Search This Blog

Sunday, August 21, 2011

Kwanini wachezaji Hispania wana haki ya kugoma.

Migomo sio suala geni kwenye soka nchini hispania, kumekuwa na migomo miwili katika kipindi cha miezi nane iliyopita .
Wa kwanza ulitokea mwezi disemba, ukianzia kwa wachezaji kupitia kwenye umoja wao (AFE) juu ya malipo ya mishahara kwa wanachama wake .


Mgomo huu ulifuatiwa na tishio toka kwa kampuni inayoendesha ligi (LFP) ambayo ililazimisha serikali ya hispania kubadilisha sheria itakayofanya mechi za mwishoni mwa wiki kulipiwa .
Pamoja na ukweli kuwa migomo yote hii ilizuiwa na mahakama, kulikuwa na hisia kuwa haya yalikuwa majaribo ya kuonyesha hisia ambazo zimekuwepo kwa muda mrefu.


Lakini hii ilikuwa tofauti kwa mgomo ambao umetokea wiki iliyopita, mgomo ambao hadi sasa umezuia kuanza kwa ligi ambayo hadi leo hii ingekuwa imechezwa raundi mbili. Mgomo huu umetokana na mzozo unaoendelea juu ya malipo ya mishahara ya wachezaji.
“hakika hili sio tishio dogo, ni kitu cha ukweli” alisikika akisema waziri wa michezo wa hispania Albert Soler ambaye aliitisha mazungumzo baina ya pande mbili zinazozozana.


Naye kipa namba moja wa timu ya taifa ya hispania na klabu ya Real Madrid Iker Cassilas alitoa kauli thabiti akisema kuwa “naweza kusema kwa uhakika kuwa hatutacheza”.
Kwa sasa kuna msuguano mkali baada ya miezi mitatu ya mazungumzo juu ya mkataba mpya kati ya pande mbili . Rais wa AFE Luis Rubiales anasema kuwa Euro milioni 40 ambazo LFP imetoa kama ofa ya kugharamia mishahara ya wachezaji ambao hawalipwi na vilabu vyao haitoshi na mgomo ndio njia pekee ya kutatua suala hili.
Hakutakuwa na michezo yoyote hadi hapo mkataba mpya utakaposainiwa alisema Rubiales wakati alipokuwa akizungumza na waandisho wa habari huku akiwa amezungukwa na wachezaji karibu 100 wakiwemo Iker Casillas,Xabi Alonso , Carles Puyol na Fernando Llorente . Wanachosema wachezaji ni kwamba hawataki fedha zaidi ila mikataba izingatiwe kwa mujibu wa rais wa AFE ambaye alisema kuwa Hispania imekuwa chini kuliko nchi zote barani ulaya kwenye suala la haki za wachezaji .
Rais wa LFP Jose Luis Astiazaran ambaye kwa upande wake aliwahi kuongoza mgomo mwezi mei alibishana na kauli ya rais wa umoja wa wachezaji akisema kuwa haelewi sababu za mgomo unaoendelea hivi sasa : “Sidhani AFE wana sababu za kuitisha mgomo .


Rais huy anasema kuwa fedha kiasi cha Euro millioni 70 zimewekwa kando kwa ajili ya malipo ya wachezaji huku nyingine Euro milioni 30 zikitumika kwa miaka mitatu na zilizobaki kwa miaka minne .
AFE ilijibu kwa kusema kuwa fedha zilizopo kiukweli ni Euro milioni 40 tuna pia Ligi ina deni inalodaiwa na wachezaji ambalo ni Euro milioni 50 kwa wachezaji 200 . “Tunachotaka kuona ni hali ya mashindano ambapo wachezaji wa timu zote wana mazingira yanayofanana” , ni kauli ya AFE .
Hoja hii inaungwa mkono na ukweli kuwa kati ya timu 20 za Ligi kuu ya hispania , kati yake zimefirisika na ziko chini ya usimamizi maalum wa serikali yaani Administration. Wachezaji toka timu iliyopanda daraja ya Rayo Vallecano ndio kwanza wameanza kulipwa fedha walizokuwa wanaidai klabu yao kwa kipindi cha miezi 14 iliyopita .



LFP inasema kuwa hakuna fedha za kuipa AFE na wanachotaka wao kama Ligi ni kuzungumza ili kufikia muafaka . ‘Tunawezaje kutoa fedha ambazo hatuna? Alihoji Rais wa ligi.
Kama mgomo ukiendelea hali itakuwa hatari kwa kuwa ratiba nzima ya ligi itavurugika huku kukiwa na mlolongo wa mechi za katikati ya wiki kama zile za Ligi ya Mabingwa , Kombe la Mfalme yaani Copa Del Rey na mechi za tarehe za kimataifa za FIFA na za UEFA .


Hii italazimu ligi kufuata mapumziko ya wakati wa Krismasi jambo ambalo AFE inalipinga pia.
AS ambalo ni gazeti maarufu la michezo Hispania limeutaja mgomo unaoendelea kama balaa huku Marca wakiionya AFE kuwa ni lazima ielewe kuwa mgomo huu una madhara makubwa sana ambayo yatafika mbali.
Mwandishi Emilio Perez de Rozas wa jarida la Sport amelalamikia uendeshwaji mbovu wa soka la Hispania uendeshwaji ambao umevishuhudia vilabu vikidaiwa madeni ambayo yanafikia Euro Bilioni 3.5 huku pia vilabu vikidaiwa kodi zinazofikia Euro millioni 694. “Kinachoshangaza ni kwamba kiongozi wa LFP ndio mtu yule yule aliyeiua klabu ya Real Sociedad ’’ anasema mwandishi huyo wa jarida la Sport akimzungumzia Rais wa LFP Astiarazan ambaye aliwahi kuwa Rais wa Real Sociedad.
Mgomo ulioitishwa na na AFE kwa vyovyote utaleta majonzi makubwa kwa mashabiki wa soka nchini Hispania na hata wale walioko nje ya nchi hiyo ambao walipanga kusafiri kwenda kushuhudia mechi za ligi ya Hispania . Hata hivyo hali ni mbaya kiasi kwamba wachezaji hawana njia nyingine zaidi ya kugoma.
Kila mwaka kuna wachezaji wengi ambao hawalipwi na ahadi ni lazima zitimizwe ”anasema kocha wa Malaga Manuel Pelegrinni.
Mgomo huu hauwaathiri watu kama Casillas na Puyol japo wameuunga mkono kwa asilimia zote lakini wenzao wanaotoka kwenye timu ndogo na pia wale walioko kwenye madaraja ya chini ya ligi ambako mishahara inachelewa na hata pale inapofika inakuwa imeshapungua.

Uendeshwaji mbovu wa soka nchini Hispania na utumiaji mbaya wa miundo mbinu haupaswi kupelekea wachezaji kugoma kwa kwa hawawezi kununua mafuta kwa ajili ya magari yao ili waende mazoezini kama ilivyotokea kwa Rayo Valecano msimu uliopita.
Mgomo huu hautabadilisha hali za wachezaji na kwa vyovyote kuna vilabu vinaathirika kwa kukosa mapato muhimu katika kipindi hiki . Lakini kwa bahati mbaya AFE haina njia nyinginr zaidi ya mgomo ili kuleta muafaka na ni lazima wachezaji wagome hadi hapo matatizo yao yatakapotatuliwa.

No comments:

Post a Comment