Search This Blog

Monday, November 21, 2011

JULIO: BOBAN BADILI TABIA - ULITUMIKIE TAIFA LAKO VIZURI


Assistant coach wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Jamhuri Kihwelu 'Julio' amemtaka kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' kubadilika ili kuepukana na tuhuma mbalimbali zinazokua zikimkabili.

Mchezaji huyo amekuwa akikumbwa na kashfa mbalimbali, nje na ndani ya uwanja jambo ambalo linamfanya aonekana mtukutu machoni mwa wapenzi na mashabiki wa soka nchini huku wengine wakimuona kuwa ni mtovu wa nidhamu.

Julio alisema kuwa uwezo na kiwango cha Bobani ni cha juu na anastahili kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu za taifa hata nchini lakini tabia yake ndiyo hasa inayomfanya ashindwe kupata nafasi hiyo.

"Hakuna mwenye wasiwasi na uwezo wa Boban, kila mmoja anayefuatilia soka anaijua soka yake, lakini tabia yake ndiyo tatizo hivyo anapaswa kubadilika na kuangalia mafanikio zaidi katika maisha yake ya soka.

"Kwa uwezo alionao hapaswi kuendelea kuwa hapa nchini hivyo namuomba ayatumie mashindano ya Chalenji kujitangaza na vilevile kuisaidia Tanzania Bara kutetea ubingwa wake," alisema Kihwelu ambaye kwa kauli hiyo, ni wazi wameshampitisha kuitumikia timu hiyo katika michuano ya Chalenji.

Katika hatua nyingine; Julio alisema kuwa ana matumaini makubwa na Boban pamoja na wachezaji wengine kuhakikisha Tanzania Bara inatetea ubingwa wake kwenye mashindano ya Chalenji yanayoanza kutimua vumbi Jumamosi ijayo Novemba 25.

Katika mashindano hayo Tanzania itaanza kutetea ubingwa wake kwa kupambana na Rwanda, Ethiopia na Djibouti katika hatua nya makundi.

No comments:

Post a Comment