Hapo jana jioni kilifanyika Kikao kati ya CECAFA na wawakilishi wa vilabu vilivyoingia hatua ya Robo Fainal ya Michuano ya KAGAME CASTLE CUP.
Kwa pamoja walikubaliana mambo yafuatayo:
1} Kadi zote za Njano ambazo wachezaji walikuwa nazo kabla ya michezo ya robo fainal zimefutwa na kuanzia michezo ya robo fainal kila timu itaanza na Clean Sheet ya Card kasoro wachezaji wawili wa timu ya Ulinzi ambao ni Antony Edridu aliyepata kadi nyekundu kwenye Mchezo Uliopita na Laurence Owino ambaye ana kadi mbili za njano pamoja na Ssali Edward wa klabu ya Bunamwaya ambaye ana kadi mbili za njano ndio watakao kosa michezo ya Robo fainal na timu zao.
2} Kwa Michezo ya Robo fainal na ule wa kumtafuta mshindi wa tatu baada ya dakika 90 sheria ya Mikwaju ya Penalt itatumika,kasoro michezo ya nusu fainal na fainal ndipo italazimika kutumia dakika 30 za ziada kama timu zitachoshana nguvu katika muda wa kawaida.
NA
3} Timu zitakazofuzu katika Michezo yao ya Robo fainal ya kwanza siku ya Jumanne ya tarehe 5 ndizo zitakazocheza nusu fainal ya kwanza siku ya Alhamis ya tarehe 7 ya mwezi huu.
Wakati, Huo huo takwimu za Michuano hii hadi hivi sasa ni kama Ifuatavyo,
Simba ndiyo timu yenye nidhamu hadi hivi sasa baada ya kuwa na kadi mbili tu za njano toka mchezo wao wa kwanza,wakati timu ya Ports Fc ya Djibouti ndiyo inaongoza kwa kuwa na kadi nyingi za njano(11),
Pia jumla ya kadi za njano 66 na kadi 9 nyekundu zimekwisha tolewa hadi sasa.
Jumla ya magoli 67 yamekwishafungwa kwa vituo vyote viwili vya Dar es Salam na Morogoro.
No comments:
Post a Comment