Search This Blog

Tuesday, November 1, 2011

RAGE: BASENA AJIELEZE KWA KIPIGO


Baada ya kupokea kipigo cha kwanza katika ligi kuu ya TZ bara kutoka kwa watani wao wa jadi Yanga, mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage amemtaka Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mosses Basena ampatie ripoti kuhusu mechi ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Yanga na pia ushiriki wa timu hiyo kwenye duru la kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ilieleza kuwa Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini, ameiagiza Kamati ya Ufundi ya timu hiyo na Kamati ya Mashindano kukutana haraka na kuandaa taarifa kuhusu mwenendo mzima wa timu katika ligi na mechi ya Yanga.

“Pia Mwenyekiti amemuagiza Kocha Mkuu wa Simba, Mosses Basena, kuandaa ripoti kamili kuhusu timu na kuiwasilisha kwake kabla ya Ijumaa wiki hii.

Mwenyekiti wa Simba ataziwasilisha ripoti hizo za kamati na ya mwalimu, kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji kilichopangwa kufanyika Ijumaa wiki hii jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliwa.

“Kamati ya Utendaji ya klabu itafanya maamuzi yake kutokana na ripoti hizo za kamati. Kwa taarifa hii, Simba inawaomba wanachama wake kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu kwao.

Ule mmoja na ushikamano uliokuwapo wakati wa kuelekea pambano la watani wa jadi unatakiwa kuendelea kuwapo ili kuzuia maadui wasituvuruge,” ilisema Kamwaga kwenye taarifa hiyo.


2 comments:

  1. Kimsingi team coach hana tatizo,team ina cheza vizuri na hata viwango vya wachezaji ni vizuri.Ni kweli Yanga wametufunga lakini kama alivyosema jana mwenyekiti tuache kufikiria kigezo cha kufungwa na Yanga kuwa team haifanyi vizuri.Nadhani sisi Simba tulipaswa tuanze na naamini baadae wenzetu watatufuata.

    ReplyDelete
  2. We have a good team,with a best coach..and still i don think if it will be right for the admistrators of simba to send away the coach..let us gv him some more time..{MTAZAMO}

    ReplyDelete