Search This Blog

Tuesday, June 21, 2011

Goal line Technology (Teknolojia ya mstari wa goli)





Jinsi ilivyoanza
1999 Ligi ya Uingereza iliomba kuweka camera katika miamba ya goli kwa ajili ya fainali ya kombe la ligi – FIFA ikakataa
2006 Bodi ya kimataifa ya vyama vya soka iliruhusu kampuni ya Adidas na Cairos kuanza kufanya majaribio ya kuweka kitunza kumbukumbu kidogo ndani ya mipira.Mipira hiyo ikijulikana kama “Smartball” kwa Kiswahili mpira wenye akili.
2007 Mpira wa Smartball ulifanyiwa majaribio katika kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17 huko Peru.JAribio halikufanikiwa – Wakati huo huo Ligi ya Uingereza ilitoa ruhusa kwa kampuni ya Hawk Eye kutengeneza teknolojia mpya.
2008 FIFA ikishirikiana na chama ch soka cha nchi za Wales na Ireland zilipiga kura kukataa matumizi ya teknolojia ya aina yoyote ile katika kutambua magoli.Bdala yake ilikubali wazo la Rais wa shirikisho la vyama vya soka vya Ulaya Michel Platini la kuweka waamuzi wawili wa ziada nyuma ya kila goli.
2009 Mkono wa Thierry Henry ulioinyima nchi ya Ireland nafasi ya kushiriki kombe la dunia ulimfanya Sepp Blatter kuibua tena mjadala wa matumizi ya teknolojia ya kutambua magoli.
2010 FIFA ikishirikiana na chama cha soka cha Wales na Ayalandi ya kaskazini vilipiga kura kupinga matumizi ya teknolojia za ziada katika mechi za soka.Katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke alitamka kuwa huu ndio mwiso wa matumizi ya teknolojia ya ziada ya aina yoyote katika soka.
Machaguo matano tofauti
1 Hawk Eye
Teknolojia hii tayari inatumika katika michezo ya kriketi na Tennis na inawezekana kutumika kirahisi katika soka.Teknolojia hii inatumika kama ifuatavyo:
• Kamera nne zinawekwa juu kabisa ya eneo la penati na mbili nyuma ya goli
• Kamera hizi zinatengeneza picha kamili ambayo ina uwezo wa kuonesha mpira umenagukia sehemu gani katika goli.
• Majaribio yanaonesha kuwa matokeo ya picha hizi yanaweza kutumwa kwa refa ndani ya nusu sekunde katika mechi.

2 Smartball
• Mpira utumikao unakuwa na kijitufe (sensor) kinachotunza kumbukumbu kwa njia ya umeme.
• Nyanya nyembaba zenye mawimbi ya sumaku zinawekwa chini ya uwanja katika eneo la goli.
• Pindi mpira ukikaribia eneo la goli kijitufe katika mpira kinapima mahala mpira ulipo kutokana na mawimbi yaliyoko chini ya uwanja katika eneo la goli.
• Kijitufe katika mpira kinatuma zile kumbukumbu katika kompyuta kwa kutumia antenna iliyoko nje ya uwanja karibu na goli.
• Kompyuta inatuma ujumbe katika saa ya refa uwanjani iksiema kama ni goli ama la.

3 Marudio ya video
Matumizi rahisi tu ya kuangalia marudio katika video.Hi ingeweza kutambua kirahisi sana lile goli la Lampard dhidi ya Ujerumani.Lakini haitosaidia iwapo kama golikipa ataanguka juu ya mpira na kuufanya usionekane na kamera za televisheni.

4 Kamera
Kamera inayowekwa ndani ya goli inaweza kumonesha refa kama mpira umeingia ama la.

5 Waamuzi wa ziada
Waamuzi wawili wa ziada wanaongezwa ambao kazi yao pekee itakuwa ni kuangalia mstari wa goli.Hii itaondoa presha kwa refa na vibendera ambao mara nyingi huwapo mbali na mstari wa goli.

Teknolojia ya Hawk Eye iko poa
Mtaalamu aliyebuni teknolojia ya Hawk Eye anasema kuwa teknolojia hiyo inafanya kazi kwa ufanisi wa asilimia 100 na ina gharama ndogo sana kiasi kwamba yeye mwenyewe anauwezo wa kufunga mtambo huo kwa viwanja vyote bure! Anaendelea kusema kwamba gharama itumikayo katika matangazo na wadhamini itajitosheleza kabisa kwa kufunga na kuendesha mtambo huo.
Paul Hawkins ambaye ndio mmilkiwa kampuni ya Hawk Eye anasema kuwa gharama ya kufunga mtambo huo ni takriban pesa madafu milioni 250 hadi milioni 500 kwa kila kiwanja lakini yeye anaweza kufunga mitambo hiyo bure kama atapewa haki za matangazo na udhamini.Kwa hivyo kama FIFA inahofia gharama hiyo itakuwa si tatizo la wao kuhofia.

Marefa wakubali kuwa wanahitaji msaada
Waamuzi wanaafiki kuwa wanahitaji msaada sababu haiwezekani kwa wao kuona magoli yote kwa mfano kama lile la Frank lampard katika kombe la dunia mwaka huu.Muamuzi wa kiswisi aliyestaafu Urs Meier alikataa bao la Sol Campbell mwaka 2004 wakati Uingereza ilipochapwa na Ureno.Muamuzi huyu anakubali kuwa marefa wote wanahitaji usaidizi wa teknolojia ila hawawezi kusema tu.Anasema muamuzi analazimika kutoa uamuzi wa kuotea tu kwa bao kama la lampard.

No comments:

Post a Comment