Ligi kuu ya England imeamua kuachana na sheria ya kutoa adhabu kwa timu zitakazopeleka vikosi dhaifu kwenye michezo ya ligi hiyo . Kwa sasa Timu za ligi kuu zitaruhusiwa kuchezesha mchezaji yoyote aliyemo kwenye kikosi cha wachezaji 25 siku ya mechi bila kuogopa kukumbana na adhabu yoyte kama ambavyo imewahi kutokea kwa timu za Wolves na Blackpool ambao walitozwa faini ya paundi 25,000 baada ya kocha Ian Holloway kufanya mabadiliko 10 kwenye kikosi chake cha kwanza.
Mkutano uliowakutanisha wadau ambao ni vilabu 20 vya vya ligi kuu nchini England ulifikia makubaliano kuwa mchezajo yoyote kati ya wachezaji 25 walioko kwenye timu anaweza kuchaguliwa kwenye mechi , sheria hii hata hivyo haiwahusu wachezaji walioko kwenye vikosi vya wachezaji wadogo yaani “reserve” na timu itakumbwa na adhabu ya faini kama itachagua wachezaji toka kwenye vikosi vya reserve kwa ajili ya mechi .
Msemaji wa Premier League Nick Noble amesema kuwa sheria hii inaruhusu vilabu kuchagua idadi yoyote ya wachezaji wa vikosi vya wachezaji walio na umri chini ya miaka 21 hivyo sheria hii itavibana vilabu kutotumia idadi kubwa ya wachezaji toka vikosi vya vijana ili kulinda heshima ya mchezo wa soka na ligi kwa ujumla .
Itakumbukwa kuwa Novemba iliyopita , Blackpool walitoka sare ya mabao 2-2 wakiwa nyumbani dhidi ya Everton na siku nne baadae kocha Ian Holloway alifanya mabadiliko 10 kwenye kikosi chake kilichovaana na Aston Villa na matokeo yake ilikuwa ni fine ya paundi 25,000.
No comments:
Post a Comment