ROMAN ABRAMOVICH anaendelea kufanya matanuzi ya pesa baada ya kukaribia kumnasa Andre Villas-Boas kuja kuifundisha Chelsea kwa kulipa paundi million 13.25.
Kiasi hicho cha kuweza kumnyakua Villas Boas a.k.a Special One 2 ni rekodi ya dunia kwa uhamisho wa makocha, na mmiliki wa The Blues anaweza kutumia paundi mil 26.6 kwa ajili ya kumleta mshambuliaji wa Porto Falcao.
Mlinzi wa Porto Alvaro Perreira amethibitisha jana usiku kuwa:
"Andre Villas Boas ameenda Chelsea Abramovich amemchakua.Inabidi tumshukuru Andre kwa kufanya kila linalowezekana kutupa ushindi na kuleta makombe."
Villas-Boas ambaye alianza kupata uzoefu wa ukocha akiwa chini ya Sir Bobby Robson na Jose Mourinho na alichukua majukumu ya ukocha wa Porto last summer.
Ameiongoza Porto kushinda makombe manne ndani ya msimu mmoja ikiwemo kombe la EUROPA League,Ligi kuu ya Ureno, Portuguese"s Cup and Super Cup.
Mcolombia Falcao, ambaye anamebakiza miaka miwili katika mkataba wake alikuwa ni moja ya wachezzaji waliotoa mchango mkubwa katika kufanikisha mafanikio ya Porto.
Alifunga mabao 17 in Europe Cup, likiwemo goli alililofunga dhidi ya Braga katika fainali .
Claudio Mossi, wakala wa Falcao, jana amenukuliwa akisema: "Kama Villas-Boas ni kocha mpya wa Chelsea basi ni dhahiri kwa wachezaji walio karibu nae watamfuata."
No comments:
Post a Comment