FALSAFA YAKE
Anapenda zaidi timu yake icheze mchezo wa kushambulia, ndio falsafa aliyoitumia akiwa Porto huku mashambulizi hayo yakiongozwa na Facao na mwenzie Hulk.Villa Boas anasisitiza washambuliaji wake ndio wahusika wakuu wa falsafa yake, lakini yupo Pep Guardiola ndani ya Barca.
LAMPARD NA ATEGEMEE NINI?
Manager huyu mpya wa Chelsea hana muda wachezaji wavivu na ameonya: "Kama kiungo atakuwa hapigani kwa ajili ya timu basi hana nafasi ndani ya timu yangu."
ANADILI VIPI NA WACHEZAJI WAKE?
Anaongea nao kwa muda mwingi, ingawa anapenda sana kuubadilisha mfumo wa maadili ya kazi katika mtindo wake mwenyewe.Villa Boas ni muwazi sana kuhusu vitu anavyotaka.
UTOFAUTI WA MAFUNDISHO YAKE?
Mreno huyu anapenda kufundisha kwa kutumia mbinu tofauti.Ana kawaida ya kutumia dakika 30 kufundisha mbinu siku moja baada ya kila mechi na pia kila baada ya muda wa mazoezi ya kawaida katika kuhakikisha wachezaji wake wanashika mafundisho yake."
WACHEZAJI AMBAO CHELSEA WANAWEZA KUWASAJILI SASA.
Atasajili zaidi wachezaji wa kigeni.Villas Boas amejenga sifa kupitia wachezaji kama Falcao na Hulk wakiwa ni wachezaji wa kigeni.Msimu uliopita ndani ya kikosi cha Porto alikuwa na wachezaji 17 kutoka Amerika ya Kusini huku wachezaji wa kireno wakiwa 6 tu.
ANASHIRIKIANA VIPI NA VYOMBO VYA HABARI?
Hapa tatizo kidogo, Villa Boas sio Jose Mourinho.Anafanya mahojiano na media mara chache sana na hata alipokuwa Porto huu ndio ulikuwa ndio utaratibu wake.
No comments:
Post a Comment