MATOKEO NI JKT RUVU KUIFUNGA YANGA BAO MOJA KWA SIFURI,
Yanga ilikuwa inatafuta bao la kusawazisha kwa nguvu bila mafanikio.
kutokana na kipigo hiki cha yanga BLOG yako inaipa mbinu Yanga pamoja na timu zingine namna ya kushambulia na kutafuta bao la kusawazisha na ikiwezekana kupata bao la ushindi pindi zinapokuwa nyuma.
huu ni mchoro unaokuonyesha namna ya kujipanga na kucheza mipira mirefu.
“Kuwafanya wapinzani wacheze mchezo wa mipira mirefu ni lazima timu iwalazimishe wapinzani kwa kuwasukuma kwenye upande wao . Wakati kipa wao akiwa na mpira washambuliaji wawili wanapaswa kuingia ndani kidogo kumpa kipa mawazo ya kupiga mpira mbele.
Kama akianza na beki wake wa kati unapaswa kumlazimisha apige mbele. Unafanya hivi kwa kuhakikisha wachezaji wote wanapanda kwa wakati mmoja . Washambuliaji wanapaswa kuwasukuma wapinzani hasa mabeki yaani “pressing’ huku mawinga wakiwalazimisha mabeki wa pembeni kurudi nyuma .
Wachezaji pekee ambao wanapaswa kuwa na nafasi kati yao na wapinzani ni mabeki wa kati ambao wanapaswa kuwapa washambuliaji nafasi kidogo.
Kama washambuliaji ndiyo wachezaji pekee wenye nafasi mabeki watapata moyo wa kupiga mbele kwa kuwa hakuna mtu mwingine wa kumpa .
Kama wapinzani wana mshambuliaji mfupi watakuwa wanataka kupitisha mipira ya chini au kwenye mistari .
Mbinu hii haitawaruhusu kufanya hivi . Hupaswi kuwaelekeza wachezaji kukaba ‘man-to-man kwani watapata nafasi ya kuzungusha mipira katikati ya watu na kutengeneza nafasi za kufunga .
1.Tumia mabeki wa pembeni
Waelekeze wachezaji wako wasogee mbele upande wa adui , hususani mabeki wa pembeni. Unaweza kufanya hivi kwa kumbadili beki wa pembeni na winga . Mpe ruhusa apande mbele. Hili litaruhusu timu nzima kupandisha mashambulizi mbele na kuunda wachezaji watatu wa mbele na kuwalazimisha mabeki wa timu pinzani kucheza ndani ya eneo lao.
2.Hakikisha hukamatwi.
Baki na mabeki watatu huku beki wa pembeni akibaki kama beki wa kati kukupa ulinzi . Kama unafukuzia mechi ambapo unahitaji bao wapinzani (timu inayoongoza) wana kawaida ya kuacha wachezaji wawili mbele ili kujaribu kufunga kwenye counter attack.
3. Kuwa mwepesi.
Kuhakikisha kuwa wachezaji wanapenya ngome ya adui.Lazima timu inayotafuta bao ijaribu kutumia njia ya kupitisha mipira pembeni mwa uwanja , iwe kwa kujaribu kupiga krosi au kuwaweka mabeki macho na kuhakikisha kuwa hawatoki kwenye lindo .
Kama washambuliaji wanajaribu kutafuta njia ya kuwapita mabeki inabidi timu inatafute njia kwa kutumia wachezaji wanne wa mbele kwa kumpa kiungo wa kati nafasi ya kuingia kwenye mashambulizi.
No comments:
Post a Comment