Search This Blog

Wednesday, December 12, 2012

EXCLUSIVE: MRISHO NGASSA ASAINI YANGA MIAKA MIWILI NA KUPEWA MILLIONI 10 - AHAIDIWA NYINGENE MWISHO WA MSIMU

Huku masaa yakizidi kuyoyoma kuelekea muda ambao msemaji wa klabu ya El Merreikh alioutoa kwa mchezaji Mrisho Ngassa kujitokeza alikojificha na kufanya taratibu za uhamisho wake kwenda Sudan - mapema asubuhi ya leo, kuna taarifa za ndani kabisa kwamba mchezaji huyo ameamua rasmi kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya mitaa ya jangwani.

Chanzo cha habari kilicho karibu na mchezaji husika na klabu ya Yanga ni kwamba Mrisho Ngassa tayari amekubaliana kimsingi na Yanga kwamba atajiunga na klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo uliobakisha miezi isiyopungua sita  na klabu ya Simba kwa malipo mazuri kama ambavyo imekuwa kwa mchezaji Haruna Niyonzima.

"Ni kweli Ngassa tayari ameshakuwa na pre-contract na Yanga ya miaka miwili, kwa sasa hivi amepewa millioni 10 na fedha nyingine atapewa mara atakapomaliza mkataba wake na Simba mwishoni mwa msimu. Sasa hivi mchezaji amejificha ili kuepeuka usumbufu wa El Merreikh na Simba pamoja na Azam."

Mrisho Ngassa amekuwa katika vichwa vya habari kwa takribani wiki mbili sasa juu ya usajili wake wa kwenda kujiunga na El Merreikh ambao wamemuahidi mshahara wa $4000 kwa mwezi pamoja na $75000 kama ada ya usajili, huku vilabu vyake vya Simba na Azam FC vikilipwa $100,000. 

Tuesday, December 11, 2012

EL MERREIKH YATOA TAMKO DHIDI YA KUPOTEA KWA NGASSA - ASIPOPATIKANA MPAKA KESHO DILI LIMEKUFA

Songombingo la kupotea kwa mchezaji Mrisho Ngassa bila taarifa yoyote kwa vilabu vyake vya Simba na Azam FC, na klabu inayomtaka kumsajili ya El Merreikh ya Sudan limechukua sura mpya jioni hii baada ya msemaji wa klabu ya El Merreikh kuzungumza na kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM.

Akizungumza na Shaffih Dauda, shekhe Idrissa amesema kwamba El Merreikh imeshakubalina kimsingi na vilabu vya Azam FC na Simba SC na mchezaji na kilichokuwa kimebakiwa na kutia saini kwa mikataba pamoja na kufanya vipimo vya afya ili mchezaji huyo aweze kujiunga na timu hiyo tajiri ya Sudan, lakini muda mfupi baada ya kufika Dar es Salaam mchezaji huyo amekuwa mafichoni - akiwa hapokei simu na muda mwingine anazima bila kutoa taarifa zozote kwa vilabu husika.

"Mrisho Ngassa tulikuwa tumeshafanya nae mazungumzo vizuri na tukakubaliana na ikabakia kumalizana na vilabu vya Simba na Azam, lakini sasa tukiwa tayari tumemalizana na vilabu mchezaji mwenye amekuwa akifanya vitendo visivyo vya kistaarabu, simu yangu hapokei na muda mwingine anaaizima kabisa. Hili sio jambo zuri kabisa kwake na kwa mpira wa Tanzania kiujumla. Anaharibu sifa ya wachezaji wenzie wa kitanzania, ni vizuri angepokea simu na kutueleza kama dili linawezekana au tofauti, kuliko kutuacha sisi tukipoteza muda kuwepo hapa Tanzania. Kwa tabia hii ya Ngassa tumefikia maamuzi ya kwamba mpaka kesho asubuhi kama mchezaji atakuwa hajapatikana then tutasitisha uhamisho wa mchezaji huyu na kuangalia sehemu nyingine mbali na Tanzania." - Alimaliza Shekhe Idrissa.

Taarifa zilizoenea ni kwamba Ngassa hataki kwenda El Merreikh baada ya kushawishia na viongozi wa Kulwa ili aendelee kuwepo Simba mpaka mkopo wake utakapoisha mwakani na aweze kujiunga na klabu hiyo yake ya zamani.

waliopandi​sha bendera ya taifa mlima Kilimanjar​o wapokelewa na waziri wa maliasili na utalii

Mkurugenzi wa mamlaka ya hifadhi za taifa(TANAP)Allan Kijazi akiazungumza wakati wa hafla fupi ya kuwapokea wapanda mlima zaidi ya 30,waliopanda mlima Kilimanjaro Desemba 6 kwa lengo la kupandisha bendera ya taifa kwa ajili ya sherehe ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
Mwenyekiti wa bodi ya utalii Tanzania(TTB)Balozi Charles Sanga akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwapokea wapanda mlima zaidi ya 30,waliopanda mlima Kilimanjaro Desemba 6 kwa lengo la kupandisha bendera ya taifa kwa ajili ya sherehe ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
Mwenyekiti wa bodi ya Serengeti Breweries Jaji Mark Bomani akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwapokea wapanda mlima zaidi ya 30,waliopanda mlima Kilimanjaro Desemba 6 kwa lengo la kupandisha bendera ya taifa kwa ajili ya sherehe ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
Mkuu wa mkoa wakilimanjaro Leonidas Gama akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwapokea wapanda mlima zaidi ya 30,waliopanda mlima Kilimanjaro Desemba 6 kwa lengo la kupandisha bendera ya taifa kwa ajili ya sherehe ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
Mkurugenzi wa Serengeti Breweries Steven Gannon akipokea cheti kutoka kwa waziri wa maliasili na utalii Balozi Khamisi Kagasheki baada ya kufanikiwa kufika Uhuru peak.
Askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania ,Private Amani Kasanga akipokea cheti kutoka kwa waziri wa maliasili na utalii Balozi Khamisi Kagasheki baada ya kufanikiwa kufika Uhuru peak.
Askari wa jeshi la wananchi wa TAnzania Luteni Kijakazi Marijebu akipokea cheti kutoka kwa waziri wa maliasili na utalii Balozi Khamisi Kagasheki baada ya kufanikiwa kufika Uhuru peak.
Baaadhi ya washiriki wa zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro lililoongozwa na Jenerali mstaafu wa jeshi la wananchi,Jenerali George Waitara.
Mbunge wa jimbo la Kohani Zanzibar Mh Amina,akiwa na washiriki wengine waliopanda mlima Kilimanjaro.Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Moshi. 

BREAKING NEWS: NADIR CANAVARRO, AGRREY MORRIS, MCHA KHAMISI NA WACHEZAJI WENGI WASIMAMISHWA KUICHEZEA ZANZIBAR HEROES KWA MUDA USIOJULIKANA

Chama cha Soka Visiwani Zanzibar, ZFA, kimeivunja rasmi timu ya Taifa ya Zanzibar, 'Zanzibar Heroes' na kuwasimamisha kwa muda usiojulikana wachezaji 16 wa kikosi hicho kucheza soka ndani na nje ya nchi kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Akitangaza maamuzi ya kikao cha kamati tendaji cha ZFA Taifa kilichokaa leo mchana ofisi za Chama hicho zilizopo Kiembe Samaki nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Makamo wa Rais wa ZFA Taifa kwa upande wa Unguja, Alhaj Haji Ameir, amesema wameamua kuchukua maamuzi hayo ambayo kimsingi yameungwa mkono na wajumbe wote wa Kamati tendaji waliohudhuria kikao hicho ili kutoa somo kwa wachezaji wengine.


Kikao hicho cha dharura kimekuja kufuatia sakata la wachezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar, 'Zanzibar Heroes' kuamua kugawana kiasi cha dola 10,000 ambazo ilikuwa ni zawadi baada ya timu hiyo kushika nafasi ya tatu katika michuano ya kombe la chalenji iliyomalizika wiki iliyopita jijini Kampala nchini Uganda, baada ya kuifunga Timu ya Kilimanjaro Stars kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 6-5.


Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai kuwa wamekuwa wakidhulumiwa fedha zao na chama cha soka visiwani Zanzibar.


Hata hivyo katika ufafanuzi uliotolewa leo na Katibu Mkuu wa ZFA Taifa, Kassim Haji Salum amesema haijawahi kutokea wachezaji wa timu hiyo kudhulumiwa haki yao akikumbushia fedha za zawadi walizopata mwaka 1995 katika mashindano kama haya yaliyofanyika nchini Uganda na Zanzibar ikafanikiwa kutwaa ubingwa na mwaka 2009 walishika nafasi ya tatu na mara zote walipewa stahili zao.

Kufuatia maamuzi hayo wadau wa soka visiwani Zanzibar wameunga mkono hatua hiyo kwa kusema itasaidia kurejesha nidhamu katika timu ya taifa, mmoja wa waliotoa maoni yao ni Katibu mwenezi wa klabu ya New Boko, Mohammed Mrope amesema hatua hiyo ya ZFA itakuwa fundisho na kuleta nidhamu kwa wachezaji wa timu wa taifa, "Timu ya taifa ya Zanzibar imekuwa mfano mzuri kwa timu nyengine kwa wachezaji wake kuwa na nidhamu yahali ya juu....sasa hili lililofanyika imekuwa kama timu ya magengeni mimi naunga mkono 100 kwa 100 hatua ya kuivunja timu na kuwasimamisha wachezaji wote waliohusika katika suala hili'. Akisema Mrope.


Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Timu ya Zanzibar Salum Bausi ambaye jana alitangaza rasmi kujiuzulu kuifundisha timu hiyo amesema hatua hiyo ni sahihi kabisa kwa sababu kitendo hicho kimewafedhehesha wadau wa soka na wazanzibari kwa ujumla.


Tayari ZFA Taifa walikwishatuma barua rasmi kwa TFF juu ya hatua hiyo huku nakala ya barua hizo zikitarajiwa kusambazwa kwa vilabu wanavyochezea wachezaji hao.


Wachezaji wanne walionusurika na adhabu hiyo ni wale walioamua kuzirejesha fedha hizo ambao majina yao hayakutajwa kwa sababu maalum, hata hivyo taarifa zilizopo ni kuwa wachezaji hao wanatoka katika klabu ya Kipanga timu inayomilikiwa na JWTZ, Jamhuri, Zimamoto na KMKM.

EXCLUSIVE: MRISHO NGASSA AWAPOTEA SIMBA NA AZAM - AIHISIWA KUTEKWA NA KLABU YAKE YA ZAMANI

Ngassa akisalimiana na Manji
Wakati vilabu vya Simba na Azam vikiwa tayari vimeelewana juu ya haki za mchezaji Mrisho Ngassa ambaye anauzwa kwenda El Merreikh kwa ada ya uhamisho wa $100,000 - mchezaji mwenye amekuwa hapatikani kwenye simu wala haijulikani alipo kitu ambacho kimezusha tetesi nyingi mtaani.

Ngassa ambaye alirejea Tanzania hivi karibuni akitokea nchini Rwanda alipoenda na timu ya Tanzania bara kushiriki michuano ya Kombe la CECAFA Challenge Cup amekuwa hapatikani kwenye simu zake za mkononi na wala kwake hayupo, jambo ambalo limewapa hofu viongozi wa Simba na Azam ambao tayari wameelewana na wanachosubiri ni kumpa taarifa mchezaji husika.

Kutokana na kupotea huko kwa Ngassa bila taarifa zimeibuka tetesi kwamba viongozi wa klabu yake ya zamani ya Yanga wamemteka wakijaribu kumshawishi akatae kujiunga na El Merreikh na arudi jangwani huku wakimuahidi mapato mazuri kama ilivyo kwa Haruna Niyonzima.
  

ANGALIA GOLI LA KWANZA KABISA ALILOFUNGA LEO MESSI AKIWA MDOGO - NA MAELEZO YA KIUNDANI JUU YA REKODI YAKE MPYA

Maelezo ya kiundani zaidi kuhusu rekodi ya Leo Messi aliyoivunja siku ya jumapili dhidi ya Real Betis

 - By scoring a brace at the Benito Villamarín, Leo Messi took his total in 2012 to 86 goals, beating the all-time record in a calendar year set by Gerd Müller (1972).
- In the league, Messi has scored 56 goals in 34 games, while Müller got 42 in 34 games.
- Barani ulaya, Messi amefunga mabao 13 katika mechi 11, wakati Müller alitupia mabao 10 katika mechi 4.

- Kwenye kombe la FA, Messi alifunga mabao 3 katika mechi 7  na Müller alifunga 7 katika mechi 6.

- Mwezi wa tisa ndio ulikuwa mwezi mzuri zaidi kwa Messi alifunga mabao (13), wakati mwezi wa 3 ndio ulikuwa mzuri zaidi kwa Muller baaa ya kufunga mabao (13).

- Messi alifunga mabao 86 katika mechi 66 akiwa na Barça na Argentina. Boomber of the nation alifunga 85 katika mechi 60.

- Mabao 76 ya Messi aliyafunga na mguu wa kushoto, 7 na mguu wa kulia na matatu kwa kichwa. 

- Mabao 74 aliyafunga ndani ya box la penati na 12 aliyafunga nje ya boksi.

- Malaga na Bayer Leverkusen (6) ndizo timu ambazo Messi amezifunga mabao mengi zaidi mpka sasa ndani ya mwakak 2012.

- Iniesta (9), Cesc (6) and Alexis (6) hawa ndio waliompa asissits nyingi katika mabao yake 86.
 
- Mabao yake 23 katika mechi 15 ni mengi zaidi katika mwanzo wa La Liga, akiifikia rekodi iliyokwa na  Cristiano Ronaldo (2011/12).

- Jumapili, Messi alifunga bao lake la kwanza katika uwanja wa  Benito Villamarín, ingawa tayari alishawahi kufunga pale mara moja katika kombe la FA  2010/11.

Monday, December 10, 2012

BREAKING NEWS: AZAM YAIPORA SIMBA TONGE MDOMONI - YATANGAZA BRIAN UMONY AMETUA KWAO LEO


Klabu ya Azam imetangaza kupitia ukurasa wao wa Facebook kwamba mmoja  ya wachezaji waliong'ara katika michuano ya CECAFA Challenge Cup Brian Umony ametua kwenye klabu yao leo jioni.

Umony ambaye tayari alishaanza mazungumzo na Simba akiwa na timu yake ya taifa ya Uganda iliyochukuwa ubingwa wa Challenge mapema mwezi huu, lakini akashindwana nao katika suala la mahitaji yake binafsi.

Hii ndio taarifa Azam FC walioitoa muda mfupi uliopita

WACHEZAJI WA ZANZIBAR HEROES WAPORA MPUNGA WA CECAFA NA KUGAWANA WENYEWE

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar ' Zanzibar Heroes' wameingia katika kashfa nzito baada ya kudaiwa kumpora fedha Mkuu wa msafara kwa upande wa Chama cha Mpira wa Miguu Visiwani Zanzibar, ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Kassim Haji Salum, ambaye aliambatana na kikosi cha Zanzibar Heroes kilichokuwa kikishiriki katika michuano ya chalenji iliyomalizika juzi jijini Kamapal, Uganda.

Inadaiwa kuwa fedha hizo ambazo ni dola 10,000 walizopewa Zanzibar baada ya kushika nafasi ya tatu katika mashindano hayo, wachezaji hao wlizikwapua kutoka kwa katibu huyo muda mfupi mara baada ya kuweka saini ya kukabidhiwa fedha hizo.

Akizungumza leo mara baada ya kuwasili visiwani Zanzibar, Nahodha wa Zanzibar Heroes, Nadir Haroub 'Canavaro' amekiri kuzichukua fedha hizo huku akisema ni haki yao wachezaji huku akitolea mfano kwa baaddhi ya timu kuwa wamefanya kama wao na haoni kama wamefanya kosa.

Wachezaji hao inadaiwa wamegawana dola 500 kila mchezaji.

Akizungumzia sakata hilo Mkuu wa Msafara kutoka Serikalini kupitia Baraza la Michezo la Taifa la Zanzibar, Mussa Abdulrabi Fadhil, amesema kwa sasa Serikali haiwezi kuzungumza chochote mpaka watakapokaa kikao na kulitolea ufafanuzi suala hilo, "Sisi kama Serikali ni kweli tumesikia suala hilo lakini kwa sasa hatuwezi kulizungumzia kwa sababu tumekubaliana tutakutana na baadae tutao ufafanuzi juu ya suala hilo" amesema Fadhil.

Kwa upande wake kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Salum Baus Nassor, amesema amepata taarifa hizo ingawa hana uhakika na hilo ila kama ni kweli amekitaka chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kuchukua hatua kali dhidi ya kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na wachezaji hao.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa ZFA Taifa, ambaye ndiye kiongozi wa msafara wa chama hicho, Kassim Haji Salum, amekiri kupokonywa fedha hizo na kusema kikao cha kamati tendaji taifa ndio watakaoamua hatua zitakazochukuliwa dhidi ya kitendo hicho.

Akizungumza kwa hasira na kuahidi kuchukua hatua kali kwa viongozi wa kitendo ambao ni Nahodha wa Timu, Nadir Haroub 'Canavaro' na msaidizi wake Agrey Morris, Rais wa Chama cha Mpira wa miguu visiwani Zanzibar, (ZFA) Aman Ibrahim Makungu, amesema amesikitishwa na kitendo hicho kwa sababu yeye binafsi aliwasiliana na Canavaro kumsihi fedha wazirejeshe lakini akamjibu kuwa hawana imani na ZFA kwa madai kuwa wana kumbukumbu ya kutokupewa fedha zao.

Hata hivyo habari za ndani kabisa zinasema Serikali kupitia baraza la michezo la Zanzibar limewakataza kusema chochote viongozi walioondoka na timu kwa kutaka kuzuia sakata hilo kusambaa hususan kwa vyombo vya habari.

WAKATI HUO HUO: Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Salum Bausi Nassor ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kutekeleza ahadi aliyoiweka kuwa akishindwa kuchukua ubingwa anaachia ngazi.

BREAKING NEWS: HATIMAYE SIMBA NA AZAM WAFIKIA MAKUBALIANO YA KUGAWANA FEDHA ZA USAJILI ZA NGASSA

Baada msuguano wa takribani wiki mbili kuhusu nani hasa anastahili hasa kuchukua fedha za usajili wa mchezaji Mrisho Ngassa kati ya vilabu vya Simba na Azam, hatimaye leo hii umepatikana muafaka.

Viongozi wa pande mbili za vilabu hivyo wamekutana na kukubaliana kwamba watamuuza mchezaji Mrisho Ngassa kwenda klabu ya El Merreikh kwa ada ya usajili ya $100,000 na fedha hizo zitagawanywa kwa Simba na Azam FC.

Kwa upande wa mchezaji mwenye Mrisho Ngassa atapokea kiasi cha $75,000 kama gharama ya usajili kwa mkataba wa miaka miwili, na pia atalipwa kiasi cha $4000 kama mshahara kwa kila mwezi.

Simba na Azam zilikuwa zikigombana kuhusu nani hasa alikuwa mmiliki halali wa mchezaji huyu.

KUTOKA MAKTABA: SIKU KABURU ALIPOMTAMBULISHA MRISHO NGASA

HATIMAYE RAY C ARUDI KATIKA HALI YAKE YA ZAMANI BAADA YA KUSAIDIWA NA RAISI KIKWETE

Mh.Raisi Kikwete akiwa na mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati mwanamuziki huyo alipoenda kumtembelea Raisi na kumpa shukrani kwa kumsaidia kwenye matibabu ya juu ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua. Aidha Ray C alimueleza Raisi kwamba afya yake imeimarika na kwamba muda mfupi ujao atarudi kuendelea na kazi yake ya muziki. Kwa upande wa mama yake Ray C amemshukuru Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanae kwa kugharamia matibabu yote ya mwanae.

Raisi Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Ray C, Mama yake mzazi Ray C - Margreth Mtweve na aliyevaa nguo za pinki upande wa kulia ni dada yake Ray C - Sarah Mtweve. (Picha na Freddy Maro)

SAKATA LA TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR NA KUJIUZULU KWA KOCHA MKUU!

Ally Mohamed Mwandishi wa stori hii pia ni mtangazaji wa kipindi cha michezo cha Coconut fm.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar ' Zanzibar Heroes' wameingia katika kashfa nzito baada ya kudaiwa kumpora fedha Mkuu wa msafara kwa upande wa Chama cha Mpira wa Miguu Visiwani Zanzibar, ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Kassim Haji Salum, ambaye aliambatana na kikosi cha Zanzibar Heroes kilichokuwa kikishiriki katika michuano ya chalenji iliyomalizika juzi jijini Kamapal, Uganda.
Inadaiwa kuwa fedha hizo ambazo ni dola 10,000 walizopewa Zanzibar baada ya kushika nafasi ya tatu katika mshindano hayo, wachezaji hao wlizikwapua kutoka kwa katibu huyo muda mfupi mara baada ya kuweka saini ya kukabidhiwa fedha hizo.
Akizunga leo mara baada ya kuwasili visiwani Zanzibar, Nahodha wa Zanzibar Heroes, Nadir Haroub 'Canavaro' amekiri kuzichukua fedha hizo huku akisema ni haki yao wachezaji huku akitolea mfano kwa baaddhi ya timu kuwa wamefanya kama wao na haoni kama wamefanya kosa.
Wachezaji hao inadaiwa wamegawana dola 500 kila mchezaji.
Akizungumzia sakata hilo Mkuu wa Msafara kutoka Serikalini kupitia Baraza la Michezo la Taifa la Zanzibar, Mussa Abdulrabi Fadhil, amesema kwa sasa Serikali haiwezi kuzungumza chochote mpaka watakapokaa kikao na kulitolea ufafanuzi suala hilo, "Sisi kama Serikali ni kweli tumesikia suala hilo lakini kwa sasa hatuwezi kulizungumzia kwa sababu tumekubaliana tutakutana na baadae tutao ufafanuzi juu ya suala hilo" amesema Fadhil.
Kwa upande wake kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Salum Baus Nassor, amesema amepata taarifa hizo ingawa hana uhakika na hilo ila kama ni kweli amekitaka chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kuchukua hatua kali dhidi ya kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na wachyezaji hao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa ZFA Taifa, ambaye ndiye kiongozi wa msafara wa chama hicho, Kassim Haji Salum, amekiri kupokonywa fedha hizo na kusema kikao cha kamati tendaji taifa ndio watakaoamua hatua zitakazochukuliwa dhidi ya kitendo hicho.
Akizungumza kwa hasira na kuahidi kuchukua hatua kali kwa viongozi wa kitendo ambao ni Nahodha wa Timu, Nadir Haroub 'Canavaro' na msaidizi wake Agrey Morris, Rais wa Chama cha Mpira wa miguu visiwani Zanzibar, (ZFA) Aman Ibrahim Makungu, amesema amesikitishwa na kitendo hicho kwa sababu yeye binafsi aliwasiliana na Canavaro kumnasihi fedha wazirejeshe lakini akamjibu kuwa hawana imani na ZFA kwa madai kuwa wana kumbukumbu ya kutokupewa fedha zao.
Hata hivyo habari za ndani kabisa zinasema Serikali kupitia baraza la michezo la Zanzibar limewakataza kusema chochote viongozi walioondoka na timu kwa kutaka kuzuia sakata hilo kusambaa hususan kwa vyombo vya habari.
WAKATI HUO HUO: Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Salum Bausi Nassor ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kutekeleza ahadi aliyoiweka kuwa akishindwa kuchukua ubingwa anaachia ngazi

OFFICIAL: ANGALIA MABAO YOTE 86 ALIYOFUNGA LEO MESSI KATIKA MWAKA 2012


GERD MULLER: MWANAUME AMBAYE REKODI YAKE IMEVUNJWA NA LEO MESSI

Swarmed: West Germany's Gerd Muller trying to find a way through the Holland defence during the 1974 World Cup final
Gerd Muller akijaribu kufunga mbele ya ukuta wa Holland katika 1974 World Cup final


Gerd Muller alifunga mabao 85 katika mechi 60 akiichezea Bayern Munich na Ujerumani Magharibi mwaka 1972 - rekodi ambayo imekuwepo kwa miaka 40  sasa.

Hivi ndivyo Muller alivyojitengenezea rekodi yake.

BAYERN MUNICH
Bundesliga: Mabao 42 katika mechi 34
European Cup: Mabao 10 katika mechi 4
Cup Winners Cup: Bao 1 katika mechi 2
DfB Pokal: Mabao 7 katika mechi 6
DfB Ligapokal: Mabao12 katika mechi 5 
 
GERMANY

Euro1972: Mabao 5 katika mechi 4
Mechi za kirafiki: Mabao 8 katika mechi 3

Kipindi bora kabisa cha ufungaji: Mabao 16 katika mechi 8

Muda mrefu bila kufunga: Mechi 3 

Katika magoli yote 85 aliyofunga - alifunga yote bila mkwaju wa penati. 


KIKOSI KIPYA CHA TAIFA STARS: SELEMBE HAJAITWA - MCHA KHAMIS NDANI

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12 mwaka huu kuajianda kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia.

Katika kikosi hicho, wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Aishi Manula anachezea kikosi cha U20 cha Azam na timu ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), beki wa kushoto wa Azam, Samih Nuhu, beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid na mshambuliaji wa Azam, Mcha Khamis.

Pia kati ya wachezaji walioitwa, sita walikuwa kwenye kikosi cha Zanzibar (Zanzibar Heroes) kilichokamata nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Jumamosi jijini Kamapala, Uganda. Wachezaji hao ni Mwadini Ally, Nassoro Masoud Cholo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Samih Nuhu, Aggrey Morris na Mcha Khamis.

Kikosi kamili kilichoitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally na Aishi Manula (Azam U20). Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Samih Nuhu (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Amir Maftah (Simba), Issa Rashid (Mtibwa Sugar) na Kevin Yondani (Simba).

Viungo ni Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd Chuji (Yanga), Mrisho Ngasa (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Mcha Khamis (Azam), Salum Abubakar (Azam), Amri Kiemba (Simba) na Mbwana Samata (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- DRC).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Mwinyi Kazimoto (Simba).

ZAMBIA YATAJA KIKOSI CHA KUIVAA STARS
Kocha Mkuu wa timu ya Zambia (Chipolopolo) ambayo ni mabingwa wa Afrika, Herve Renard ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachoikabili Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa Desemba 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Zambia (FAZ), wachezaji hao ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.

Wengine ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.

MICHUANO YA KOMBE LA UHAI KUANZA KESHO
Michuano ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inaanza kutimua vumbi kesho (Desemba 11 mwaka huu) kwenye viwanja viwili tofauti.

Viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo ni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Viwanja vyote viko Dar es Salaam.

Timu hizo zimegawanywa katika makundi matatu ya michuano hiyo itakayomalizika Desemba 23 mwaka huu. Kundi A lina timu za Coastal Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Toto Africans.

Kundi B ni African Lyon, Azam, Mgambo Shooting, Polisi Morogoro na Simba, wakati timu za Kagera Sugar, Oljoro JKT, Ruvu Shooting na Yanga zinaunda kundi C.

Mechi za fungua dimba kundi A ni Coastal Union vs Tanzania Prisons (saa 2 asubuhi- Karume), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (saa 10 jioni- Karume). Kundi B ni African Lyon vs Polisi Morogoro (saa 3 asubuhi- Chamazi) na Azam vs Mgambo Shooting (saa 10 jioni- Chamazi).

Kundi C litaanza mechi zake Desemba 12 mwaka huu ambapo Kagera Sugar itacheza na Oljoro JKT saa 8 mchana- Karume wakati Yanga na Ruvu Shooting zitakuwa kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.

MJADALA: JE NI KWELI ASHLEY YOUNG ALINYIMWA GOLI DHIDI YA CITY?? USHAHIDI HUU HAPA

ASHLEY YOUNG

1355064703714 GIF: Ashley Youngs offside goal v Man City
PICHA YA MNATO

WAYNE ROONEY AVUNJA REKODI YA HENRY NA CHARLTON KWA MABAO MAWILI DHIDI YA MANCHESTER CITY

Magoli mawili aliyafunga Wayne Rooney jana dhidi ya Manchester City yalimfanya avunje rekodi ya Bobby Charlton ya kuwa mchezaji mwenye mabao mengi katika Manchester Derby kwa upande wa Man United.

Rooney ambaye jana pia alifikisha idadi ya mabao 150 ya Premier League na kuvunja rekodi ya Thierry Henry kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga mabao 150, Henry alifunga goli la 150 akiwa na miaka 28, wakati Rooney ametimiza mabao 150 akiwa na umri wa miaka 27 na siku 46.

FALCAO HATARI - AFUNGA MABAO MATANO PEKE YAKO, ATLETICO IKIIUA DEPORTIVO



[www.online-soccer.ru] Atletico Madrid 6-0... by all-goals

FRANSIC MIYEYUSHO AZIMA NGEBE ZA NASSIBU RAMADHANI


BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO AZIMA NG'EBE ZA NASSIBU RAMADHANI



Bondia Fransic Miyeyusho akionesha ufundi wake kwa kumtupia masumbwi Nassibu Ramadhani wakati wa Mpambano wao wa kugombania ubingwa wa WBF uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Miyeyusho alishinda kwa T.K.O ya raundi ya kumi picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
 
Bondia Mohamed Matumla  kulia  akimuhadhibi Doi Miyeyusho wakati wa mpambano huo usiku wa kuamkia  leo Matumla alishinda kwa K,O raundi ya pili Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Juma Fundi kushoto na Fadhili Majia wakioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki Majia alishinda kwa pointiPicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Miyeyusho kushoto akimwazibu mpinzani wake Nassibu Ramadhani kwa kumtupia makonde mazito wakati wa Mpambano wao wa kugombania ubingwa wa WBF uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Miyeyusho alishinda kwa T.K.O ya raundi ya kumi picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Miyeyusho akionesha ufundi wake kwa kumtupia masumbwi Nassibu Ramadhani wakati wa Mpambano wao wa kugombania ubingwa wa WBF uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Miyeyusho alishinda kwa T.K.O ya raundi ya kumi picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara kulia akimvisha mkanda wa ubingwa wa WBF bondia Fransic Miyeyusho baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani  kwa T.K.O raundi ya kumi kushoto ni promota wa mpambano huo Mohamed Bawaziri www.superdboxingcoach.blogspot.com
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara kulia akimpongeza Bingwa wa ubingwa wa WBF bondia Fransic Miyeyusho baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani  kwa T.K.O raundi ya kumi kushoto ni promota wa mpambano huo Mohamed Bawaziri www.superdboxingcoach.blogspot.com
bondia Fransic Miyeyusho akiwa amebebwa juu akiwa na mikanda miwili alioshinda baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani picha nwww.superdboxingcoach.blogspot.coma
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila  'Super D' kushoto akiwa na wadau waliojitokeza kuangalia mpambano huo

MJUE MESSI TOKA UDOGONI MPAKA LEO ANAPOVUNJA REKODI KIBAO


Lionel Andres Messi anazidi kuishangaza dunia kwa uwezo wake mkubwa karika soka. Lionel Messi aliezaliwa miaka 25 huko Rosario , Argentina. Messi ni mtoto wa Mzee Jorge Horacio Messi ambae alikuwa mfanyakazi wa kiwanda cha Chuma na mama yake  Celia Maria Cuccitti. Kwa upande wa Baba yake Messi anaasili ya Italy tokea mji mmoja unaitwa Ancoma, ambako ilikuwa ni asili ya babu yake aitwae Angelo Messi aliehamia Argentina mwaka 1883. Messi ana kaka wawili na dada mmoja.

Katika umri wa miaka mitano Leo Messi alianza kucheza soka katika club ya Grandoli. Hii ilikuwa klabu ya mtaani kwao iliyokuwa inasimamiwa na Baba ake. Mwaka 1995 Messi alihamia katika klabu ya Newell's Old Boys iliyopo katika mji wake wa Rosario. 
Messi akiwa na miaka 11

Akiwa na miaka 11 Messi aligundulika kukosa hormone za ukuaji. Baada ya kugundulika na tatizo hilo, Klabu ya River Plate moja ya klabu kubwa sana nchini Argentina ilitaka kumchukua ila ikashindwa kutokana na gharama za matibabu yake. Dola $900 ilitakiwa kila mwezi kwa ajili ya gharama za matibabu ya mtoto Messi. Carles Rexach mkurugenzi wa michezo wa Barcelona alikifahamu kipaji cha Messi baada ya kumuona akiwa katika majaribio na Klabu ya Llieda.
Raxach alikubali kumpa Messi mkataba na Barcelona, akiwa hana karatasi yoyote mkononi alimwandikia mkataba wa kwanza Messi katika Leso.
Hatimaye Barcelona walikubali gharama za matibabu ya Messi kwa masharti kuwa ahamie Hispania. Bila kipingamizi Messi na Baba yake wote wakahamia Hispania na Lionel akaanza kuitumikia klabu ya Barcelona akiwa katika katika shule ya vipaji ya  klabu hiyo iliyo maarufu sana kama La Masia. 
Messi na Macarena 

Inasemekana Messi amewahi kuwa na uhusiano na mwanadada Macarena ambae naye anatokea katika mji wa Rosario.  Messi alitambulishwa kwa Rosario na baba yake Rosario kipindi aliporudi kuuguza majeraha yake kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia 2006. Messi pia alishawahi kuwa na uhusiano na mwanamitindo wa Argentina mwanadada Luciana Salazaar.
Januari 2009 katika mahojiano ya kipindi "Hat-Trick Barca'" cha Canal 33 Messi alisema anauhusiano na mwanamke mmoja hivi (hakumtaja jina) na anafuraha kuwa nae swali hilo lilikuja baada ya Messi kuonekana katika sehemu mbalimbali na mwanadada Antonella Roccuzzo. Juni mwaka 2012 Messi akicheza mechi dhidi ya Ecuador alifanikiwa kufunga goli, alishangilia Goli hilo kwakuweka mpira ndani ya jezi yake kuashiria kuwa mpenzi wake ni mjamzito. Siku kadhaa baadae ikaripotiwa na vyombo vya habari kuwa mpenzi wake ana ujauzito wa wiki 12 (miezi 3). Mnamo Tarehe 2 Novemba mwaka 2012 mtoto wa kwanza wa Messi alizaliwa na kupewa jina la Thiago.


Messi akishangilia bao dhidi ya Ecuador




Messi ana ndugu wawili ambao waacheza mpira. Maxi anaichezea klabu ya Club Olimpia nchini Paraguay na Emmanuel Biancucchi. Pamoja na kuishi Spain kwa muda mrefu ila Messi hajaacha kupakumbuka Rosario. KIla mara hutembelea mji huu na pia ana mawasiliano na marafiki na ndugu kadhaa wanaoishi katika mji huo. Inasemekana wakati mmoja Argentina ilipokuwa ikifanya mazoezi mjini Buenos Aires. Messi aliendesha mwendo wa masaa matatu baada ya mazoezi kwenda Rosario kula chakula cha jioni na kulala na kesho yake kugeuza mapema kabla ya mazoezi. Messi bado anamiliki nyumba yao ya zamani ambako alikuwa anaishi na familia yake japokuwa hakuna mwanafamilia anayeishi hapo siku hizi.

  

Mwaka 2007, Messi ameanzisha Charity Foundation kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji.
Messi alitangazwa kuwa balozi wakujitolea wa UNICEF katika maswala ya kupigania haki za watoto. Barcelona nao wako nyuma wanamsaidia messi katika hili kwakuwa Barcelona na Messi wana uhusiano mzuri.


Messi alianza kuichezea timu ya wakubwa ya Barcelona tarehe 16 Novemba mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 16 na siku 145 katika mchezo wa kirafiki kati ya Barcelona na F.C Porto ya Ureno.
Miezi michache baadae Frank Rijkaard kocha wa barcelona kipindi hicho alimpatia Messi nafasi ya kucheza ligi ya Spain dhidi ya RCD Espanyol akiwa na Umri wa miaka 17 na siku 114 hivo kumfanya Messi kuwa mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo kuichezea Barcelona na mdogo kabisa kuichezea Barcelona katika ligi. Rekodi ambayo baadae ilikuja kuvunjwa na Bojan Krikic. Goli la kwanza la Messi katika timu ya wakubwa alilifunga dhidi ya Albacete Balompie mwezi Mei mwaka 2005. September mwaka huohuo Messi alipata urai wa Spain.
Baada ya hapo amekuwa akicheza kwa mafanikio makubwa. Messi katika kipindi hichi chote toka alipoanza kuichezea Barcelona amepata mafanikio mengi. Mafanikio Binafsi kama mchezaji na Mafanikio ya timu pia. 

Messi ameweza kuvunja rekodi nyingi ambazo ziliwekwa na magwiji wa soka wa zamani. Tukianzia katika klabu yake Messi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji anaeongoza kwa kufunga mabao mengi katika historia ya klabu hiyo akiwa na magoli 283 na pia ni mchezaji alieifungia Barcelona mabao mengi katika ligi ya Hispania uku akiwa na mabao 192. Messi anashikilia rekodi ya klabu yakufunga Mabao mengi kwenye msimu mmoja akiwa amefunga magoli 73 katika msimu wa 2011-2012. Messi anashikilia rekodi ya Barcelona ya mchezaji aliefunga magoli mengi katika mashindano ya ulaya akiwa na magoli 57 na 56 katika ligi ya mabingwa ulaya. Messi anaongoza listi ya mchezaji aliefunga magoli mengi katika Spanish Super Cup akiwa na magoli 10.
 
Messi ana rekodi ya kuwa mchezaji alieifunga magoli mengi kwa msimu mmoja katika michuano ya mabingwa ulaya akiwa na magoli 14, Messi huyuhuyu ana rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo mmoja wa ligi ya mabingwa ulaya akiwa amefunga 5 katika mechi dhidi ya Bayern Leverkusen msimu wa 2011-2012. Messi ana rekodi pia yakufunga hat-tricks nyingi ndani ya msimu mmoja akiwa amefunga hat-trick mara 8 msimu wa 2011-2012. Na bila kusahau Messi anashikilia rekodi ya Barcelona ya kufunga magoli mengi katika ile michuano ya klabu bingwa ya dunia akiwa na magoli 4.


Kwa ujumla Messi anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliefunga magoli mengi katika msimu mmoja wa ligi ya hispania akiwa amefunga magoli 50 katika msimu mmoja. anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika msimu mmoja wa ligi ya mabingwa huko akiwa a magoli 14 na pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliefunga magoli mengi ndani ya msimu mmoja akiwa na magoli 73 katika mashindano yote. Messi hajaishia hapo, Jana tarehe 09-Dec-2012 Messi amevinja rekodi ya mkongwe Gerd Muller ya mabao 85 katika mwaka mmoja ambayo ilidumu kwa miaka 40. Messi amefunga goli la 85 na 86 jana akiisaidia Barcelona kushinda mchezo wake dhidi Real Betis. Messi ameweka rekodi hiyo mpya uku akiwa na michezo mitatu mpaka mwisho wa mwaka. 


Messi bado ana rekodi zake binafsi. Messi ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka kwa miaka 3 mfululizo (209,2010,2011) na mwaka huu yuko katika ile tatu bora. Messi anashikilia tuzo ya mfungaji bora wa bara la Ulaya ya mwaka 2010 na mwaka 2012. Mshambuliaji bora wa ligi ya Hispania mwaka 2009,2010,2011,2012. Mchezaji bora wa ligi ya hispania mwaka 209,2010,2011,2012.  Mfungaji bora ligi ya Mabingwa ulaya mwaka 2009,2010,2011 na 2012. Man of the match fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 2011.
SOURCE:http://valetyno.blogspot.ca/