Search This Blog

Thursday, December 1, 2011

MKWASA AKERWA NA MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA


Manager wa timu ya soka ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) Charles Boniface Mkwasa
ameshutumu tabia za mashabiki wa soka nchini kuingiza siasa za Simba na Yanga katika kushangilia timu ya taifa.

Mkwasa alisema hayo wakati akijibu swali kama kitendo cha kumuingiza kiungo wa Yanga Nurdin Bakari katika mechi ya Kombe la Chalenji juzi dhidi ya Djibouti kilitokana na kutaka kuungwa mkono na mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wakiizomea timu hiyo karibu muda wote wa mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa ambapo Stars iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Katika mchezo wa juzi kabla ya Bakari na Godfrey Taita kuingia kipindi cha pili kikosi cha timu hiyo hakikuwa na mchezaji yoyote kutoka Yanga hali iliyofanya mashabiki wa Yanga kuizomea mara kwa mara timu hiyo.

Akizungumzia hali hiyo kocha Mkwasa alisema sio vizuri kwa mashabiki kuingiza siasa za
U Simba na U Yanga katika kushangilia timu hiyo kwani hiyo siyo Simba wala Yanga bali
ni timu ya Taifa.

Mkwasa alisema kuna kipindi timu ya Taifa iliundwa na wachezaji zaidi ya 15 kutoka Yanga na wala hakuwahi kuona mashabiki wa Simba wakiizomea timu hiyo kwa kuwa haikuwa na wachezaji wao wengi.

“Ni jambo la kawaida kuna kipindi Yanga ilikuwa na wachezaji zaidi ya 15 katika kikosi cha timu ya Taifa lakini sijawahi kuona mashabiki wa Simba wakiizomea timu hiyo,”alisema
Mkwasa kwa masikitiko.

Aliwataka mashabiki wa soka nchini kuiunga mkono timu hiyo na kwamba kama ikifanya
vibaya basi wajue aibu ni ya nchi nzima.

Maneno ya Mkwasa yaliungwa mkono na nahodha wa timu hiyo Juma Kaseja aliyesema
anasikitishwa na hali hiyo na kuongeza wao watakuwa pamoja na wale wote wanaowaunga mkono mpaka mwisho wa mashindano.

“Sio kitu kizuri lakini kama wanatuzomea waache watuzomee lakini sisi tupo pamoja na wale wote wanao tuunga mkono,”alisema Kaseja.

3 comments:

  1. WASHABIKI WANAOSHANGILIA TIMU PINZANI WAKO SAHIHI,HIYO TIMU YA MKWASA NA JULIO HAIKO ORGANIZED KWA KIFUPI TIMU AU MAKOCHA HAKUNA. NA WATANZANIA TUTABAKIA KUWA VICHWA PANZI MPAKA DUNIA IPAUKE. TUMEKUWA WAJINGA WA KUJISIFU PALE TUNAPO WAFUNGA VIDONDE LAKINI UKIKUTANA NA WANAOPIGA MPIRA PRESHA TUPU. MAGAZETI NAYO YANAZINGATIA UNDUGU NA BIASHARA HAWAELEZI UKWELI HALISI WA MAMBO. WAMENG'ANG'ANIA WAZAWA WAPEWE TIMU LEO GOMA HILO, MAJUNGU TU!

    ReplyDelete
  2. MKWASA NA JULIO TIMU INAMATEGE HIYO, KWA ZIMBABWE MTALALA MAPEMA TU!

    ReplyDelete
  3. siwaungi mkono wanaozomea timu ya taifa hata kidogo. Kama ulikuwepo katika mechi ya ufunguzi pale Rwanda walipofunga goli, kikundi fulani kwenye jukwaa la yanga, washangilia mpaka tukashangaa wote. Lakini kwa upande mwingine inawajenga wachezaji hata wakicheza mechi za ugenini haiwapishinda kuzomewa na wenyeji wao wakati wao wamezoea kuzomewana watanzania wenzao.

    ReplyDelete