ukazidi.
“Amekuwa kitandani weekend nzima na leo alikuja mazoezini kwa mara ya kwanza lakini atakuwa nje kujiweka sawa kwa mchezo wa Jumapili.

United ambao wapo mbele kwa goli 2-0 dhidi ya Ajax, ikiwa watapita watakutana na aidha Lokomotiv  Moscow au Athletic Bilbao.                                                                                                                                                                                                                               

No comments:

Post a Comment