Jina: Emmanuel Okwi
Klabu: Simba
Nafasi: Mshambuliaji
Klabu ya zamani: SC Villa ya Uganda
Naamka asubuhi na mapema kabla ya saa 1:00, najiandaa halafu nafanya mazoezi ya kukimbia. Baada ya mazoezi narudi nyumbani na kupata kifungua kinywa.
Baada ya hapo, naangalia runinga na kusoma vitabu vya hadithi mpaka wakati wa chakula cha mchana. Nikimaliza chakula cha mchana huwa najiandaa kwenda mazoezini. Nikitoka mazoezini naoga na kupata chakula cha usiku kisha nalala ifikapo saa 3:00 usiku.
Klabu ipi unaipenda nje ya Afrika?

Naipenda Arsenal kwa sababu haina mashabiki wengi, pia wana soka safi.
Mchezaji yupi anayekuvutia duniani:
Mchezaji yupi anayekuvutia duniani:
Thierry Henry, pia napenda kucheza kama yeye.
Mchezaji yupi anayekuvutia Simba:
Mchezaji yupi anayekuvutia Simba:
Haruna Moshi ‘Boban’, ana kila kitu anachotakiwa kuwa nacho kiungo.
Tanzania
Club ipi ya usiku unayoiona inafaa Afrika Mashariki?:
Club ipi ya usiku unayoiona inafaa Afrika Mashariki?:
Club Silk ya Uganda
Chakula kizuri:
Chakula kizuri:
Matoke ya Uganda
Klabu ipi ya Afrika Mashariki inayolipa vizuri?:
Klabu ipi ya Afrika Mashariki inayolipa vizuri?:
Simba, wananipa mshahara mzuri, ambao sijawahi kulipwa katika soka.
Ni nchi ipi yenye uongozi bora wa soka Afrika Mashariki:
Ni nchi ipi yenye uongozi bora wa soka Afrika Mashariki:
Tanzania naweza kusema ina uongozi bora wa soka, ukianza kwa TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), wanafanya kazi zao vizuri na kwa umakini kubwa kuliko FUFA (Shirikisho la Soka Uganda), pia kwa ngazi ya klabu Simba ina uongozi imara, viongozi wake wanaelewana kuliko timu niliyotoka.
wanamuziki watatu unawaona bora kwako:
wanamuziki watatu unawaona bora kwako:
Ali Kiba, Jua Kali na Moses Radio.
nyimbo tatu unazoziona bora kwako:
nyimbo tatu unazoziona bora kwako:
This Bird and Bata (Moses Radio), Nakshi Nakshi Mrembo (Ali Kiba) na Salary wa Nameless
Andrew Mukasa wa SC Villa, huyu ni mshambuliaji wa kati aliye katika ‘fomu’ sasa.
Kwa nini unavaa jezi namba 25?
Kwa nini unavaa jezi namba 25?
Navaa jezi namba 25 kwa sababu nilizaliwa Desemba 25, sikuwahi kuivaa nilipokuwa SC Villa kwani kuna mchezaji niliyemkuta aliyekuwa akiivaa. Villa nilivaa namba 7.
Tueleze jambo lolote tusilolijua kuhusu wewe:
Tueleze jambo lolote tusilolijua kuhusu wewe:
Napenda kuwa karibu na familia yangu, hasa mama yangu. Mungu pia ndiye chaguo langu namba moja.
Ulipofunga bao dhidi ya Toto African ulishika kiatu na kuonyesha ishara ya kusikiliza simu, ulimaanisha nini?
Ulipofunga bao dhidi ya Toto African ulishika kiatu na kuonyesha ishara ya kusikiliza simu, ulimaanisha nini?
Ni bao langu la kwanza nilikuwa nikimtumia salamu mama yangu kumfahamisha.
Kama usingekuwa mwanasoka, unafikiri ungekuwa nani?
Kama usingekuwa mwanasoka, unafikiri ungekuwa nani?
Ningependa kuwa mwanasheria.
No comments:
Post a Comment