Search This Blog

Friday, July 15, 2011

MESHACK ABEL: "SIMBA NIACHENI NIONDOKE NA SITAKI KUCHEZA RUVU SHOOTING"


Masaa machache baada ya uongozi wa klabu ya Simba kutangaza kumpeleka kwa mkopo katika klabu ya Ruvu Shooting, beki Meshack Abel ameongea na blog hii na kufunguka juu sakata hilo la uhamisho wake.

"Kiukweli nimeshangazwa sana na taarifa hizi za mimi kupelekwa kwa mkopo Ruvu Shooting, kwa sababu mimi nilishakataa kwenda huko.Jumatatu iliyopita Uongozi uliniita na kuniambia juu ya suala hili na mimi nikawaambia siwezi kwenda Ruvu, ni bora wanipe barua ya kuniacha ili niende nikatafute timu ninayoitaka mwenyewe lakini uongozi ukaniambia mimi ndio niandike barua ya kuvunja mkataba.Kutokana na sharti hilo nikashindwa coz sikuwa na uwezo wa kulipia gharama za contract termination, hivuo nikawaomba waniache nitafute timu mwenyewe lakini sitaki kuichezea Ruvu Shooting.

"Kiukweli Simba wamekuwa hawanitendei haki tangu wanisajili, mpaka sasa nawadai fedha zangu za usajili za mwaka jana, waliniahidi kunilipa kwa kunipa gari lakini mpaka msimu unaisha sikupewa kitu, na wakati tunajiandaa kwa ajili ya mechi ya pili ya Motema Pembe niliumia hivyo nikashindwa kuitumikia klabu, lakini cha ajabu mwisho wa mwezi(May) ulipofika walinikata mshahara wangu eti kwa madai walitumia fedha waliyonikata kunitibia majeraha niliyoumia nje ya Simba.

"Mambo yote haya niliyavumilia lakini sasa imefika mwisho, nahitaji uongozi wa klabu ya Simba waniache niende sehemu ninayoitaka kama walivyowaachia Haruna Shamte na Jabu kuchagua sehemu wanazozitaka."

Meshack ambaye alihamia Simba akitokea Mtibwa Sugar anasema tayari amepeleka maombi rasmi ya kuomba Simba wamuandikie barua ya kumuacha kwa sababu ameshapata timu ya kuichezea nchini Botswana, "Niliongea na katibu na nimweleza kuwa nimepata timu inayotaka kunisajili nchini Botswana inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo "Tigers Sports Club, na kama mambo yakienda vizuri Jumapili natarajia kwenda Gabarone kumalizana nao.Naamini bado nina uwezo mkubwa wa kucheza na nitathibitisha uwezo wangu ndani ya msimu mmoja tu."


No comments:

Post a Comment