Hatimaye Carlos Tevez amejishusha na kuomba msamaha kwa mashabiki na timu yake ya Manchester City.
Tevez ametoa taarifa ya kuomba msamaha leo baada ya karibia miezi 5 kugoma kuitumikia City kitendo kilichomgaharimu kiasi cha paundi million 10 kupitia mishahara, bonsai na faini.
Taarifa iliyoandikwa na Tevez iliwekwa kwenye mtandao rasmi wa City ilisomekana hivi: “Napenda kuomba samahani kwa kila mtu ambaye matendo yangu ya hapo nyuma yalimuumiza. Umakini wangu sasa upo katikakuichezea Manchester City Football Club”
Pia klabu hiyo ilitoa taarifa kwamba Carlitos ameondoa rufaa yake aliyopinga adhabu ya City ambayo ilikuwa imepangwa kusikilizwa na jopo la watu wa premier league katika siku zijazo.
Taarifa hizi zinasemakana kumfurahisha sana Mancini na Tevez sasa anaweza akaanza kurudi kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza na kuweza kutimikia klabu hiyo.
ujanja mwingi mbele kiza...kibuli hakisaidii, kiko wapi sasa si amefanya kilekile alichokuwa ziku zote anashauriwa kufanya!
ReplyDeleteby JJ