Search This Blog

Friday, December 2, 2011

RAMADHAN WASSO, MUKENYA NA WANAIGERIA KUONGEZA NGUVU COASTAL UNION


Timu ya Coastal Union imetangaza majina ya wachezaji waliowasajili wakati wa dirisha dogo
kwa ajili ya kuwatumia katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akitangaza majina hayo, Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Hemed Aurora alisema wachezaji waliosajiliwa wametoka klabu mbalimbali hapa nchini wengine wakiwa ni wachezaji huru.

Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Felix Ameche na Samuel Temi wote raia wa Nigeria. Ramadhani Wasso( huru), Ahmed Shiboli kutoka Simba aliyechukuliwa kwa mkopo, Edwin Mukenya (huru), Lameck Dayton (Villa Squad ), David Changula (Azam FC), Laurent Mugia, Mugenzi Philipo na Bakari Mohamed ambao wote ni huru.

Alisema kuwa katika usajili huo wamewatoa baada ya wachezaji kwenye timu za ligi daraja la kwanza hapa nchini na kuwataja kuwa ni kipa Omari Hamis aliyepelekwa kwa mkopo timu ya Kwarara FC ya Zanzibar inayoshiriki ligi daraja la pili.

Wengine ni Konji Yohana na Abdallah Ulasi na Ramadhan Nyumbi waliopelekwa kwa mkopo AFC Arusha na Omari Maligwa (Morani SC).

Aliwataja walioachwa kuwa ni Yahaya Akilimali kutokana na kushindwa kuripoti tangu
alivyosajiliwa, Juma Salum, Sabri Makame, Abdallah Abasi,Hassani Banda na Farouq Ramadhani ambao walienda Oman kushiriki Kombe la Mafuta.

No comments:

Post a Comment