Search This Blog

Monday, August 22, 2011

ARSENE WENGER AFUNGIWA MECHI 2

Arsene Wenger amefungiwa mechi mbili baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja sheria kwa kukiuka mipaka ya kifungo cha mechi alichoadhibiwa na UEFA katika mechi ya kwanza UCL play off dhidi ya Udinese.

Wenger amepatikana na hatia ya kutoa maelekezo kwa kocha msaidizi kutokea jukwaani katika mechi dhidi ya Udinese kupitia msaidizi wake wa pili Boro Primorac kwenda msaidizi wake wa kwanza Pat Rice.

UEFA pia wameipiga faini ya £8,743 Arsenal kwa makosa yaliyofanywa na wafanyakazi wake wakati wa mechi, hata hivyo Wenger na klabu wanayo nafasi ya kukata rufaa.

No comments:

Post a Comment