Search This Blog
Friday, December 23, 2011
YAYA TOURE NDIYE MWANASOKA BORA WA AFRIKA 2011
KIUNGO wa Ivory Coast Yaya Toure (28) ametawazwa kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa mwaka 2011 kupitia tuzo zilizotolewa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) na kufanyika katika ukumbi wa Banquet uliopo ndani ya Ikulu ya Ghana.
Toure anayekipiga katika klabu ya Manchester City ya Uingereza alitwaa tuzo hiyo baada ya kupata kura nyingi na kuwapiku nyota wenzake aliotinga nao fainali, Mghana Andre Ayew na Seydou Keita wa Mali .
Mbali na tuzo hiyo pia kulitolewa tuzo mbalimbali kama ifuatavyo:
Mchezaji bora wa mwaka (anayekipiga Afrika):
-Oussama Darragi (Tunisia).
Mchezaji bora (Wanawake)
- Perpetua Nkwocha (Nigeria)
Mchezaji anayechipukia:
- Souleymane Coulibaly (Ivory Coast)
Mwamuzi bora:
-Noumandiez Doue (Ivory Coast)
Kocha Bora:
-Harouna Doula (Niger)
Timu bora ya Taifa (Wanawake):
-Cameroon
Klabu bora:
- Esperance ya Tunisia)
Nidhamu ya Mchezo:
-Libya
Tuzo ya Heshima:
-Mustapha Hadji( Morocco) na Austin ‘Jay-Jay’Okocha ( Nigeria)
source:
http://mamapipiro.blogspot.com/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
kwa kuangalia tu hizo tuzo that means soka afrika ipo afrika magharibi na kati hapo kwa warabu sie huku kwingine makida makida na sarakasi nyingi hakuna kitu,mpaka libya?
ReplyDeletechela wa dom
Yahya Toure amestahili kabisa Tuzo hiyo, jamaa yuko nondo kwa kweli, ukijaribu kuangalia performance ya mancity kwa kweli jamaa anmchango mkubwa sana.
ReplyDelete