Licha Yanga kumkabidhi mikoba ya kuifundisha klabu hiyo, Mserbia Kostadin Papic, uongozi bado unafanya naye mazungumzo ili kukubaliana naye vitu vya msingi kabla ya kuingia naye mkataba.
Hatua hiyo inatokana na kocha huyo kuwa na matatizo madogo madogo ambayo yalisababisha uongozi awali kushindwa kumuongeza mkataba, kabla ya kocha huyo kutimka.
Mmoja wa viongozi wa Yanga, aliiambia blog hii kwamba kinachofanyika sasa ni kuzungumza na Papic masuala mbalimbali, ambayo yatasaidia kuweka mambo katika mstari ulionyooka.
“Papic ni kocha mzuri na ndiyo maana tumeridhia arudi, lakini ana mambo fulani fulani yasiyopendeza, hivyo tumeona kuna haja ya kukaa na kuwekana sawa kabla ya kuingia naye mkataba,” alisema.
Papic ambaye alikuwa akiifundisha Yanga msimu uliopita kabla ya kutimkia kwao kabla ya kumaliza mkataba wake, amepewa tena jukumu la kuinoa timu hiyo akirithi mikoba ya Sam Timbe.
No comments:
Post a Comment