Search This Blog

Tuesday, June 21, 2011

USAJILI BARANI ULAYA



JUVENTUS YATHIBITISHA KUMTAKA AGUERO

Kibibi kizee cha Turin Juventus wamethibitisha kwamba wanajipanga kupeleka ofa kwa Atletico Madrid ili kuweza kupata saini ya mshambuliaji wa Kiargentina Sergio Aguero.
Aguero ambaye ameshasema anataka kuhama anauzwa kwa kiasi cha euro million 45, na amekuwa pia akihusishwa na klabu za Chelsea, Real Madrid na Man City.
"Aguero ni mchezaji mkubwa na ninaposema nataka kukijenga upya kikosi cha Juve, namaanisha kuwa namuhitaji Margentina huyo" - amesema kiongozi wa Juventus Giuseppe Morotta.




VARANE: KUJIUNGA NA UNITED KUTANIFURAHISHA

Beki wa kimataifa wa Lens ya ufaransa ambaye amezifanya klabu za Man United na Real madrid kupigana vikumbo kupata saini yake, amesema kuwa ni heshima kubwa sana kwake kutakiwa na vilabu hivyo vikubwa barani ulaya ila endapo atajiunga na Manchester United atafurahi zaidi.



BARCA YAMUONA RAFAEL KAMA MRITHI WA ALVES

Barcelona wanaonekana kuvutiwa na beki wa kibrazil anayechezea klabu ya Man United Rafael Da Silva kwa mujibu wa El Mundo Derpotivo.
Catalunya wanamuona Rafael kama mrithi sahihi wa DanI Alves ambaye amesaini mkataba mpya na Barca mwanzoni mwa mwaka huu, lakini UEFA champions league club wanapanga kuwa timu yenye mipango ya muda mrefu, hivyo wanamuona Rafael ni moja ya wachezaji wanaotakiwa kujiunga na timu hiyo.




FABREGAS ANAFANYA KILA AWEZALO KUJIUNGA NASI - RAISI WA BARCA

Sandro Rosell raisi wa klabu ya Barcelona amekiri kuwa klabu yake haipo tayari kulipa kiasi cha paundi millioni 35 ili kuweza kupata huduma za Cesc Fabregas kutoka Arsenal, huku akisema kiungo huyo anafanya kila analoweza ili kukamilisha ndoto yake ya kujiunga na klabu bingwa hiyo ya ulaya.



JAMIE O'HARA AJUNGA RASMI NA WOLVES

Jamie O'Hara amekamilisha uhamisho wa paundi mil 5 kutoka Tottenham na kujiunga na Wolves kwa mkataba wa miaka 5 CEO wa klabu ya Wolves amethibitisha.





No comments:

Post a Comment