Search This Blog

Monday, July 4, 2011

11 BORA KUTOKA SHAMBANI LA MASIA




LA MASIA ni neno la kihispania lenye maana ya nyumba ambayo inakuwa ndani ya shamba.
La Masia ni jina la kituo cha mafunzo ya soka cha klabu bingwa ya ulaya Barcelona F.C.Ndani ya academy hii wamepatikana wachezaji ambao wameupa mchezo wa soka ladha ya kusisimua.Kutokea katika kizazi cha baba mzazi wa Sergio Busquets mpaka kizazi hiki cha akina Leo Messi.
La Masia ilifunguliwa katika miaka ya 1970s kutokana na ushauri wa mchezaji aliyekuwa akiondoka katika klabu hiyo Johan Cruyff.
Mdachi huyu ambaye ni moja ya wachezaji waliofanikiwa sana akiwa ndani ya kikosi cha Catalan club, lakini mpaka anaondoka Nou Camp mwaka 1978, Barca bado walikuwa wanakikimbiza kivuli cha wapinzani wao wakubwa Real Madrid.Hivyo Johan Cruyff alimwambia raisi aliyekuwa akiingia madarakani kipindi hicho Josep Lluis Nunez kuwa ili kuweza kukabiliana na kuwashinda Madrid inabidi wafungue kituo bora cha soka kama ambacho Ajax Amsterdam wanacho.
Matunda ya kituo hiki cha soka yalianza kuonekana kipindi Cruyff aliporudi Nou Camp akiwa kocha miaka 10 baada ya kuondoka Catalunya, na tangu wakati huo La Masia imetoa mchango mkubwa katika kutoa wachezaji ambao wameiletea mafanikio makubwa timu ya Barcelona na Spain national team katika kuutawala ulimwengu wa soka.
Ndani ya kipindi hiki cha usajili vipaji kutokea katika shamba la LA MASIA wamekuwa gumzo na sasa kupitia blog hii tunawaletea listi ya wachezaji 11 waliotengenezwa la masia waliowahi na wanaoutikisa ulimwengu wa soka duniani.


GUILLERMO AMOR

Age: 43


Position: Midfielder


Country: Spain (37 caps, 4 goals)


Career apps: 524 (69 goals)


Barca apps*: 421 (67)


Trophies at Barca: 17


La Masia fact: Amor alikuwa ndio mchezaji wa kwanza kutoka La Masia kufanikiwa katika kikosi cha kwanza cha Barca.



Guillermo Amor alizaliwa katika katika sehemu maarufu ya utalii eneo la Benidorm, lakini alijulikana zaidi katika maeneo ya fukwe za mji wa Barcelona baada ya kufaulu kutoka La masia na kung'ara katika kikosi cha Johan Cruyff.Kiungo huyu alifanikiwa kucheza michezo 40 katika kikosi cha Spain, aliwakuwemo ndani kikosi cha Barca kwa mara 400 huku akishinda makombe 17 katika timu iliyokuwa inaundwa kocha wa sasa wa Barca Pep Guardiola, Hristo Stoichkov, Micheal Laundrup, Romaria na baadae Ronaldo na Luis Figo.Miaka 10 baada ya kuitumikia Catulanya, Amor aliuzwa Fiorentina na kocha Louis Van Gaal mwaka 1998.




SERGIO BUSQUETS

Age: 22


Position: Midfielder


Country: Spain (30 caps, no goals)


Career apps: 170 (4 goals)


Barca apps*: 139 (5)


Trophies at Barca: 10


La Masia fact: Sergio na baba yake Carles Busquets ambaye alikuwa golikipa wa zamani wa Barca wote ni madini ya La Masia.


Sergio Busquets ana umri wa miaka 22 tu, lakini kiungo huyu mkabaji ameshashinda makombe 10 tangu aingie katika kikosi cha kwanza mwaka msimu 2008-09.Ameshajitegenea nafasi ya kudumu katika vikosi vyenye ushindani vya Barca na timu ya taifa ya Spain.


CESC FABREGAS

Age: 24


Position: Midfielder


Country: Spain (58 caps, 4 goals)


Career apps: 303 games (57 goals)


Barca apps*: -


Trophies at Barca: -


La Masia fact: Fabregas anakumbuka aliambia siku moja na Guardiola, "Siku moja utakuwa utakuwa namba


Cesc Fabregas ndio mchezaji pekee katika listi hii ambaye hajawahi kuichezea Barca katika kikosi cha kwanza, lakini historia hii inaweza kufutika hivi karibuni.

Fabregas akiwa ndani ya La Masia kocha wake alikuwa anamficha pindi maskauti wanapokuja kuangalia wachezaji, kwa sababu aliogopa angechukuliwa lakini mwisho wa siku alishindwa kumzuia pindi mchezaji alipoona ufinyu wa nafasi yake katika kikosi cha wakubwa hivyo akaamua kujiunga na Gunners akiwa na miaka 16.

Kwa sasa akiwa na miaka 24 Barcelona wanajipanga kumrudisha Cesc nyumbani.Inakumbukwa kipindi wazazi wake Fabregas walipotengana, Guardiola alikutana na Fabregas na kutia saini katika fulana ya Cesc na akaandika "One day you will be Barca's No. 4." kitu ambacho kinaweza kikatokea muda wowote kutokea sasa.



PEP GUARDIOLA

Age: 40


Position: Midfielder


Country: Spain (47 caps, 5 goals)



Career apps: 477 (25 goals)


Barca apps*: 384 (11)


Trophies at Barca : 16 (plus 10 more as coach)


La Masia fact: Pep alikuwa ni kijana muokota mipira Nou Camp.

Pep Guardiola siku zote amekuwa akijuta maisha yakiungana na Barca.Guardiola alipoingia La Masia kama mchezaji aliwapigia simu wazazi wake na akawaambia ni jinsi gani alifurahi kuwepo mahali pale kwani alikuwa anaweza kuona uwanja wa Nou Camp kupitia dirisha la chumbani kwake.Hata baadae alipoondoka kwenda kucheza nchini Qatar na Mexico uwanja ule haujawahi kuwa nje ya mawazo yake.Guardiola kama mchezaji aliacha alama ya kukumbukwa ndani historia ya Barca, ingawa hakufunga mabao mengi, hakuwa mwepesi lakini alikuwa fundi na kiungo muhimu katika kikosi cha Johan Cruyff, Bobby Robson na baadae Van Gaal.Sasa anafanya walichokuwa wanafanya makocha wake akiwa na mafanikio zaidi.


ANDRES INIESTA ALIPOKUWA DOGO

Age: 27


Position: Midfielder


Country: Spain (58 caps, 9 goals)


Career apps: 415 (38 goals)


Barca apps*: 363 (33)


Trophies at Barca: 15


La Masia fact: Iniesta alikuwa na picha ya Guardiola aliyoibandika katika ukuta wa chumba chake alipokuwa La Masia.

Andres Iniesta ametokea katika ukanda wa Albacete - Spain, lakini wazazi wake walikuwa wanafahamiana na kocha wa Barcelona hivyo walimuomba amchukue mtoto wao afanye majaribio na timu hiyo.Barca waliona kipaji chake na Iniesta akahamia La Masia, ingawa ilikuwa vigumu sana kwa Iniesta kutengana na wazazi wake anakiri alilia sana kwa tukio hilo.

Kijana huyu mwenye aibu, uwezo wake unajidhihilisha wenyewe uwanjani akiwa na swahiba wake XAVI wametengeneza mfumo ambao ni hatari kwa sasa kwenye ulimwengu wa soka.Mwaka jana wote wawili walitajwa katika kugombea tuzo za Ballon d'Or . Pia Iniesta amewahi kutajwa na Wayne Rooney kama ndiye kiungo bora.Mwaka jana Iniesta ndio alifunga bao lililoipa ubingwa wa dunia timu ya taifa ya Spain, pia ameshinda makombe 15 akiwa na Barcelona.





LIONEL MESSI

Age: 24


Position: Forward


Country: Argentina (56 caps, 17 goals)


Career apps: 291 (186 goals)


Barca apps*: 269 (180)


Trophies at Barca: 15


La Masia fact: Messi Barca baada ya klabu hiyo kukubali kulipia matibabu kwa ajili ya ugonjwa wa upungufu wa homoni.


Lionel Messi amekuwa akitajwa kuwa ndio mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya soka, lakini inawezekana asingekuwa mchezaji kabisa kwa kuwa Margentina huyu alikuwa na matatizo ya upungufu wa homoni za ukuaji na familia yake ikiwa haina uwezo wa kugharamikia matibabu na hakuna klabu yoyte nchini Argentina ilikuwa tayari kumsaidia hivyo Barca kupitia scouts wake waligundua kipaji cha mchezaji na wakaamua kulipia matibabu, kilichofuata na kila mtu anajua.

Messi alikuwa mdogo sana alipojiunga na kikosi B ndani la masia hata kufikia Gerard Pique kuwahi kusema wachezaji wenzie walikuwa hawajui kwanini alikuwepo pale.Messi kwa sasa ni star asiyeshindika ndani ya historia ya Barcelona akiwa amefunga magoli 100 ndani ya misimu miwili iliyopita pekee.Ama kwa hakika Barca hawatajuta kamwe kulipia gharama za matibabu yake.


PEDRO RODRIGOEZ

Age: 23


Position: Forward


Country: Spain (13 caps, 2 goals)


Career apps: 177 (62 goals)


Barca apps*: 122 (45)


Trophies at Barca: 10


La Masia fact: Pedro ni moja kati ya wachezaji watatu waliopandishwa timu ya wakubwa na Pep Guardiola mara baada ya kuwa manager.


Pamoja na kuwa kipaji, Pedro anakumbukwa na watu wa La Masia kutokana na kujituma kwake.Alizaliwa mjini Tenerife, alikwenda Catulunya akiwa kijana mdogo na haraka akafanikiwa kumvutia kocha wa timu B - Guardiola katika msimu wa kwanza, na mara Guardiola alipopandishwa katika kikosi cha kwanza akamchukua Pedrito.

Winga huyu sasa ni moja wachezaji tegemeo katika kikosi cha Guardiola akiweka rekodi ya kufunga katika mashindano sita tofauti ndani ya msimu 1.Pedro pia ni mmoja ya wachezaji watatu waliopeleka kiio jijini Manchester baada ya kuitungua United katika UCL final 2011.Uwezo anaouonyesha Barca umemuongezea imani kwa kocha wa timu ya taifa ya Spain.



GELARD PIQUE AKIWA FABREGAS LA MASIA

Age: 24


Position: Defender


Country: Spain (33 caps, 4 goals)


Career apps: 196 (16 goals)


Barca apps*: 145 (11)


Trophies at Barca: 10


La Masia fact: Pique alianza kucheza kama kiungo mkabaji akiwa La masia.


Gerard Pique aliondoka Barca akiwa mdogo na kwenda kujaribu bahati yake nchini England kama ilivyokuwa kwa Fabregas, lakinit tofauti na mwenzie Pique alikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara akiwa na United hivyo akapelekwa mkopo Zaragoza na baadae akarudi tena United.

Pep Guardiola aliamua kumrudisha Pique nyumbani na baba Shakira akaishinda vita ya kugombea namba ya kushirikiana na Carles Puyol dhidi ya Rafael Marquez na Gabi Millito, halafu akafanikiwa kujenga moja ya safu bora za ulinzi duniani ndani ya kikosi cha Barca na timu ya taifa ya Spain.


CARLES PUYOL

Age: 33


Position: Defender


Country: Spain (94 caps, 3 goals)


Career apps: 605 (15 goals)


Barca apps*: 516 (9)


Trophies at Barca: 15


La Masia fact: Puyol alikuwa anakaribia kuuzwa kwa Malaga.


Carles Puyol alianza kucheza soka kama beki wa upande wa kulia na alipewa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na mdachi Van Gaal.Ingawa alikuwepo Barca kwa muda mrefu lakini ilimbidi kusubiri mpaka mwaka 2004 kuweza kushinda kombe.Tangu kipindi hicho, Puyol ameendelea kushinda makobe kila kukicha, akiwa tayari ana medali 3 za Champions League, 5 za la liga na medali nyingine tofauti.

Puyol ni kiongozi asiyetia shaka ndani ya timu, akiwa beki wa kati anajua jinsi ya kuwapanga wachezaji wenzake, anajituma nakufanya kazi kubwa katika kuondoa na kupanga mashambulizi ya timu.Kufungwa kwa Barca mara nyingi katika msimu uliopita kulitokea alipokosekana uwanjani, kitu ambacho kinaelezea vizuri umuhimu wake ndani ya timu hiyo.



VICTOR VALDES AKIWA PEPE REINA

AGE : 29


Position: Goalkeeper


Country: Spain (4 caps)


Career apps: 483


Barca apps*: 406


Trophies at Barca: 15


La Masia fact: Valdes aliwahi kuondoka Barca na kwenda Tenerife kwa miaka 3 lakini baadae alirudi.


Victor Valdes alianza kuwemo ndani ya kikosi cha Barca chini ya Radomir Antic na alishikilia nafasi yake hata baada ya kuingia kwa raisi Joan Laporta ambaye alimsajili Rustu Recber . Valdes amekuwa mtu asiyeshindika katika nafasi yake akiwa moja ya magolikipa bora katika kizazi hiki cha soka.

Valdes sio golikipa pekee aliyetokea La masia , Pepe Reina nae alitokea shambani.




XAVI HERNANDEZ AKIWAKILISHA

Age: 31


Position: Midfielder


Country: Spain (101 caps, 9 goals)


Career apps: 638 (62 goals)


Barca apps*: 577 (58)


Trophies at Barca: 16


La Masia fact: Xavi alikuwa ndani ya kikosi cha Barca B kilichofanikiwa kucheza ligi ya daraja la pili mwaka 1998.


Xavi alionekana ndio mrithi wa Pep Guardiola, kitu ambacho kilimpa mzigo mkubwa kijana mdogo kutokana na mategemeo makubwa juu yake, hali ambayo ilipelekea Xavi kufikiria kuondoka Barca.Xavi alipata nafasi katika kikosi cha kwanza baada ya Guardiola kuumia na baadae alimrithi kabisa baada ya Pep kuondoka Nou Camp kelekea Brescia.

Kwa sasa Xavi amejiandikia historia ya kuwa moja ya viungo bora kuwahi kutokea katika historia ya soka duniani, na amekuwa ndio moyo wa klabu yake na timu ya taifa ya Spain.


No comments:

Post a Comment