Search This Blog

Wednesday, December 19, 2012

MANCHESTER UNITED NA SAKATA LA KUBEBWA



MIMI  AMBAYE NI MDAU WA  SPORTS EXTRA  NAPENDA  KUONGELEA  KAWAIDA  ILIYOPO  KWA  MASHABIKI  WENGI  WASIOIPENDA  UNITED  AMBAO MARA NYNGI WAMEKUWA WAKISEMA  INABEBWA,  KWA  UJUMLA  SUALA  HILI  MARA  NYINGI  HUA  NALICHUKULIA  KISHABIKI  JAPO  KUWA  HUWA  NAONA  WAO WAPO  SERIOUS.
LAKINI  KUBWA ZAIDI  WATANGAZAJI  NAO  WAMEKUA  WAKIWAUNGA  MKONO  MASHABIKI  HAO NA  HASA  WATANGAZAJI  WA  SPORTS  EXTRA  HUWA  NAWASIKIA  MARA  KWA  MARA PAMOJA NA KATIKA  SPORTS  BAR (Labda pia ni kwasababu ndio kipindi cha michezo cha redio na TV ambacho huwa nasikiliza hivyo sijui redio na TV zingine kama nao hua wanaiponda man united).
SASA HILI  LA  WATANGAZAJI  NDIO  LIMENIFANYA  NIANDIKE  WARAKA  HUU  SABABU  NYIE  NDIO  TUNAWATEGEMEA  ZAIDI  KUTUPA  ELIMU/TAARIFA  ZA  KIMICHEZO  NA  BURUDANI  KWA USAHIHI.
NILITEGEMEA  MNGEENDELEA  KUWA  TETRACICLINE  HATA  KATIKA  ANGA  ZA  KIMATAIFA  KAMA  ILIVYO  HAPA BONGO,  JAPO  KUNA  BAADHI  YA  MASHABIKI  WA  HAPA  BONGO  UPANDE  WA  MSIMBAZI  WANAWASAKAMA NYIE  HASA  SHAFII  KWAMBA  ANAFAGILIA  JANGWANI,  HAPO NAWEZA  KUWASHANGAA HAWA  MASHABIKI  KWA   KUSAHAU  KUWA  KUNA  WAKATI  HUKOHUKO  JANGWANI  SHAFII  ALISHAZUSHIWA  KUWA  ANATUMA E-MAIL  KWA  MAXIMO  ILI  MAXIMO  ASIJE  YANGA. KWAKWELI KWA HAPA BONGO NAWASIFU KWA KUWABANA WABABAISHAJI WA MPIRA  WA  BONGO  MKO  JUU NA  HAMUONYESHI  MAHABA  KWA  UPANDE  WOWOTE.
TUKIRUDI KWENYE  MADA  KUU   UNITED  KUBEBWA  NDANI  YA  EPL    
HIVI  SASA  IMEKUWA  NI  KAWAIDA  KILA  MAN UNITED  ANAPOPATA  FAIDA  KWA  MAKOSA  YA  REFA  INAONEKENA  MAN  U  KABEBWA  NA  SIO  KOSA  LA  MWAMUZI  LAKINI  MWAMUZI  HUYOHUYO  ANAPOIUMIZA  MAN  U  INAKUA  NI  KOSA  LA  MWAMUZI  NA  SIO  KWAMBA  MPINZANI  AMEBEBWA  SASA  NASHINDWA  KUELEWA  HII  TERMINOLOGY  YA  KUBEBWA  TAFSIRI  YAKE  NI  NINI?.
KUNA  MIFANO  MINGI  AMBAYO  INAONYESHA  NAMNA  AMBAVYO  UNITED  IMEKANDAMIZWA  NA  WAAMUZI  NA  MIFANO  MINGI  AMBAYO  TIMU  ZINGINE  ZIMEFAIDI  DHIDI  YA  UNITED  NA  PIA  DHIDI  YA  TIMU  ZINGINE;
1.     KOLO TOURE  ALISHAWAHI  KUDAKA  SHUTI  LA  ROONEY  NDANI  YA  MITA  6 WAKATI  KIPA  ALISHAPOTEA  NA  REFA  HAKUONA  TUKIO  HILO  UNITED  WAKAPEWA  KONA  BADALA  YA PENALT- hakuna  aliyeshika  bango
2.     FLETCHER AKIWA KTK KIWANGO BORA  ALIIKOSA  FAINALI  YA  BARCELONA  MWAKA 2009  BAADA  YA  KUPEWA  KADI  NYEKUNDU  ISIYO  SAHIHI NA PENALTI  IKAPIGWA  KTK  NUSU  FAINALI- hakuna  aliyeshika  bango
3.     DROGBA  ALISHAFUNGA  MAGOLI  YA OFF SIDE  MFANO DHIDI  YA  MAN CITY  NA  PIA DHIDI YA  MAN  UNITED  MWAKA 2009 NA  CHELSEA  WAKACHUKUA  UBINGWA  KWA POINT  MOJA  JUU YA UNITED.  hakuna  aliyeshika  bango
4.     DEMBA BA WA NEWCASTTLE  ALIZAWADIWA PENALT 28/11/2011 WAKATI  RIO  RERDINAND  HAKUCHEZA  FAULO.  hakuna  aliyeshika  bango
5.     JUZI 9/12/2012 GOLI  LA  ASHLEY YOUNG  LIMEKATALIWA  DHIDI  YA MAN CITY.  kuna  mashabiki  mpaka  leo  wanasema  Young  alikua  offside.   ILA HILI  CLOUDS  WALIZUNGUMZIA  NA  HATA  SHAFII  AME-POST  KTK  BLOG  YAKE  KUONYESHA  KUWA  YOUNG  HAKUWA  OFFSIDE  ILA  ALICHOMOZA  WAKATI  WA  KUICHEZA  RE-BOUND AMBAPO  HAPO  HAKUNA  OFFSIDE
6.     JUZI  9/12/2012  PIA  EVRA  ALINYIMWA  PENALT  KWA  FAULO  YA  KOLO  TOURE  NDANI  YA MITA  18.  hakuna  aliyeshika  bango
7.     SANT CARZOLA ALIPATA PENALT ISIYO SAHIHI DHIDI YA WEST BROM  MPAKA  KOCHA  WAKE  KAOMBA  MSAMAHA.  Angalau Wenger kaonyesha uanamichezo
8.     MATERSAKA  ALISHIKA  MPIRA  NDANI  YA  MITA 18  LAKINI  WEST BROM  HAWAKUPEWA  PENALT  WAKATI  ARSENAL  WALIPATA  PENALT  MBILI  KATIKA  MECHI  HIYO.  hakuna  aliyeshika  bango

KUTOKANA  NA  MIFANO  HIYO  MICHACHE  SIJAWAHI  KUSIKIA  MASHABIKI  AU  WATANGAZAJI  WAKISEMA  ARSENAL  AU  CHELSEA  AU  MAN CITY  KABEBWA  AU KUSIKIA  KUWA  DROGBA NI  MUOTEAJI, ILA  UTASIKIA  ‘’MAKOSA  YA  REFA’’  ‘’REFA NAE  BINADAMU’’  AU  PRESHA  ILIKUA  KUBWA  HIVYO  REFA HAKUONA.  LAKINI  KWA UNITED SABABU HUWA  SIO  PRESHA, NA  HAPO  INASAHAULIKA KABISA  KUWA  KARIBU  MECHI  ZOTE  ZA  UNITED  HUWA  PRESHA  YA  MCHEZO  IKO  JUU.

KWA  MTAZAMO WANGU;
 UNITED  INACHUKIWA  NA  WENGI  SABABU  YA  MAFANIKIO  YAKE.  NDIO  MAANA  HATA IKIFANYA  VIZURI  WATU WANATAFUTA WAPI PA KUSHIKA KAMA WAFA MAJI, KUNA KIPINDI KIKOSI  KILIKUA KINATISHA SANA  KILIKUA  KINAPIGA GOLI NYINGI KILA MPINZANI  PALE ENGLAND  BASI  WAPINZANI  UTETEZI  WAO  IKAWA  ‘’UNAMKUMBUKA  REDONDO?’’  ‘’UNAMKUMBUKA  KAKA?’’,  ‘’KIBOKO  YENU  MADRID’’  BADALA YA KUONGELEA  TIMU ZAO.  KWASASA  TIMU  INASHINDA  JAPO  HAITISHI  SANA,  SASA WANASEMA ‘’INABEBWA’’. KIFUPI  HAWAKUBALI  UKWELI  SUALA  AMBALO  SIO  UANAMICHEZO.  MCHEZAJI  AKIWA  UNITED  SIO MZURI  AKITOKA  ANAKUA  MZURI  KWA  KIWANGO KILEKILE  MFANO  MZURI NI  RONALDO  NA SASA  VAN  PERSE  ONA HATA  KWASASA  YALE  MAJINA HATUYASIKII  TENA  ‘’VAN MAGOLI’’  ‘’VAN   HAKUNAGA’’  YAMEISHIA WAPI NA KIDUME BADO ANATUPIA!  KAZIPIGA TIMU  KUBWA ZOTE MPAKA SASA.
KAKA  SHAFII  ALIKUWA NI MTU AMBAYE  ANAMFAGILIA  SANA  RVP  NA  KUMPAMBA KWA MAJINA  HAYO LAKINI  KWA SASA  KAHAMIA  KWA  FALCAO.
SIJUI  ITAKUAJE  PALE  RVP  ATAKAPOKUJA  KUWA  KAMA  TORRES  ALIVYO  SASA 
AU  SIJUI  ITAKUA  VIPI  IKITOKEA  GHAFLA  JANUARY  FALCAO  AKATUA  MAN UNITED.

UNITED INA MASHABIKI WENGI LAKINI PIA INA WAPINZANI WENGI;
SABABU WALE  WOTE  AMBAO  HUWA INAPAMBANA  NAO NA BAADAE  WAKAKATA  PUMZI WENGI WAO HUANGUKIA  KWA WAPINZANI WENGINE, MFANO MZURI  TANGU 1992 NDANI YA PREMIER LEAGUE UNITED IMEBADILI WAPINZANI WENGI. BINAFSI  NIMEANZA  KUFUATILIA KIDOGO LIGI HII MWAKA 1996 NA NIKAWA ZAIDI MWAKA 1998 MPAKA SASA.
HIVYO  KUMBUKA  KUWA  TANGU 1992 WALIKUWEPO  LIVERPOOL,  LEEDS UNITED (Kina Tonny Yeboah), BLACKBURN ROVERSE (Kina Allan Wright na Allan Shearer kabla hajaingia Newcastle mwaka 1996 kwa £15 million) , NEWCASTLE UNITED (Kina Les Ferdinand na Faustin Asprilla)  WAKAJA ARSENAL   WAKAJA CHELSEA (miaka ya 2000 baada ya kuja Abramovich) WAKAJA MAN CITY (baada ya sheikh Mansoor)
HAWA NINAOSEMA  WALIKUJA  SINA MAANA KUWA  HAWAKUWEPO  AU KWAMBA  NAWADHARAU  ILA  NI KWAMBA  WALIKUA KAMA  ASTON VILLA WASASA (yaani walikua wa kawaida tu). HII  NI DHAHIRI KUWA WALE WALIOKUA  LEEDS, NEWCASTLE NA BLACK BURN+ WALE WASIOZIJUA HIZO TIMU KAMA LEEDS  NDIO  SASA  WAKO  KWA  MAN  CITY  NA CHELSEA. NA  PIA  WAKIKIMBIA  LIVERPOOL  NA  ARSENAL  WENGI  WANAENDA HUKO(CITY NA CHELSEA).  HIVYO CHUKULIA  HAO  TU WALIOKUA TIMU  HIZO SABA WAWE DHIDI YA  UNITED  INAKUAJE  HAPO  HALI  YA  HEWA  LAZIMA  ICHAFUKE,  ACHILIA  MBALI  TIMU  ZINGINE  ZOTE  ZINAZOSHIRIKI  LIGI  KUU.

SABABU  YA  KUSEMA  TIMU HIZI  ZINAIKIMBIZA  UNITED  NI  KUWA  TANGU  1992  UNITED  INABADILISHA  WAPINZANI  WA  MBIO  ZA  UBINGWA  SABABU  IMEKUA  AKIKOSA  UBINGWA ANAKUA  WAPILI  ISIPOKUWA  MISIMU  MITATU TU (2001/2002, 2003/2004 NA 2004/2005 TU) INAMAANA HII MISIMU MITATU NDIO  ALIFANYA  VIBAYA  ZAIDI  NA  HAPA  TATIZO  KUBWA  ILIKUA  PENGO  LA  PETER  SCHMEICHEL KABLA YA KUPATA KIPA MWINGINE  MZURI,  JE  HII INAWEZEKANA  KWA  KUBEBWA  TU!?.  HAO  WABEBAJI  HAWACHOKI  KATIKA  MIAKA  YOTE  HIYO?.
 WAKATI HAWA WENYE UWEZO KAMA  LIVERPOOL  AMESHAWAHI  KUWA  WA  8 MWAKA 1993/94 NA  ARSENAL  AMESHAWAHI KUWA WA 12 MWAKA 1992  SIKUAMBII KUHUSU  CHELSEA  NA  MAN CITY.

MSAADA

IKIWEZEKANA  TUSAIDIANE  ILI  KAMA NI KWELI  TUWEZE  KUJUA   UNITED   ANATOA  NINI  ILI  KUBEBWA  AMBACHO  KINAWASHINDA   MAN  CITY, CHELSEA  AU QUEENS PARK RANGERS KUTOA  ILI  NAO WABEBWE!?

UNITED  NDANI  YA  CHAMPIONS  LEAGUE

UNITED HUYU  ANAYEBEBWA  KWENYE EPL  VIPI  KWENYE  CHAMPIONS  LEAGUE MBONA  NI BINGWA  MARA  3  NA KACHEZA  FAINALI  NYINGI TU NA ALISHAKUA BINGWA WA VILABU DUNIANI.  VIPI  HAWA  WENYE  UWEZO  WA MPIRA KAMA  ARSENAL, MAN CITY  MBONA  HATA  KOMBE HAWAJAWAHI  KUBEBA,  NA  CHAMPIONS  LEAGUE  INACHEZESHWA  NA  MAREFA  WENGI  WA  KIWANGO  CHA  JUU  WASIOTOKA  UINGEREZA KWENYE MAREFA WACHOVU KAMA WAO WASEMAVYO?.


NAOMBA  MUELEWE  KUWA  MPINZANI WA  UNITED  HAWEZI  KUISIFU  UNITED
·       HATA  MOURINHO  ALIPOKUA  CHELSEA ALIKUWA  ANAMPONDA  RONALDO  NA KUMUITA  MSHENZI  HANA  ELIMU, LAKINI  KWASASA  NDIE  ANAYEMPA  UHAKIKA  WA  KULA  FEDHA  ZA PALE SANTIAGO BERNABEU  (sio siri ndio jembe lake) NA UTAMWAMBIA  NINI KUHUSU  RONALDO.


MTANGAZAJI  ANAYEONGOZA  KWA  KULIPEPERUSHA  NENO  MBELEKO  KWA  UNITED 
NI  ALEX  LUAMBANO  SABABU  HATA  IKISHINDA  BILA  REFA  KUIPA  FAIDA  YEYE  ATAULIZA  MBELEKO  VIPI.  MFANO  KUNA  SIKU  ALIKUA  YEYE  NA  JEFF REDIONI  UNITED  ILIKUA  IMEPATA  MATOKEO  MAZURI  KTK  MECHI  KUBWA  AMBAYO SIKUMBUKI VIZURI  ILIKUA  KAMA  SIO  DHIDI  YA  ARSENAL  BASI  NI  LIVERPOOL  AU  CHELSEA  NDANI  YA  MSIMU  HUU.  JEFF  AKAWA  ANASEMA  UNITED  WANGETULIA  WANGEPATA  MAGOLI  MENGI  LAKINI  LUAMBANO   AKAWA  ANACHOMEKEA  MANENO  YANAYOMAANISHA  MBELEKO  ILIISHIA  HAPO  NDIO  MAANA  HAWAKUFUNGA  ZAIDI.
VITU  KAMA  HIVI  SIDHANI  KAMA  NI  SAHIHI  KWA NYIE  WATANGAZAJI  KUVIONGEA  HEWANI  SABABU  NI  DALILI  YA  KUONYESHA  MAHABA  YENU  KWA  HIZI  TIMU  HALI  YA  KUWA  MNATAKIWA  KUWA  NEUTRAL  PINDI  MUWAPO  HEWANI.

HAIWEZI  KUWA  RAHISI  KUWABADILI  MASHABIKI WOTE  HUKU  MTAANI  SABABU  WAKO  HURU  KUONGEA  CHOCHOTE  JAPO  WENGINE  HATA  HIZO  MECHI  HUA  HAWAANGALII  ILA  WANAONGEA  TU.

USHAURI  WANGU
·      NI  KAMA  NI  LAZIMA NENO KUBEBWA  LITUMIKE HEWANI  BASI  LITUMIKE  KWA  USAWA  PALE  MWAMUZI  ATAKAPOIPA  FAIDA  TIMU  YOYOTE BASI IWE  HIVYO  KUWA  TIMU  ILE  IMEBEBWA  NA  SIO  NENO  HILO  KUAMBATANISHWA  NA  UNITED  TU HIYO  ITAKUA SIO  FAIR.
·      WATANGAZAJI  MUWAPO  HEWANI  HAMTAKIWI  KUONYESHA  MAPENZI  YENU  KTK  TIMU YOYOTE. NA HATA UKIONYESHA KUIPONDA SANA  TIMU  FULANI WAKATI  INAFANYA VIBAYA  KUWA  TAYARI  KUISIFIA SANA  INAPOFANYA  VIZURI  KINYUME NA  HAPO  ITAKUA  NI KAMA  WEWE  UNAOMBEA IWE INAFANYA  VIBAYA  TU  ILI  UPATE CHA  KUONGEA (Yaani usiwe na uchambuzi wa kina ktk mabaya tu wakati yanapokuja mazuri ya timu hiyo unaona ni kitu cha kawaida tu, na ku-act kuwa hauko deep kwenye mambo mazuri ya timu hiyo ‘’that is not fair’’) FAIR PLAY SIO KTK PITCH PEKEE NI HATA HUKU KWENYE HABARI.    
·      NA  KUWA TUJARIBU  KUUPA  SUPPORT  MSEMO  WA  JEFF  KUWA  TUNATAKIWA  KUWAPA  HESHIMA  ZAO  WAPINZANI  PALE  WANAPOPATA  USHINDI  KWA  JUHUDI  ZAO. NA NDIO  MAANA VYAMA VYA MICHEZO  HUMWAJIBISHA MWAMUZI PALE  ANAPOCHEMSHA NA SIO TIMU ILIYOPATA FAIDA KUTOKANA NA MAKOSA YA MUAMUZI.

NINA UHAKIKA KUWA HAYA YOTE NYIE WATANGAZAJI MNAYAFAHAMU ILA HII NI KUKUMBUSHANA TU NA KUCHANGIA MAWAZO ILI HATA WASIKILIZAJI WENGINE WAWEZE KUPATA KILE WASICHOFAHAMU.  
PIA MIMI KWA UJUMLA NAOMBA MUENDELEE KUTUPATIA HABARI SAHIHI KAMA MFANYAVYO SASA. SABABU MAMBO MENGI HUWA TUNAANZA KUYASIKIA KWENU NA BAADA YA MUDA TUNAYASHUHUDIA DHAHIRI.
HUO NI UTHIBITISHO KUWA CLOUDS NI CHOMBO AMBACHO KINA WAANDISHI MAKINI NA WATANGAZAJI BORA HAPA TANZANIA KUTOKANA NA KUA NA HABARI ZA UHAKIKA KILA WAKATI.

KWA LEO NI HAYO TU.
NATANGULIZA SHUKURANI ZANGU KWENU.
MDAU-SPORTS EXTRA






SUALA LA ZANZIBAR HEROES KUFUNGIWA KUJADILIWA NA KAMATI YA NIDHAMU - MTIBWA YATINGA NUSU FAINALI YA UHAI CUP

SUALA LA AKINA MORRIS, CANNAVARO KWENDA KAMATI YA NIDHAMU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) ikieleza kuwafungia wachezaji kadhaa Wazanzibari wanaochezea klabu mbalimbali za timu za Tanzania Bara na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).

Suala hilo limepelekwa kwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF kwa hatua zaidi, hivyo kwa sasa Shirikisho litasubiri uamuzi wa kamati hiyo. Baadhi ya wachezaji hao ni nahodha msaidizi wa Taifa Stars, Aggrey Morris, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nassoro Masoud Cholo, Mcha Khamis, Seif Abdallah na Selemani Kassim Selembe.

MTIBWA YAINGIA NUSU FAINALI KOMBE LA UHAI
Mtibwa Sugar imekata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) kuzamisha African Lyon mabao 3-1.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam,  hadi mapumziko Mtibwa Sugar ilikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 22 na Hillary Kasela. Hassan Kabunda aliisawazishia African Lyon katika dakika ya 53.

Mabao mengine ya washindi yalifungwa na Godfrey Mohamed dakika ya 64 na Juma Lazio akapachika la mwisho dakika ya 87. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar sasa itacheza mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Azam ambayo nayo leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) iliilaza JKT Ruvu bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Chamazi. Bao la Azam lilifungwa dakika ya 46 na Mudathiri Yahya.

Mechi hiyo ya kwanza ya nusu fainali itachezwa Ijumaa (Desemba 21 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Nusu fainali ya pili nayo itachezwa kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 10 kamili jioni.

Robo fainali ya tatu kati ya Oljoro JKT na Simba, na robo fainali ya nne zinachezwa leo saa 10 kamili jioni (Desemba 19 mwaka huu) kwenye viwanja vya Karume na Chamazi, Dar es Salaam.

Mechi ya fainali na ile ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

BREAKING NEWS: KOCHA WA BARCELONA TITO VILANOVA AUGUA GHAFLA NA KUACHA KAZI - BARCA WATAFUTA MBADALA


Stepping down: Barcelona coach Tito Vilanova has suffered a relapse of a tumor he had removed last November Kocha wa Barcelona Tito Vilanova anajiandaa kuachia ngazi kutoka kwenye nafasi yake ya ukocha wa Barca baada ya kurudia kuugua ugonjwa uliokuwa unamsumbua wa tezi kwenye mdomo ambalo alifanyiwa upasuaji mwaka uliopita.

Kocha huyo mwenye miaka 44 alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe/tezi hilo mwezi November 2011 wakati alipokuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo.

Alichukua majukumu ya kuwa kocha mkuu wa Barcelona baada ya Pep Guardiola kuachia ngazi na Vilanova akasaini mkataba wa miaka miwili.

Barcelona wametangaza kusitisha shamra shamra za sikukuu ya Krismas huku wakiwa kwenye mchakato wa kumtafuta mbadala wa Tito

RECORD ZA VILANOVA AKIWA NA BARCELONA MPAKA SASA

Pld 27 W 23 D 2 L 2 (85.18% win ratio)
Successor: Vilanova replaced Pep Guardiola (right) as Barcelona manager in the summer

KOCHA WA STARS: NIPO TAYARI KUPOTEZA KAZI KWA KUTOWACHEZESHA WATOVU WA NIDHAMU SAMATTA NA ULIMWENGU

KOCHA wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema yuko tayari kutimuliwa kazi iwapo tu msimamo wake wa kutetea nidhamu kwa wachezaji kwenye kikosi chake utakuwa kikwazo kwa wengine.
Poulsen alisema hayo wakati akizungumzia kitendo cha Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu kuchelewa kujiunga Stars kujiandaa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zambia mwishoni mwa wiki hii.

Ulimwengu na Samata wanaocheza soka la kulipwa na timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameitwa kuja kuivaa Chipolopolo.
Poulsen alisema hana muda wa kuwabembeleza wachezaji hao, na kama ni lazima afanye hivyo ili wacheze, basi yuko tayari kuachia ngazi.
“Nasisitiza nidhamu. Timu ya Taifa siyo kitu cha mchezo.

Mchezaji hapaswi kubembelezwa kucheza timu ya taifa, yeye mwenyewe ndiye wa kufanya juhudi kwa taifa lake,” alisema Poulsen.
“Kama wanadhani ipo sababu ya mimi kuwabembeleza ndipo wacheze, ni heri nikatishe mkataba wangu kuliko kufundisha wachezaji waliokosa nidhamu,” alisema wakati akiongea na Mwananchi.


“Sina tena sababu ya kuwachezesha, siko tayari kuona wachache wanavunja nidhamu ya timu, mchezo wa soka ni pamoja na nidhamu, siyo kipaji tu.”
Kauli ya Poulsen imekuja baada ya kuulizwa kama haoni atakuwa anahatarisha kibarua chake kwa kuwaacha nyota hao, hasa ukizingatia makocha watangulizi wake walitimuliwa kwa sababu ya nidhamu mbaya ya wachezaji.


Alisema: “Moja ya falsafa yangu kama kocha mwenye taaluma ni kusimamia nidhamu ya timu. Siwezi kulea watovu wa nidhamu kwa sababu tu ya kulinda kibarua changu.
“Wachezaji wanajifunza kila siku, kuna mema na mabaya.
Kuwaruhusu Samata na Ulimwengu kuwafundisha wengine utovu wa nidhamu kwa sababu wao wanajua soka, wanacheza nje ya nchi na kupendwa na mashabiki, maana yake ni kuivuruga timu. Siko tayari.”


Aliongeza: “Uamuzi wao wa kukaa nyumbani bila kutoa taarifa, ni dharau kwa taifa lao, wachezaji wenzao, mashabiki na pia wamenidharau mimi na benchi langu lote.”
Kocha Marcio Maximo, alitanguliwa na wakati mgumu kutoka kwa mashabiki kabla ya kuondoka, kufuatia uamuzi wake wa kutowachezesha kwenye kikosi, Haruna Moshi, Athumani Idd na Juma Kaseja, huku Jan Poulsen naye akiingia matatani baada ya kumtema Samata kwa madai ya kutojituma.


Source: Mwananchi

MADA MAUGO NA MATUMLA WAJIANDAA KUFANYA MAANGAMIZI KWA WAPINZANI WAO



Kocha wa ngumi Pascal Mhagama kushoto anaemfua bondia Mbwana Matumla kwa ajili ya mpambano wake na David Chalanga wa kenya mpambano utakaochezwa Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mbwana Matumla kushoto akionesha ufundi wa kutupa masumbwi mbele ya kocha wake Pascal Mhagama kwa ajili ya mpambano wake na David Chalanga wa kenya mpambano utakaochezwa Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mada MAUGO AKILUKA KAMBA KWA AJILI YA MAANDALIZI YA MPAMBANO WAKE NAbondia Yiga Juma wa Uganda mpambano utakaofanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es salaam picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi Said Chaku kushoto akimwelekeza bondia Mada Maugo jinsi ya kutupa Ngumi wakati wa mazoezi yake ya mwisho kwa ajili ya kumkabili bondia Yiga Juma wa Uganda mpambano utakaofanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mada Maugo kushoto akionesha umaili wa kutupa makonde na kocha wake Said Chaku wakati wa mazoezi yake ya mwisho kabla ya kupambana na bondia Yiga Juma wa Uganda Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

PRIMETIME PROMOTIONS YATOA MILLION 105 KUFANIKISHA SHAMRA SHAMRA ZA MKUTANO MKUU WA YANGA

Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi millioni 105 kwa uongozi wa timu ya Yanga kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wao mkuu pamoja na mechi ya kirafiki ya kimataifa katika kukamilisha shamrashamra za kusindikiza mkutano huo wa kwanza wa uwazi wa kihistoria kwa Club ya Yanga. 
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga na Makamu Mwenyekiti wa Club ya Yanga,Clement Sanga wakikabidhiana mikataba yao ya makubaliano ya kikazi.
 Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akitiliana saini ya makubaliano na club ya Yanga kuhusiana na makubaliano ya timu ya Yanga  kusaini mkataba wa maelewano na kampuni ya Primetime Promotions Ltd,ambapo Prime Time Promotions imekubali majukumu ya matayarisho yote ya mkutano wa wanachama wote wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 19 2013.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akifurahia jambo na baadhi ya Wanahabari mara baada ya kutiliana saini mikataba yao ya kikazi na Club ya Yanga,uliofanyika mapema leo kwenye makao makuu ya ofisi za club hiyo,Jangwani jijiini Dar
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akizungumza machache kuhusiana na makubaliano yao ya kikazi na Club ya Yanga ikiwemo sambamba na makabidhiano ya mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 105 yaliyotolewa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd.
Pichani kati ni Makamu Mwenyekiti wa Club ya Yanga,Clement Sanga akizungumza mapema leo kwenye makao makuu ya timu hiyo na Waandishi wa habari kuhusiana na timu ya Yanga  kusaini mkataba wa maelewano na kampuni ya Primetime Promotions Lt,ambapo Prime Time Promotions imekubali majukumu ya matayarisho yote ya mkutano wa wanachama wote wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 19 2013.Kushoto ni katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako na kulia ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga.

Aidha katika mkutano huo imeelezwa kuwa matayarisho hayo yatahusisha ukumbi na viambatanisho vyote muhimu,ikiwemo Live TV coverage na matangazo mbalimbali ya kuhamasisha mafanikio ya mkutano.


Aidha katika kuongeza mapato kwa maendeleo ya club na matayarisho ya kumalizia ligi, Prime Time Promotions Ltd,imetoa milioni 105 mapato ya uhakika kwa timu ya Yanga na Prime Time Promotions  itaandaa mechi ya kirafiki ya kimataifa katika kukamilisha shamrashamra za kusindikiza mkutano huo wa kwanza wa uwazi wa kihistoria kwa Club ya Yanga. Habari Picha na Michuzijr Blog.