HIZI NI TICKET ZILIZOTUMIKA KWENYE MCHEZO WA COASTAL UNION vs MTIBWA SUGAR KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI SIKU YA JUMAMOSI ( 20/08/2011 ).
viingilio vikiwa ni Tsh 3,000 KWA 5,000
kinachosikitisha ticketi za shilingi 3,000 zilikuwa ni tiketi zilizotumika kwenye mchezo wa msimu wa 2009/10 ( 24/2/2010 ) kwenye uwanja wa MAJIMAJI mjini Songea kati ya Majimaji na Kagera Sugar.
na tiketi za shilingi 5,000 zilikuwa ni za mchezo uliochezwa NOVEMBA 24,2007 KATI YA ASHANTI na COASTAL UNION kwenye uwanja wa USHIRIKA MOSHI.
WADAU NINI MAONI YENU JUU YA HILI!!
Dear Shaffii,
Please find attached tickets that were used kwenye game namba 1 ya premier kati ya Coastal Union Sports Club na Mtibwa, Tanga tarehe 20/08/2011.
Hivi kweli kitu kama hiki kinafanyika duniani kwingine jamani. Hivi institution kubwa kama hii wanawezaje kufanya dharau ya namna hii kwenye mchezo unaopendwa na wengi. Hapa huu ni wizi moja kwa moja kwani mahesabu huko yanapigwa kwamba kumechapishwa tickets while watu wanachakachua. Hizi ticket gharama yake ilikwisha kuwa met lakini chakushangaza bado katika makato gharama za tiketi zinaonyeshwa, this is daylight robbery na bila aibu. Auditors wanasemaje juu ya kitu kama hiki jamani?Tumeingiza mil 8 baada ya kuibiwa na mgao tumeambulia 1.9mil hebu angalia unyang'anyi huu.
Kama nilivyokueleza kuhusu leseni. Tumelipia leseni kwa wachezaji 38 badala ya 46 ambayo inajumuisha 25 senior players and 21 under 20 players. Na nimelipia 38 kwasababu nilikwenda na pesa nikiamini leseni moja ni sh 5,000 lakini nikaambiwa ni 7,000. Cha kushangaza pia why TFF wafanye biashara? Nasema hivi kwasababu wanasema wenyewe wanatengeneza leseni moja kwa 5,500 kuna sababu gani ya kutucharge 7,000? Sijui details za mkataba wa udhamini lakini naamini hizi ni costs ambazo zingekuwemo kwenye mkataba lakini kama hazimo hakuna sababu ya TFF kufanya faida, hili ulisemee mkuu. Tuendelee, baada ya kulipa nikaambia leseni zitakuja na match commissioner bila kuniambia kama wanaleta za wakubwa tu ila za under 20 zitatengenezwa upon request, ningejuaje hayo? Matokeo yake zimeletwa leseni 25 za wakubwa na hii ilitukosesha kuwatumia 3 key players ambao wako under 20. Nimelalamika kwa Saad (mkurugenzi wa mashindano wa tff ) na yeye kukubali ni kosa lao wao lakini hata nilipotoa wazo la kupiga picha wachezaji na match commissioner alikataa kata kata lakini leo Yanga wameruhusiwa kucheza bila leseni. Nakushukuru sana kwa kuwa msemaji wa wanyonge bila kujali itikadi ya klabu unayoi-support. Katika hali hii hatufiki kwani kumekuwa na malalamiko kwamba TFF imejaa Yanga, ni ya ukweli na watu hawakatazwi lakini unapoacha uwe mtumwa wa itikadi ya klabu yako kwakweli hufai kuwa kiongozi au mwandishi wa habari.
Naomba fanyia kazi at least sauti zetu zisikike
WARAKA HUU UMETOKA KWA MDAU !!
naomba majina ya wachezaj wa coast msimu huu,hongera kwa kuwa wa kisasa katika utendaji wako,your like kampun ya goal
ReplyDeletecom,nadhan tiefuefu wakuige
naomba majina ya wachezaj wa coast msimu huu,hongera kwa kuwa wa kisasa katika utendaji wako,your like kampun ya goal
com,nadhan tiefuefu wakuige