Search This Blog

Saturday, November 12, 2011

SAMATTA AGOMA KULA CHAD


Katika hali ya kushangaza, mshambuliaji tegemeo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na TP Mazembe ya Congo, Mbwana Samatta hajakula chakula chochote cha asubuhi tangu timu hiyo ilipowasili Jumatano usiku.

Samatta hakuonekana katika ukumbi wa chakula wa Hoteli ya Santana ambayo Stars wamefikia jijini N’djamena na wakati wote wa asubuhi huku akilalamika kuwa mazoea ya maisha ya DR Congo yanamuathiri kwa kiasi kikubwa.

“Siwezi kula ndugu yangu. Kule DRC kumenizoesha vibaya. Huwa tunafanya mazoezi kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa sita.

"Tukirudi tunasubiri kidogo tunakwenda kula chakula cha mchana. Huwa hatuli chakula cha asubuhi, muulize Thomas (Ulimwengu),” alisema Samatta.

Alipouliuzwa kuhusu suala hilo , Ulimwengu ambaye pia anaichezea TP Mazembe alikiri kwamba na yeye ameanza kuathirika na hali hiyo ingawa tofauti na Samatta yeye alikuwa anapiga msosi kama kawaida.

“Hata mimi nimeanza tabia hiyo. Sijisikii kula asubuhi kwa sababu ratiba ya Congo ni tofauti kabisa na ya Tanzania au huku” aliongeza Ulimwengu ambaye anakaa chumba kimoja na Samatta.

Katika pambano la jana, kocha wa Stars Jan Poulsen alitarajiwa kumuanzisha Samatta na kumuweka benchi Ulimwengu katika mfumo wa 4-5-1 ambao unamuweka mshambuliaji mmoja tu katika eneo la mbele.

EDO KUMWEMBE, N’DJAMENA

No comments:

Post a Comment