Mlinzi wa Chelsea Jose Bosingwa ameweka wazi kuwa hatoichezea tena timu yake ya taifa ya Ureno mpaka kocha wa sasa wa timu hiyo Paulo Bento atakapoondoka kwenye nafasi hiyo.
Bosingwa aliachwa katika kikiosi kitakachocheza play off ya Euro dhidi ya Bosnia and Herzegovina, huku Bento akiwa na mashaka huu ya mentality na tabia ya Bosingwa.
Akizungumza leo Bosingwa alisema: “Sijui nini anaongea kuhusu maoni yake juu mentality na altitude yangu. Nahisi kudhalilishwa na kutoheshimiwa kutokana na maneno yake. Sitovaa tena jezi ya Portugal ikiwa huyu Bento ataendelea kuwa kwenye benchi,” Bosingwa alikaririwa na A Bola.
“Jamii nzima inatambua juu ya tabia ya kocha huyu, haelewani na wachezaji na anagombana nao kila mara. Ana uwezo wa kiakili wala kihisia kuongoza kundi la wanaume na hafai kabisa kuiongoza timu ya taifa.”
Bosingwa anakuwa mchezaji wa pili wa Ureno kuamua kustaafu kuichezea Ureno, baada ya beki wa Real Madrid Ricardo Carvalho kujiondoa katika timu hiyo baada ya kugombana na kocha Bento.
No comments:
Post a Comment