Search This Blog

Wednesday, February 22, 2012

ISRAEL BADO ANARANDARANDA STAMFORD BRIDGE - CHELSEA AKIPIGWA 3-1 NA NAPOLI

Wabishi wa darajani waliomchana Andre Villas Boas wakiwa wamepigwa benchi katika mechi dhdi ya Napoli.
Wachezaji wa Chelsea walipingana waziwazi na boss wao Andre Villas-Boas – kabla ya kipigo cha Napoli jana usiku.

Ashley Cole, Frank Lampard na Micheal Essien waliongoza revolt hiyo dhidi ya AVB, ambaye yeye mwenyewe ndiye aliyesababisha hali hiyo.

Villas-Boas aliweka kikako cha kuzungumzia na kutoa maoni juu ya matokeo mabaya wanayoyapata katika siku za hivi karibuni jumapili iliyopita.

Lampard na Essien ndio walioanza kutoa maoni yao – lakini alikuwa Cole ambaye aliongea na kuonyesha wazi kukerwa na mreno huyo.

Beki huyo wa kushoto wa England alimwambia AVB, “Nimekuja hapa kushinda medali na makombe, lakini sitokuja kushinda vitu hivyo na hivi mbinu zako.”
Cole pia ana furaha na anajihisi kama robot kwa AVB anavyomwambia ni jinsi gani anataka acheze kwa kufuata masharti yake tu, na haampi uhuru wa kucheza mwenyewe.

Wachezaji wengine wa Chelsea pia waliudhiwa kuona wenzao watatu muhimu wakipigwa benchi  baada ya kumbwatukia kocha kuelekea katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa UEFA Champions league.

Inasemekana AVB alimwambia Cole “umeifanya issue iwe binafsi.”
Cole alikasirishwa zaidi alipomuona manager wake akisema kwenye interview kwamba Ashley ameachwa kwakuwa hayupo fit vizuri.
Cole alifanya mazoezi zaidi na kusisitiza kwamba alikuwa yupo fit kucheza lakini AVB hakumsikiliza, na Ashley  akafanya kejeli kwamba AVB alimuita baada ya Jose Bosingwa kuumia.

No comments:

Post a Comment