Alikuwa mgeni katika michuano ya Tennis, ATP World Tour final kati ya Roger Federer na Jo-Winlfried Tsonga at the 02 Arena. Lilikuwa tukio kubwa na soka ilikuwa imewakilishwa vizuri.
Gareth Bale, Robert Pires, Chris Smalling, Luis Nani na Andrey Arsharvin wote walikuwepo. Federer alishinda, lakini kipindi Ronaldo anaondoka palitokea gumzo kubwa katika eneo hilo la mchezo tofauti anaoucheza yeye.
Mapema siku asubuhi, ilisemekana, Ronaldo alionekana katika eneo la Les Ambassadeurs, private club na casino karibu na Hyde Park. Alikuwa na wakala wake, Jorge Mendes na cha kushangaza zaidi alikuwepo David Gill, CEO wa Manchester United. Haikuwahi kuthibitishwa na yoyote kati ya hawa watatu juu mkutano huu, lakini bado kumekuwepo na maneno maneno kuhusu mkutano huu.
Inawezekana Ronaldo, Mendes na Gill walikutana tu kwa bahati. Eneo la Les Ambassadeurs ni sehemu maarufu kwa watu wa soka kuhudhuria. Wanaume hawa wote watatu wanafahamika mahala pale. Kama Gill alimkuta Mendes na Ronaldo wakiwa wanakunywa kahawa, kwanini ashindwe kuungana nao? Watu wa magazeti wanaweza kuandika na kutoa habari yoyote kuhusu mkutano huo na isiwe ukweli.
Kumbuka mwaka 2005, yaliripotiwa mazungumzo yaliyofanyika mahala pale kati ya Rio Ferdinand na Peter Kenyon(CEO wa zamani wa Chelsea at that time). Vyombo vya habari vikaripoti kuwa Ferdinand alikuwa njiani kuelekea Chelsea kutokana na kukutana na Kenyon ambaye alijulikana kwa kucheza michezo ya kimafia katika kusajili wachezaji. Lakini sasa ni miaka 7, Je Rio ameshawahi hata kukaribia kuwa mchezaji wa Chelsea.
Indeed, kama Gill alikuwa anafanya mkutano wa siri na Ronaldo, kwa hakika asingeichagua sehemu ile ambayo siku zote inakuwa inajazwa na wadau wa soka wakiwemo waandishi wa habari.
Sasa taarifa za kusema kuwa Ronaldo alikuwa na mkutano wa siri na CEO wa United, inawezekana walikutana na tu kwa bahati mbaya. Lakini swali moja tu linabakia. Fikiria kama kweli kuna jambo la siri katika mkutano wa Gill na Ronaldo pamoja na Mendes?
Suppose kwamba Manchester United wana mpango wa siri kumrudisha CR7 at OT? Je suala hilo halitakuwa jambo zuri kwa United ambao sasa wanapambana na kivuli cha City katika kutawala soka la England?
Speculation kwamba Ronaldo anafaa kurudishwa Theatre of dreams itazidi kama Mreno huyo atacheza vibaya leo usiku dhidi ya Barcelona katika robo fainali ya Copa DE Relay. Tabia yake ya kutokucheza vizuri katika El classico imeanza kuwachosha baadhi ya watu @Bernebeu.
Mfano mzuri mchezo wa kwanza baada ya mapumziko ya winter, nyumbani dhidi ya Grenada alizomewa sana na mashabiki wa Madrid kipindi chote cha mchezo, Ronaldo hata alipofunga goli la 5 la Madrid hakushangilia, na baadae hata Raisi wa heshima wa klabu hiyo Alfredo di Stefano aliungana na mashabiki kumsema Ronaldo.
Leo Jumatano, kama Lionel Messi ataibuka mshindi na kucheza vizuri kiasi cha kumfunika Ronaldo, wabaya wa Mreno huyo wataongezeka zaidi. Mchezo wa pili wa marudiano siku saba baadae, by which time habari za kurudi Manchester United zinaweza kuongezeka zaidi.
Naamini, hata kama kumuachia Ronaldo kuondoka itakuwa sio sasa, Wakiwa mbele kwa pointi 5 dhidi ya Barcelona in La Liga, na wakiwa katika champions league. Sioni nafasi ya Madrid kumuacha Ronaldo in the short term. Labda mwishoni mwa msimu. Nani anajua?
Ikiwa zengwe dhidi ya Ronaldo litaendelea huku mashabiki wakiendelea kumzomea, hii crisis inaweza kuzidi. Inevitably, Ronaldo anaweza kuwa disappointed ukizingatia kucheza Madrid ilikuwa ndoto yake tangu akiwa mtoto, hivyo kuendelea kufanyiwa anavyofanyiwa na mashabiki na baadhi ya wakubwa Madrid kutamuumiza sana – hali ambayo sio Jose Mourinho au mrithi wake anaweza kui-handle katika kumfanya Ronaldo acheze kwa moyo wote in katika circumstances za namna hii.
Kocha anaweza hata kuanza kukubaliana na maoni juu ya inferiority complex ya Ronaldo, dhidi ya Ronaldo na Messi, anaweza kuanza kuhisi kwamba star asiyeweza kupambana vizuri na adui mkubwa wa Madrid sio mtu muhimu kabisa katika kikosi chake, na kama Barcelona watakuja kuwakamata Madrid katika ligi ya msimu huu na kuchukua ubingwa, Ronaldo atakuwa na hali mbaya zaidi, hali ambayo itaongeza na kuupa nguvu uvumi wa winga huyo kurudi United.
Of course, itakuwa ni kosa kubwa kwa Madrid kumpoteza Ronaldo, lakini klau hiyo imeshafanya makosa ya namna hii huko nyuma. Katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Perez alikubali kumuuza Claude Makelele ambaye alikuwa ndio nguzo ya safu ya ulinzi ya Madrid, na hapo ndipo alipojua umuhimu wa mfaransa yule. Sawa sawa na baadhi ya mashabiki wasio na shukrani wale Man United walipojua umuhimu wa Ronaldo mara tu baada ya kuondoka.
Watu wenye nguvu ya kulazimisha maamuzi ndani ya Madrid wata underestimated mchango mkubwa alioutoa Ronaldo ndani ya klabu hiyo (akiwa tayari na magoli 26 msimu huu, akifunga mabao 53 last year, na magoli 33 katika msimu wake wa kwanza).
Ronaldo ni La liga top scorer akiwa anaongoza kwa kupiga michomo mingi langoni mwa adui huku akiwa katika top 5 kwa kutoa assists. United wanaomba na kutumaini Madrid wawe vipofu kwa mchango mkubwa namna hii. Ni chizi pekee ambaye bado anaamini Ronaldo hakumbukwi at Old Trafford.
Udhaifu wa safu ya kiungo ya United umekuwepo kwa muda mrefu kiasi cha sasa kufikia hatua ya Paul Scholes kuamua kurudi uwanjani, hivyo United stalwarts sasa inabidi washukuru uwezo binafsi wa Ronaldo liziba mapengo yaliyoonekana baada ya kuondoka. Wayne Rooney hakuwahi kuonekana kutokuwa na furaha kipindi Ronaldo alipokuwa uwanjani kwa sababu aliifanya United iogopwe hata kushambulia na wapinzani. Bila Ronaldo, United imekuwa ikimtegemea zaidi Rooney, na hilo limeonekana. So itakuwaje ikiwa Ronaldo akiwa radhi kurejea? Je atawafaa United?
Vipi kuhusu kutoa ofa sahihi, haitakuwa dhulma kuwapa Madrid fedha yao £80million waliyotoa kumsaini CR7?
Ashley Young na Antonio Valencia ni wachezaji wazuri, lakini hakuna kati yao anaweza kufikiriwa kuwa mchezaji sahihi wa kuziba pengo la Ronaldo. Tumtoe Messi, nani anaweza kubisha? Haya kwa mfano tufikirie kwamba Gill, Mendes na Ronaldo walikutana kweli in Les Ambassadeurs siku ile, na haikuwa bahati mbaya na ni kweli waliongea kuhusu United kumnunua tena Ronaldo, na mara tu baada ya kikombe cha mwisho kahawa wote watatu walikubaliana itabidi wafanye tena mkutano tena, perhaps sehemu ya siri zaidi ili kukamilisha ujio wa CR7 mjni Manchester. Kwa sababu Ronaldo amemisiwa na United, soka la England pia.
Kama watu 80,000 katika uwanja wa Bernabeu hawautaki ama hawajui utamu wa mchezaji huyu, watu wa England wanaujua na Ronaldo anapaswa kujua hilo. Ronaldo ana thamani ya kila shilingi ya pesa waliyolipa Madrid. Ana thamani ya hata ya zaidi ya £80million plus hata kadi 1000 ya CEO ya uanachama wa Les Ambassadeurs (kadi moja ya klabu hiyo ina thamani ya £1000). Indeed, hiyoinaweza kuwa cheki bora iliyowahi kusainiwa na Glazers.
Mwisho kabisa Ronaldo anastahili kila shilingi ya pesa waliyolipa Madrid kwa Manchester United.
HIYO PICHA YA AKINA MAKELELE INANIKUMBUSHA MBALI SAAANA.
ReplyDeleteNYUMA WAPO LE CAPTANO HIERO,KARANKA,KALOSI,SALGADO PALE KATI MAKELELE,ZIDANE,FIGO,CAMBIASO,SOLARI NA PALE MBELE RAUL,RONALDO,SAVIO!MZEE DEL BOX ANAKUNA NDEV PALE BENCH
NATAMANI KM MUDA UNGEWEZA KURUDI NYUMA.