Search This Blog

Tuesday, August 9, 2011

VITUKO VYA WANASOKA...

John Terry hayuko peke yake katika kuvizia mademu wa wachezaji wenzake, Juan Roman Riquelme, umahiri wake dimbani umevuka mipaka hadi kwa wake za wachezaji wenzake. Vyombo vya habari vya Argentina mwezi Mei mwaka huu vilianika hadharani mara baada ya kuiweka hadharani ujumbe mfupi wa maneno kwa simu ambao Riquelme aliutuma kwa rafiki wa kike wa mchezaji mwenzake. Bahati mbaya, ‘shemeji’, uzalendo ukamshinda na kumwonesha Pablo Mouche ambaye naye aliuwasha moto.


Romario kwa kawaida huwa haishi misala mtaani. Akikataa kuchukuliwa kipimo cha kipima mwendo mara baada ya kunaswa na polisi akiendesha mwendo mkali, polisi walikiri kuwa ni hawakujua ni sababu ipi imemfanya Romario kukataa kuchukuliwa kipimo hiko. Ni huyu huyu Romario ambaye mwaka huu alitangaza nia ya kugombea nafasi ya uwakilishi bungeni, ‘sera yangu kuu ni kutaka kuwasadia watoto maskini’, alijigamba Romario. Lakini ni huyu huyu Romario ambaye alikuwa na mashtaka lukuki ya ukwepaji kodi, kuchunguzwa kwa kesi ya kuua kutoka na visa za michezo ya bahati nasibu, kuendesha gari huku akiwa amelewa, mali zake ikiwemo nyumba yenye thamani ya Dola milioni 4.4 kuwekwa rehani kutokana na madeni yake lukuki.




FAINALI za Kombe la Dunia zilizopita hivi punde zimecha historia mbalimbali kwa bara la Afrika, nzuri na mbaya pia. Lakini dunia inakumbuka kwa mazuri tu, ila si kwa ukweli kwamba pamoja na hayo mazuri mengi, takribani watu 20,000 nchini Soweto waliachwa bila makazi kupisha fainali hizo kuchezwa maeneo yao. Hii ni pamoja na wale waliopisha ujenzi wa viwanja pia na wale wakazi wa maeneo ya karibu na viwanja husika.
Sepp Blatter tangu kutangazwa kuwa Afrika Kusini itaandaa fainali za kombe la dunia alitoa ahadi kuwa atazifanya kuwa fainali ambazo matunda yake yatasambaa kwa wananchi wote wa Afrika Kusini. Tofauti na ukweli kwamba waathirika wa ‘bomoa bomoa’ hiyo kamwe hawakupata nafasi ya kukutana na FIFA hata pale
walipoandika barua mara kadhaa kuomba kufanya hivyo.



Kama unadhani wewe una nuksi au gundu kuliko watu wote duniani, basi ndugu yangu fikiri tena mara baada ya kusoma hii stori ya Michael Ballack. Miaka miwili tu iliyopita, 2008, matukio ya mwaka 2002 yalijirudia tena kwake, akiiongoza timu yake katika fainali ya Kombe la Mabingwa Barani Ulaya na wakati huohuo wakiwania kunyakua EPL.

Yaliyojiri ni kwamba, Ballack alivikosa vikombe vyote. Lakini kama vile haitoshi aliiongoza timu yake ya taifa kushika nafasi ya pili ya Kombe la Ulaya wakija nyuma ya mabingwa Hispania. Hapo bado hatuja hesabu medali za mshindi wa pili alizonyakua akiwa na Bayern Munich, 2004, na pia ligi kuu kwa misimu mitatu mfululizo ukiondoa msimu uliopita.
Mwisho kabisa, hivi unajua kuwa Ballack aliumia katika mechi yake ya mwisho kabisa ya msimu akiwa na klabu yake ya Chelsea wakicheza na Portsmouth, kitu kilicho muweka nje ya fainali za Kombe la Dunia mwaka huu?

Ballack hayuko peke yake, na si zaidi ya haya utakayoyasoma hapa chini yamhusuyo Paulo Maldini pale linapokuja suala la kuwa mshindi wa pili, na medali zake 12. Beki Paulo Maldini wa AC Milan ana medali za mshindi wa pili 17 — 3 za kombe la mabingwa barani Ulaya (1993, 1995, 2005), 3 za klabu bingwa dunia (1993, 1994, 2003), 2 za Copa Italia (1990, 1998) 2 za Supercoppa Italia (1996, 1999, 2003), 1 ya UEFA Super Cup (1993), 1 ya kombe la dunia (1994), 1 ya ubingwa wa Ulaya (2000). Huku timu yake ya AC Milan ikiwa naye ikishika nafasi ya pili mara tatu, (1990,1991 na 2005). Umeamini?


Kama timu yako unayoipenda katika ligi yoyote Barani Ulaya ikifungwa na ukashindwa hata kunywa, kula au hata kufikia kugombana na rafiki yako jua hauko peke yako.

Usain Bolt ambaye dunia inamtambua kama ni mwanadamu mwenye kasi zaidi kuliko wote ni nazi wa kutupwa wa Man Utd, na siku ilipochapwa mabao 3-0 na Everton duru la pili la msimu uliopita, sio tu alifika mazoezini kwa kuchelewa, pia alishindwa kufanya mazoezi huku akiibamiza luninga yake kupooza hasira.

No comments:

Post a Comment