Baada ya kushindwa kuanza katika muda muafaka sasa ligi kuu ya Soka ya Zanzibar imepangwa kuanza Novemba 1 baada ya kampuni ya usafiri wa meli ya Seagull kutangaza kuidhamini kwa Sh 25 milioni.
Awali ligi hiyo ambayo itashirikisha klabu 12 za Unguja na Pemba ilikuwa ikiahirishwa mara kwa mara baada ya kukosekana kwa mdhamini wa kuiendesha.
Akizungumza kwa simu kutoka Zanzibar jana,Msemaji wa Chama cha Soka Zanzibar, ZFA, Munir Zacharia alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kitagharimia usafiri kwa klabu 12 zitakazoshiriki ligi hiyo.
"Ligi yetu sasa itafanyika Novemba 1 baada ya kampuni ya Seagull kujitokeza kuidhamini kwa kutoa kiasi cha Sh.25 milioni.
"Tunashukuru kwa udhamini huu ingawa bado tunayaomba makampuni mengine yajitokeze kwani bado tunahitaji kuungwa mkono kwavile uendeshaji wa ligi ni gharama kubwa,"alisema Munir.
Aliongeza kuwa mdhamini wa ligi hiyo pia atatoa kiasi cha Sh 10 milioni kwa timu itayoibuka bingwa wakati mshindi wa pili atapata Sh 5 milioni huku mwandishi bora wa televisheni,magazeti na redio atakayeripoti vizuri kila atazawadiwa Sh 500,000.
Zakaria alizitaja klabu zitakazoshitiki katika ligi hiyo kuwa ni pamoja na Mufunzo, Kikwajuni, Jamhuri, Mundu, Miembeni United, Miembeni FC, Polisi, Zimanimoto, KMKM, Chuoni, Chipukizi na Super Falcon.
Search This Blog
Thursday, October 27, 2011
LIGI KUU YA ZENJI YAPATA MDHAMINI KUANZA MWEZI UJAO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment