Mshambuliaji wa kihispania anayechezea timu ya Schalke 04 ya Ujerumani, Raul Gonzalez Blanco amevunja ukimya juu ya tetesi kuwa ataihama klabu hiyo.
Raul alikutana na viongozi wa Schalke wiki hii kujua hatma yake baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichofungwa 2-0 na HJK Helsinki katika mzunguko wa kwanza mechi za mtoano za Europa League katikati ya wiki hii.
Baada ya Schalke kuipiga chini ofa kutoka kwa Blackburn Rovers kwa ajili ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, kulikuwa na speculation kwamba Raul alikuwa anataka kuondoka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mmoja.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid, ambaye ataanza katika mchezo wa leo wa Bundersliga dhidi ya Mainz amekanusha kuhusu kutaka kuondoka na kusema kuwa ana furaha kubaki mjini Gelsenkirchen kwa ajili ya mwaka wa mwisho wa mkataba wake.
No comments:
Post a Comment