Search This Blog

Monday, August 22, 2011

WAKALA: INTER WAMETUMA OFA KWA AJILI YA KUYT


Inter wametuma ofa kwa Liverpool kwa ajili ya Dirk Kuyt, wakala wa mchezaji husika amesema.

Inter ambao kwa sasa wapo sokoni kutafuta mbadala wa Samuel Eto’o anaetarajiwa kujiunga na Anzhi, na sasa wakala Rob Jansen anasema timu hiyo ya Italia wametuma ofa kwa majogoo wa jiji kwa Mdachi Dirk Kuyt.

“Inter Milan wametuma ofa nzuri kwa ajili Dirk na mchezaji anafikiria juu ya ofa hiyo,” Jansen aliambia RTV West. “Ingawa, klabu hizo mbili bado hawajakubaliana juu ya dili hilo.”

Kuyt, ambaye alikuwa ndani ya kikosi cha Liverpool kilichoshinda dhidi ya Arsenal @Emirates wikiendi iliyopita bado ana mkataba na The Reds mpaka mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment