Search This Blog

Friday, November 4, 2011

JOHN BOCCO AMTEMESHA NAMBA MRWANDA TAIFA STARS


Wakati kikosi cha Taifa Stars, kikiingia kambini jana kujiandaa na mechi ya mchujo dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 jijini N’Djamena, kocha wa timu hiyo, Jan Poulsen, amemtema mshambuliaji Dan Mrwanda na kumuita John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC kuziba nafasi yake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Poulsen alisema amemua kumuacha mchezaji huyo anayekipiga katika klabu ya DT Long An, Vietnam kutokana na kutokuwa na uhakika kama atajiunga na wenzake kwa wakati kwani muda wa kujiandaa kabla ya mechi hiyo ni mdogo.

Stars inatarajiwa kuondoka nchini kwenda Chad Novemba 9 kwa ajili ya mchezo huo kabla ya kurudiana Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam kuwania kuingia kwenye makundi ya kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.

Kikosi hicho kinaundwa na Makipa, Juma Kaseja (Simba), Mwandini Ally (Azam Fc). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam Fc), Juma Jabu na Juma Nyoso (Simba), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya), Erasto Nyoni (Azam Fc), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Godfrey Taita (Yanga).

Viungo ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Ramadhan Chombo (Azam Fc) na Shomari Kapombe (Simba).

Washambuliaji ni, Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam Fc), Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).

No comments:

Post a Comment