Chelsea 1 – 2 Liverpool 20-11-11 FULL HIGHLIGHTS... by garethbetty007
1 – Manchester City sasa ndio timu pekee ambayo haijafungwa katika Barclays premier league baada ya kuwa timu ya kwanza kuipa kipigo Newcastle United msimu huu.
2 – Ushindi wa Manchester United wa 1-0 dhidi ya Swansea City ulikuwa wa kwanza katika uwanja wa nyumbani wa timu inayotoka Wales katika mechi 9.
3 – Mshambuliaji wa Norwich City Steve Morison sasa amefunga katika mechi 3 za mwisho za EPL.
4 –Stoke City wamefungwa mechi zote nne za mwisho katika EPL, baada ya kufungwa na QPR 3-2 nyumbani kwao.
5 – Sunderland sasa wameshindwa kufunga katika mechi zao 5 za mwisho na Fulham kufuatia sare ya tasa katika uwanja wa Stadium of Light juzi Jumamosi.
6 – Straika wa Bolton Wanderers Ivan Klasnic sasa amefunga magoli sita katika mechi sita za mwisho za premier league alizoanza baada ya kufunga katika mechi waliyofungwa na 2-1 na West Bromwich Albion.
8 – Goli la penati la Mario Balotelli dhidi ya Newcastle United linamaanisha kuwa sasa amefunga magoli 8 katika mechi tisa zilizopita.
9 – Kufungwa 2-1 na Liverpool sasa kunamaanisha Chelsea wamefungwa mfululizo kwa mara ya kwanza katika miaka 6 na nusu tangu mwezi wanne na watano mwaka 2002 walipofungwa na Manchester United na Aston Villa @ Stamford Bridge.
31 – Magoli mawili ya Robin Van Persie at Norwich City yaliongeza idadi ya magoli kuwa 31 katika mwaka 2011, yakimfanya kuwa mchezaji wa tano wa pekee wa Premier league kufunga magoli 30 katika kalenda ya mwaka.
No comments:
Post a Comment